Uzembe wa NECTA ndio sababu ya vijana wengi kuonekana wamefeli

sasa kama hakuna vitabu mtoto atasomaje????TIE wameandaa mwongozo,vitabu hawajatoa,inakuwaje????na hili kwa sasa lipo,syllabus ni mpya ila hakuna vitabu,,,,wizara,TIE NA NECTA hawajasema,,,,
Mkuu tuwekane sawa....NECTA hawahusiki kabisa na wala halijawahi kuwa jukumu lao kuandaa vitabu...awali lilikuwa Jukumu kuu la TIE lakini tulipolazimishwa na hao mabwana zetu tuliowabatiza jina zuri la Development Partners tukawanyangang'anya TIE jukumu hilo na kuruhusu soko huria .....baada ya kugundua tumekosea na tunakoelekea siko then kuna juhudi za kuwarudishia TIE jukumu lao la msingi kwamba wanapotoa Syllabus watoe na vitabu vya rejea/kiada...NECTA wao wakishapokea Syllabus toka TIE wanaandaa Examinations Format...kwamba tutatoa pepa ngapi....maswali mangapi ya mtindo gani nk....Sasa hapa ndipo walipolikoroga kwamba format imepunguza pepa 3 kuwa 2 lakini mfumo wa kukokotolea matokeo bado ukabaki unasoma pepa 3.......Ndio maana kwa wadau (wakuu washule zilizoathirika na tatizo hilo walielewa kirahisi kuwa tatizo lilitokea wapi... i mean chanzo cha tatizo na ufumbuzi ulipotolewa walielewa na ku-appreciate ila tulio nje...ambao wengine hata hawajawahi kufikia hiyo level ya elimu na wala hana hata mtoto wa rafiki yake na baba yake mkubwa aliyeathirika na tatizo hilo anapaza sauti na kulia kuliko wenye msiba.
 
Necta hua hawakosei katika kusahihisha mitihani na wala suala la vitabu sio lao. Na hata mtu aki spiel na kupeleka mwalinu wake amsahihishie bado matokeo hubaki yaleyale, pia naomba kuuliza kosa la ukokotozi katika mitihani limeshatokea mara ngapi tangu NECTA ianzishwe??.....
 
Acha kuitetea necta. Mle ndani kuna madudu. Mnaweza kuyapuuza madai ya Waislamu kwa vile tu yamepitia mkondo wa dini, lakini ukweli necta ni hovyo hovyo kupindukia tangu utungaji, kuhifadhi mitihani na kusahihisha ndo balaa. Usahihishaji ni hovyo kabisa, wanalipua. Mwanao akikumbwa na 'ajali' ya necta, utajua watu wanalalamikia nini!
 
Kwa kweli NECTA ni waonevu wakubwa na ni mafisadi wa fedha na haki kuliko hata tunavyofikiri kwa mfano angalia watu wanarudia mitihani yao ya 4m4 ndio utapata jibu, watu wangharamikia fedha nyingi kwenye usajili lakini kwenye usahishaji unakuta wanaburuza tu bila hata kujali, ningependa hiki kilio cha wanaroduia mitihani kingepatiwa jibu na kuwa mwisho kwenye bunge hili la bajeti na tabia hiyo ya kufelisha ikome kabisa, sabau hatuwezi kuendelea na hujuma za wazi wazi na watu tumekaa kimya.

Taarifa iliyotolewa inajitosheleza ni kosa la kiutendaji. Kwa msomi hatahoji zaidi ya kudai marekebisho yafanyike, anaelalamika akili hakuna.
 
NECTA wanamatizo sana kuna dogo alikuwa safi sana toka standard 7 mpaka form 4 matokeo ya form 6 dogo ana 4 mbaya, dogo alipoteza fahamu baada ya matokeo.
 
Taarifa iliyotolewa inajitosheleza ni kosa la kiutendaji. Kwa msomi hatahoji zaidi ya kudai marekebisho yafanyike, anaelalamika akili hakuna.

mkuu unaongea kwa kuwa huja declare hili swala kwako ama kwa mtu wako wa karibu xo nakushaur uwe unafanya research kwanza kabla ya kuongea, alafu unaposema kuwa anayelalamika akili hakuna sijui unakuwa una maana gani? Hilo ni tusi kubwa sana kwan umetiukana majority ya watu wanaofahamu fika kuhusu hili. Mungu akusamehe.
 
Usinikumbushe uonevu huu wa necta walimfelisha mwanangu form 6. Nikalipa sh 60,000 baada ya kukata rufaa, majibu ati 'majibu hayakubadilika', kumbe hata hiyo mitihani hawarudii kuisahihisha jamani wizi wa mchana kabisa! Lakini swali ni hili, inakuwaje hakimu unayemlalamikia hakutoa hukumu ya haki ndo ukate rufaa kwake? Kiwepo chombo kingine mbali na necta ambacho watahiniwa wanaweza kukata rufaa.

