Uzembe wa Idara ya Mawasilliano Ikulu na Mgogoro wa Ukweli

unamaanisha kuwa inaongozwa na Nguvu za Giza?

Salva should Go na sitafute Mchawi hapa
mkuu, Gembe sina maana hiyo
yaani hawa jamaa, wameiweka nchi chini ya meza kiutawala, we ukiingia sebuleni utaangali
juu ya Meza lakini mabo yote uvunguni mwa meza, maana asiyependa wengine wajue mambo
mbali mbali ya kihabari juu uongozi wake ujue ni muovu, vipi atoe sirize?
 
Mwanakijiji

Wakati mwingine huwa najiuliza labda na hili linahitaji wawekezaji?

Tumepiga kelele toka 2007 kuhusu hili ila hakuna chochote

Au ni moja ya masuala yanayohusu usalama wa Taifa?

Imefikia wakati wa watu kuwajibika sasa.

Kama wameshindwa kutengeneza tovuti ya ikulu waache kazi!

Mkuu I salute!! Mimi nafikiri tungelianza kuubinafsha uongozi kwanza halafu baade rasilimali maana hakuna tunalofanya. Tunazunguka palepale tulipo bila kukoma. What a mess!!
 
Ngoja nimtumie text mkuu na ninatuma hiyo kwa email uliyonipatia. Thanks

Kipindi cha Mkapa kulikuwa na tovuti ya ikulu sasa sijui ilipotelea wapi?ama aliondoka nayo?na kwa kuwa yuko msumbuji anaweza kumuonesha Ben SMS yako na naona kama wanazungumza hivi

Muungwana:Unajua Mwanakijiji hniachi kabisa,jana anasema nipo na tetere leo kaja na hili la tovuti

BM:Huyu jamaa kipindi changu alikuwa hanisumbui kabisa, sana sababu nilikuwa najua jinsi ya kuwabana waandishi wa habari wa bongo(vicheko).Kidogo yule rafiki yangu ulimwengu alitaka kulewa sifa nikamshughulikia akatulia..

Rukhsa:Hivi huyu Mzee Mwanakijiji huwa ni nani,huwa inanipa shida sana sababu ana habari nyingi zaidi yangu!

Muungwana:Mie nimeshindwa kabisa sababu ya utandawazi bana,ukisema hili wanasema ndege haipai,Lowassa alitaka kulia na huyu jamaa..Nikamwambi hamwezi mwache..ila wapo kina kibanda wale,walikuwa watu wangu ila wananisumbua sana..silali

BM:Jitahidi kufanya wanayokuagiza,Hili suala la tovuti mbona dogo sana,ile niliyoicha iko wapi?

Muungwana:Embu naomba mniitie Salva huko nje,Kila siku nimekuwa naiulizia hii tovuti wanasema inafanyiwa marekebisho...eeh kwani Mzee Mkapa inachukua muda sana?

BM:Labda unasafiri sana na haupati muda wa kuitazama ili uizundue...Tovuti siyo jambo kubwa,mie ninayo na kale kafoundation kangu ilichukua wiki moja tu na iko up todate

Rukhsa:Mie hayo mambo ya tovuti huwa nayasikia kwa Hussein tu,jitahidini mmwawekee ili walizike!

Muungwana:sawa Mzee Rukhsa..Mzee Mkapa,he he ..ooh unajua,hapana mzee ila siku ile ya WEF ulimwaga cheche(Vicheko)..mambo ya watu kuwa omba omba ila tunajitahidi kuweka mambo sawa..nadhani huu mswaada mpya wa madini utasadia kupunguza makali

Salva:Mzee Unasemaje?

Muungwana:Rafiki yako Mwanakijiji anauliza ile website yangu lini itakamilika?na ile ya Tanzania mbona ina teknolojia ya zamani

BM:toka niiche ile mpaka leo hamjaibadili..This does not make sense ata all..

