Uzezeta wa viongozi,wasomi wa kitanzania !

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Kuna wimbi kubwa la viongozi wa kisiasa na wasomi wa kitanzania kuingizwa mjini na watu wanaojidai kutoa tiba mdala.
Imekua ni kawaida kusikia mtu anatibu na kumaliza kabisa magonjwa sugu kama kisukari,vidonda vya tumbo,ukimwi n.k
mbaya zaidi watu wa kwanza kufika kwa waganga hawa ni viongozi wakubwa serikalini,wasomi wenye degree zao na wafanyabiashara wakubwa.

Huu ni ulimbukeni wa hali ya juu,yani kweli hamjui kama mnatapeliwa?kisomo chenu hakijawakomboa kabisa!
Najua baadhi yenu mpo humu jamvini,jirekebisheni jamani.
Nawasilisha;
 
Kama viongozi wanaamini katika tiba hizi ni vipi wataweza kuimarisha sekta ya afya nchini?
 
Nadhani sasa mliokwenda kwa babu mmeanza kuelewa ukweli juu ya tiba hiyo.
 
Ngumu sana kwa watu waliokwisha kata tamaa kuelewa!
Ni vigumu sana kwa watu waliozoea kuamini kila jambo wanaloambiwa kuamini kinyume na lile wasilotaka!
Sidhani kama inawezekana kwa anaejua kwamba anafanikiwa kutokana na maprofesa wa ndumba akakubali kwamba mafanikio yanatokana na bidii yake ya kazi................>>>>>
Tuwasomeshe watoto wetu kwa bidii kubwa kabisa ili wasije wakarithi ujinga kama huu tulionao leo!
Maana kukubali haya yanayotokea sasa nao ni UFISADI, tena UFISADI MBAYA KABISA WA NAFSI ZETU.
 
Siri itafichuka kwa nini askofu laizer alitoa support kwa hii tiba ya babu.askofu huyu ni msomi lakini tamaa yake ya fedha imemfanya kutetea ulozi.
 
Mtoto umetumwa eeeh, hebu pisha nisikupamie huko, acha watu tukapige kikombe, tukitapeliwa itakupunguzia nini kwendraaaaaaa.
 
Babu kawaingiza mjini watu kibao hapa TZ na nje ya nchi.Najua ni ngumu kwa watu wengi kuukubali ukweli huu ila ndo hivyo tena mmeshaibiwa kwa wale ambao mlishakwenda huko.Time will tell what will happen hapo baadaye...
 
Back
Top Bottom