Wabongo bana ....tumeshadhani kuwa kukata rufaa ni sehemu ya kufanya mitihani...jitu jingine halijaandika chochote lakini oooh baba nimeonewa nakata rufaa....wewe unakata rufaa sasa unataka NECTA ndio wamuandikie majibu?? unasema wamemfelisha au kafeli??kwani hakuna wanaofaulu?? kama kazi ya NECTA ni kufelisha hao wengine walifaulu vipi?
Tusitumie makosa ya kawaida ya kiutendaji kuonesha kuwa chombo hiki nyeti hakifai kiasi hiki kwasababu binafsi....Ni wangaqpi tunarukwa kwenye Payroll za hazina na wala hatuandiki humu??
 
NECTA wanamatizo sana kuna dogo alikuwa safi sana toka standard 7 mpaka form 4 matokeo ya form 6 dogo ana 4 mbaya, dogo alipoteza fahamu baada ya matokeo.

Kumbe form four alifanya vizuri sio?? sasa alifanya mtihani wa NECTA AU NACTE? iweje sasa afike form 6 afelishwe na chombo kile kile ilihali form 4 alifaulu?? huoni kuwa mlimpa kichwa akategemea historia kufaulu?? Ngoja tu niondoke kwenye hili jukwaa maana huku ni kuinajisi elimu...kila mtu hata asiyejua lolote kuhusu elimu ni msemaji na mkosoaji kuhusu elimu...
Wengine mnadanganywa na alama za juu wanazopata watoto wenu toka kwenye shule za binafsi ili muendelee kuwapelekea mamilioni ya pesa akikutana na pepa ya NECTA anaangukia pua...eti alikuwa anaongoza darasani...sasa si unaweza kuongoza kundi la wajinga utajiita pia kipanga?? kwananini? Sikatai kuwa kama binadamu wanaweza kufanya makosa ukizingatia pia matumizi ya teknologia hayaruhusu sana human interraction kwani katika computa kuna lugha maarufu inayosema Gabbage in Gabbage Out na kwa ufaham,u wangu kwa kusoma statement ya Kawambwa ndicho kilichofanyika sasa sijui kwnini wengine tunataka kusingizia hata madhaifu yetu kuwa ni sehemu ya utendaji wao.
 
Ivi matokeo ya islamic knowledge yanasaidia nin?

kama una busara jiulize pia matokeo ya bible knowledge yanasaidia nini ?
mimi ninachojua matokeo haya ya masomo ya dini yanasaidia tu mtu kuonekana ana division 1 au 2, yaani yanaongeza points, zaidi ya hapo hayana kazi yoyote, kwa sababu kwenye selection ya kwenda chuo huwa hayahesabiwi wanapotafuta points. kwa maana hii nadhani ni kwa ajili ya kupamba cheti chako tu lakini hayana maana yoyote kwa future use
 
RPRESSIslamicstudiesFinal1.pdf

Tamko la Serikali hili hapa.
Pongezi kwa aliyelisaini.Vinginevyo asingekanyaga msikitini tena!
 
Usinikumbushe uonevu huu wa necta walimfelisha mwanangu form 6. Nikalipa sh 60,000 baada ya kukata rufaa, majibu ati 'majibu hayakubadilika', kumbe hata hiyo mitihani hawarudii kuisahihisha jamani wizi wa mchana kabisa! Lakini swali ni hili, inakuwaje hakimu unayemlalamikia hakutoa hukumu ya haki ndo ukate rufaa kwake? Kiwepo chombo kingine mbali na necta ambacho watahiniwa wanaweza kukata rufaa.

Congrats!!!! Haya ndiyo mawazo tunayoyatafuta ili tusonge mbele
 
kuanzia mwaka huu masomo ya arts form V na VI yamebadilishwa(kwenye format ya mitihan ya NECTA),syllabus inayotumika ni mpya imeanza 2009,ajabu ni kwamba NECTA na TIE hawajatoa vitabu,pia kuanzia mwakani watu wa sayansi wataanza kufanya mitihan kwa syllabus mpya

Unayosema ni kweli!! Walimu wanahangaika mno kufundisha watoto kwa kuunga unga vitabu vya kudhania dhania wao wenyewe. Lakini Necta wanacho jua ni 35,000/= za mitihani, kana kwamba hawapewi bajeti na serikali.
 
Kwa kweli NECTA ni waonevu wakubwa na ni mafisadi wa fedha na haki kuliko hata tunavyofikiri kwa mfano angalia watu wanarudia mitihani yao ya 4m4 ndio utapata jibu, watu wangharamikia fedha nyingi kwenye usajili lakini kwenye usahishaji unakuta wanaburuza tu bila hata kujali, ningependa hiki kilio cha wanaroduia mitihani kingepatiwa jibu na kuwa mwisho kwenye bunge hili la bajeti na tabia hiyo ya kufelisha ikome kabisa, sabau hatuwezi kuendelea na hujuma za wazi wazi na watu tumekaa kimya.

Kweli kabisa mkuu Wamewafanya hawa wanaorudia mitihani kama chanzo cha kipato yaani wanakufelisha kwa maksudi ili urudie kujisajili wapate tena pesa na sijui zinaenda wapi.
 
1.hakuna watu ninawachukia kama necta
2.hakuna watu ninawachukia kama bodi ya mikopo

hawa jamaaa wanahuhumu sana vijana wa kitanzania makusudi natamani siku nisikie alshababu,boko haram,
au uamsho wamejiitoa muhanga na kuua hawa watu kwenye hizi secta....ili kuwakomboa watanzanis
 
Back
Top Bottom