Salva:Mzee tuko kwenye hatua ya Mwisho kuikamilisha,nadhani tukirudi Dar basi tutafanya uzinduzi

Muungwana:Mwanakijiji kaomba nikufute kazi,sasa nasema usipokamilisha hili tusilaumiane meble ya safari

Salva:Huyu Mbayuwayu kila siku anakufuata fuata tu mbona haoni mazuri unayofanya

BM:Tovuti ni jambo muhimu sana sababu linakufanya unakuwa karibia na wananchi ,wakati huo huo wawekezaji wanaweza kupata habari mbali mbali kuhusu Tanzania.Jakaya Naomba namba ya mwanakijiji

Muungwana:hii hapa,hii lazima nimjibu na hata suala la tetere niamjibu pia..alinichekesha sana huyu kijana

BM:nilisoma,nililetewa na Mama Anna nikashtuka yamekuwa haya..Ila tovuti iwepo bana na Masuala ya walimu angalia jinis ya kuyafanyia kazi ili wasipige kelele

Rukhsa:Kweli kabisa,hili ni la Muhimu ili kusaidia kujenga Chama chetu

Muungwana:Nalifanyia kazi,unajua kama nisingekuwa mkali wale kina Mgaya wangeaharibu mkutano,sasa ikabidi nimwite Mwamunyange pale na nikawapiga mkwara kidogo ila najua jinsi ya kusawazisha...tutayamaliza haya

wangonga glass..Cheers!

NOTE:Maelezo hayo yote ni ya kubuni tu sababu hamkawiii
 
Ndugu yangu naomba unihakikishie hayo uliyoandika hapo juu kwa kumhusisha salva na premi moja kwa moja katika tuhuma zako , hao watu ni waajiriwa wana majukumu mengine yanayohusiana na mawasiliano lakini siamini kama majukumu yao yanahusiana na teknohama moja kwa moja kutokana na mkataba wao wa kazi eneo hilo , hili ni jukumu la idara zingine za kiserikali zinazotakiwa kusimamia masuala ya teknohama pamoja mawasiliano kwa ujumla sasa tunatakiwa kujua idara hii na wakuu wake ni wakina nani , kina nani walipewa kazi ya kusimamia masuala ya teknohama eneo hili .

Masuala ya kuendesha tovuti yanahusiana na mambo mengi sana ndio maana huko nyuma kwanza tuliwahi kushauri kuwe na mfumo mmoja wa kueleweka wa tovuti zote za serikali nchini Tanzania hizo tovuti ziwe chini ya kitengo kimoja cha taasisi inayohusika na masuala ya teknohama nchini chini ya wizara ya mawasiliano kwa kushirikiana na kampuni zingine za sekta binafsi ambazo zinaweza kutoa changamoto kwenye masuala ya kiteknologia .

Kwahiyo tukiwa na vitu kama hivyo mtu yoyote anayechaguliwa kuingia kwenye serikali na idara zake italazimika kuingia mkataba na hiyo taasisi kuu ya teknohama ambayo itakuwa na viidara vidogo kwenye kila wizara serikalini pamoja na sekta binafsi .

Tukiwa na mipango mizuri naamini haya yote yanaweza kutimia lakini ni hadi pale tutakapoweka tofauti zetu pembeni na kuamua kufanya kazi kama taifa kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo .

Kuna watu wanafanya kazi kwa muda maalumu uongozi Fulani ukiisha basi nae anaacha kila kitu kwa wengine bila maelezo yoyote kwa hao wengine wanaokuja hii tabia tuache .
Haya bwana safari njema. Kidole kimoja hakivunji chawa. Lakini nani anayemkimbiza mwenzake asimsogelee karibu, wewe au hawa wahusika na uongozi wa nchi yetu maana ni kweli kabisa kama tunataka kufika salama ni muhimu kuunganisha nguvu. But it takes two to tangle...bila kuwa na partner wa kufanya naye maendeleo hilo halitawezekana.
 
Kuhusu Sava na Internet: Ineaelezwa kuwa wakati Salva akiwa Mhariri Mkuu wa Habari Corporation alikuwa hapendi matumizi ya internet kwa wahariri. Mara kadha alikuwa akitishia kuzi-disable computer zote za newsroom zilizokuwa na huduma hiyo eti kwa sababu wahariri wanakalia ku-download tu news and other info kutoka Internet, badala ya kuandika zao wenyewe.

Ingawa kwa upande mmoja alikuwa na ka-sababu, lakini ilifahamika pia kuwa yeye mwenyewe hakuwa well-conversant katika matumizi ya Internet na hii ndiyo hasa ilimfanya kuipa mgongo teknolojia hiyo.

Hicho kitengo cha Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu anashindwa kukimudu kikamilifu, kwani inaelezwa kuwa hata taarifa za ikulu (press releases) husambazwa kwenye magazeti mbali mbali kwa lugha moja tu -- Kiswahili, hata kama baadhi ya magazeti hayo ni ya Kiingereza. Inashangaza idara ya Ikulu kukosa watafsiri - lakini inasemekana kuwa hii inatokana hasa na yeye mwenyewe Salva kutoimudu lugha ya kiingereza sawasawa -- hasa wiritten.

Kutolea mfano tu, press releases zote zitokazo TAMWA huwa zinatumwa katika lugha zote mbili -- kiswahili na Kiingereza.
 
Ndugu yangu naomba unihakikishie hayo uliyoandika hapo juu kwa kumhusisha salva na premi moja kwa moja katika tuhuma zako , hao watu ni waajiriwa wana majukumu mengine yanayohusiana na mawasiliano lakini siamini kama majukumu yao yanahusiana na teknohama moja kwa moja kutokana na mkataba wao wa kazi eneo hilo , hili ni jukumu la idara zingine za kiserikali zinazotakiwa kusimamia masuala ya teknohama pamoja mawasiliano kwa ujumla sasa tunatakiwa kujua idara hii na wakuu wake ni wakina nani , kina nani walipewa kazi ya kusimamia masuala ya teknohama eneo hili .

Masuala ya kuendesha tovuti yanahusiana na mambo mengi sana ndio maana huko nyuma kwanza tuliwahi kushauri kuwe na mfumo mmoja wa kueleweka wa tovuti zote za serikali nchini Tanzania hizo tovuti ziwe chini ya kitengo kimoja cha taasisi inayohusika na masuala ya teknohama nchini chini ya wizara ya mawasiliano kwa kushirikiana na kampuni zingine za sekta binafsi ambazo zinaweza kutoa changamoto kwenye masuala ya kiteknologia .

Kwahiyo tukiwa na vitu kama hivyo mtu yoyote anayechaguliwa kuingia kwenye serikali na idara zake italazimika kuingia mkataba na hiyo taasisi kuu ya teknohama ambayo itakuwa na viidara vidogo kwenye kila wizara serikalini pamoja na sekta binafsi .

Tukiwa na mipango mizuri naamini haya yote yanaweza kutimia lakini ni hadi pale tutakapoweka tofauti zetu pembeni na kuamua kufanya kazi kama taifa kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo .

Kuna watu wanafanya kazi kwa muda maalumu uongozi Fulani ukiisha basi nae anaacha kila kitu kwa wengine bila maelezo yoyote kwa hao wengine wanaokuja hii tabia tuache .


Kabla ya kuanza kuwa na ma-department na ma-idara ya kushughulikia hizo tovuti za serikali ni lazima kurekebisha mfumo mzima.Hawa watu wa ikulu ya Tanzania hasa wa mawasiliano wameamua kutojifunza toka kwa nchi nyingine.Yaani kabla ya kuanza kufikiria mambo makubwa inabidi lipite fagio la chuma kuondoa hawa baadhi ya watu ambao Mwanakijiji anawazungumzia....kama wewe ni boss na unashindwa kuratibu mambo madogo madogo kama haya hata tukiwa na idara kumi bado hatutofanikiwa kwa sababu hapa suala si teknolojia peke yaake yaani suala la kutengeneza na kuzi-maintain hizo websites yaani tuna tatizo kwenye "integrity"(sijui utasema kwa kiswahili fasaha hapo!) ya hizo taarifa...yaani mambo ambayo yanaripotiwa wakati mwingine yanakuwa si hasa yaliyotokea na hili ni tatizo hata ukiweka idara kama huna watu makini ni upuuzi mtupu.Ndani ya serikali tayati kuna wataalamu wa Teknohama wa idara na wizara mbalimbali...ingewezekana kufanyika mobilization tu kuweka kupata watu wa kushughulikia haya mambo tatizo hawa mabosi wa mawasiliano sio creative tatizo linaanzia hapo na wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa hiyo hawapaswi kuwa kazini wakati huu!
 
Mwanakijiji,

Unapigia vyura vya Ikulu na wapambe wao kinubi. Wao wanalia yangu yangu, yangu yangu wakigombea sehemu ya kumi ya mradi!
 
Mzee Mwanakijiji,

Unanipandisha hasira na hayo mambo .... samahani sana sijisikii kusoma huo uchafu please... kuna mengine ya www.wananchi.go.tz :angry: maaahadi kibao... performance...mmmmh:angry:

:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:
 
Mzee Mwanakijiji,

Unanipandisha hasira na hayo mambo .... samahani sana sijisikii kusoma huo uchafu please... kuna mengine ya www.wananchi.go.tz :angry: maaahadi kibao... performance...mmmmh:angry:

:angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry::angry:

kasheshe hiyo ya wananchi ndio usiseme jamaa wamekula hela hadi nawaonea huruma; niliuliza swali imepita miaka miwili sijawahi kupata jibu!!
 
Mkuu Shy, unazungumzia mfumo wa uendeshaji, lakini huo si mfumo wa kiutendaji!!!!!!!!!!!!!!!!!!
KWANZA JE TOVUTI HIZO ZIKO SAWA??? Kama hapana basi MK ana hoja. Na tushughulikie hoja ya TOVUTI BOMU.
Mifano ya Kiutendaji na uwajibikaji ipo, kwa mfano,
Mambo serikalini yakienda ovyo unamwuliza Raisi, kwa sababu ndie mkuu wake. Unapomwuliza swali Waziri bungeni, si kwamba yeye ndio anayefanya, HAPANA wako watendaji wake. KAzi yake ni kuwauliza, halafu atoe majibu.
Hivyo kama Salva ndie mkuu wa mawasiliano, hapa anaulizwa mbona anawasiliana bila TIJA, kizamani na kwa kuchelewesha taarifa na kutoa taarifa finyu. Sasa yeye afanyeje atoe majibu au afanyie kazi si jukumu la aliye mwuuliza.
Unapozungumzia utawala bora ni pamoja na kujua nani muwajibikaji hata kama mtendaji kosa ni mwingine. Raisi mstaafu Mzee Mwinyi alijiuzulu alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani si kwa sababu yeye alihusika na mauaji yale kule Shinyanga, la hasha, Mkuu wa Mkoa naye akajiuzuru, pia hakuhusika moja kwa moja la hasha, WALIWAJIBIKA kwa mambo hayo kutokea kwenye sehemu ambazo wao ndio wakuu wake.
Turudi kwenye MADA, Mkuu wa Mawasiliano IKULU afanye kazi yake, ajibu hoja zake, na naamini yumo humu jamvini, basi asingoje.
Tuige nchi za jirani wanakwenda mbio katika teknohama kama msemavyo, faida zipo.
Tujiulize maswali tu, JE HAYO ANAYOYASEMA MWANAKIJIJI KUHUSU TOVUTI HIZO NI KWELI - Kama ni kweli je NINI KIFANYIKE, au kuna marekebisho katika uelewa wake kuhusu mwonekano wa tovuti???????????????? hata kama hajui ni wajibu wa wataalamu kutengeneza. Kwani SI LAZIMA UWE MPISHI MZURI KUJUA CHAKULA KIBAYA, NA UKISEMA CHAKULA HIKI KIBAYA, SI SAHIHI KUAMBIWA ATI MBONA WEWE HUJUI KUPIKA, WANAOJUA KUPIKA WAPIKE CHAKULA KIZURI TULE.



Ndugu yangu mimi nimezungumzia masuala ya tovuti unapokuja kwenye masuala ya tovuti yale hayaingizwi tu unavyotaka ni tovuti inaandaliwa kuna kuwa na watu wa kuendesha tovuti sio kama unavyofikiria wewe kwahiyo inabidi kuandaliwa idara maalumu ya masuala hayo itakayoshugulikia tovuti zote za kiserikali , Ushauri kama huu niliwahi kuutoa kwenye mada moja kwenye www.ethinktanktz.org tembelea hapo tafuta sikumbuki ilikuwa kichwa cha habari gani ila ni miaka karibu 3 iliyopita , ushauri huu ni kwa ajili yako na wengine wanaosoma na kuandika kwa kushutumu serikali bila kuwa na taarifa za kutosha kama ulivyofanya hapo kwenye mada hii ni aibu kweli .

Huo utawala wa kifisadi unausemea wewe mwenyewe huyu raisi ni wetu sote na serikali ni mimi na wewe lazima tuhakikishe tunafanya kazi pamoja kuhakikisha tunaitoa jamii yetu sehemu moja katika maisha kwenda nyingine bila kuangalia tofauti zetu za kidini , chama wala makundi yoyote hii ni nchi yetu sote haina hati miliki
 
Kabla ya kuanza kuwa na ma-department na ma-idara ya kushughulikia hizo tovuti za serikali ni lazima kurekebisha mfumo mzima.Hawa watu wa ikulu ya Tanzania hasa wa mawasiliano wameamua kutojifunza toka kwa nchi nyingine.Yaani kabla ya kuanza kufikiria mambo makubwa inabidi lipite fagio la chuma kuondoa hawa baadhi ya watu ambao Mwanakijiji anawazungumzia....kama wewe ni boss na unashindwa kuratibu mambo madogo madogo kama haya hata tukiwa na idara kumi bado hatutofanikiwa kwa sababu hapa suala si teknolojia peke yaake yaani suala la kutengeneza na kuzi-maintain hizo websites yaani tuna tatizo kwenye "integrity"(sijui utasema kwa kiswahili fasaha hapo!) ya hizo taarifa...yaani mambo ambayo yanaripotiwa wakati mwingine yanakuwa si hasa yaliyotokea na hili ni tatizo hata ukiweka idara kama huna watu makini ni upuuzi mtupu.Ndani ya serikali tayati kuna wataalamu wa Teknohama wa idara na wizara mbalimbali...ingewezekana kufanyika mobilization tu kuweka kupata watu wa kushughulikia haya mambo tatizo hawa mabosi wa mawasiliano sio creative tatizo linaanzia hapo na wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa hiyo hawapaswi kuwa kazini wakati huu!

nilifanya my graduate research kwenye idara moja nyeti hapo serikalini ... nilihuzunika sana! kwa kweli hawa watendaji wetu wa serikali ni tatizo kubwa sana ... director mzima wa IT hajui hata coordination ya IT departments zake?? hakuna networked communication between departments, and between ministries ... kila kitu kiko manually processed ingawa wana kila equipment ya kuwawezesha ku-automate processes zao; nikajiuliza hawa watu wanafanyakazi vp?? no wonder makampuni ya kihindi ya IT yanafufuka kila kukicha sababu wana soko la uhakika la kuwauzia hawa jamaa teknolojia zilizopitwa na wakati! .... and the guys were so relaxed in their PC!! Hawa watu wanasafari kila leo kwenda ulaya, asia na america kwenye makongamano, warsha, kozi fupi na mengineo ... sasa kila siku najiuliza mbona hakuna madiliko?? wanaendaga kufanya nini huko?? Hv kwanini serikali inaingia gharama zote hizo kuwahudumia watu kama hawa?? ... manake kumlipa mtu mmoja kwenye level ya director si mchezo ati!! baadae nikaja kumuona jamaa (huyo director mchovu) yuko mjengoni anawasilisha mada kwa wabunge... kweli nilichoka!! Mungu atusaidie tu!
 
Mzee mwanakijiji umefanya kitu kizuri saaana kuwakumbusha.
Ndugu yangu naomba unihakikishie hayo uliyoandika hapo juu kwa kumhusisha salva na premi moja kwa moja katika tuhuma zako , hao watu ni waajiriwa wana majukumu mengine yanayohusiana na mawasiliano lakini siamini kama majukumu yao yanahusiana na teknohama moja kwa moja kutokana na mkataba wao wa kazi eneo hilo , hili ni jukumu la idara zingine za kiserikali zinazotakiwa kusimamia masuala ya teknohama pamoja mawasiliano kwa ujumla sasa tunatakiwa kujua idara hii na wakuu wake ni wakina nani , kina nani walipewa kazi ya kusimamia masuala ya teknohama eneo hili .

Shy 1000 % watu wa idara ya mawasiliono wanahusika na CONTENT zote zinazotlewa kwa umma. TEKNOHAMA anayosema mwanakijiji sio tu INFASTRUCTURE ( NETWORK, SERVER , DATABASE, WEB PAGE, etc)

Hata kama ikulu ina infastructure za TEKNOHAMA za kisasa zinazongaliwa na kusimamiwa na wataaalmu wenye uwezo wa juu kama END PRODUCT ina matatizo basi ni KAZI BURE

Kwa hiyo namuunga mkono mwanakijiji na kina Salva na idara yake wanahusika.
 
Lazima tukubali kwamba katika jamii yetu ya kitanzania, watumishi walio wazembe kupita wote ni watumishi wa serikali. Jaribuni kufanya uchunguzi kidogo na mtakubali hilo. Hawa watu wamesoma lakini hawajaelimika kwa kuwa kuelimika kunapimwa na faida ya elimu hiyo kwa jamii.
Uzembe na kutoelimika huko hakupo ikulu pekee bali kumeenea wizara na idara zote.
Watumishi wengi wapo kifisadi, kindugu, kirafiki nk., Hapo unategemea ufanisi kweli?
 
Nilikuwa natafuta namna moja ya kuelezea mgogoro ambao ninao na Idara hii nyeti ya Ikulu kwa muda mrefu. Mgogoro ambao tayari umeshawahi kujadiliwa hapa mara kwa mara lakini itoshe leo niuweke kwa maneno machache ili maana yake isije kupotea katika maneno mengi. NI mgogoro wa maono, uongozi, utendaji, uwajibikaji na zaidi ya yote ni mgogoro wa ukweli.

Kuna uzembe uliokubuhu ambao unaakisi tu matatizo ambayo tunayo kwenye idara nyingine mbalimbali za seriklali.

1. Tumelalamika miaka nenda miaka rudi sasa kwanini Ikulu haina mtandao mzuri kiintaneti wenye kusheheni taarifa mbalimbali za shughuli za Rais na hivyo kufanya kuwa chanzo cha kuaminika cha habari kwa vyombo vingine vya habari. Ninaamini wao ndio walipaswa kusimamia mambo hayo ya TEKINOHAMA hapo Ikulu ili kuhakikisha Ikulu ya Tanzania ina mtandao wa kisasa wa habari.

Tovuti ya http://www.statehouse.go.tz haipo kwa muda mrefu sasa na ukienda Ikulu.go.tz utashangaa kuambiwa ni "Tanzania Building Agency"! na tumelalamikia hili kwa muda mrefu. Ili kuweza kuelewa ninachozungumzia angalia tovuti za Kenya - statehousekenya.go.tz, Uganda-statehouse.go.ug, au Rwanda (wanayo ya Paul Kagame, na ya Serikali).

Kwanini vitu hivi ni muhimu? sababu moja ni kwamba vinakuwa ni kiungio cha haraka na cha uhakika katika ya wananchi na Rais wao na Ikulu yao. Badala ya wananchi kusubiri kila siku magazeti yaeleze nini Rais kafanya au nini kimetokea Ikulu leo au kitatokea kesho, Ikulu ingeweza kabisa kuwa na habari hizi kila siku na kwenye tovuti ambayo ni rahisi pia kukisiwa.

Lakini kinachouudhi ni kuwa Idara hii inadaiwa kuwa imetengewa karibu dola laki mbili! kwa ajili ya kuendeleza tovuti ya Ikulu! Sasa miaka minne na hawa watu wameshindwa kufanya jambo dogo linalochukua masaa 24 tu?

2. Tovuti ya Tanzania.go.tz; sasa baada ya hilo la hapo juu tatizo jingine ni ni tovuti rasmi ya serikali yetu, yaani ile ya anuani hiyo hapo juu. Japo tovuti hii imekuwa ikiwekewa taarifa mpya mara kwa mara lakini ni mojawapo ya tovuti zenye sura mbaya, mpangilio mbaya na inatumia teknolojia ya karibu miaka 15 ya nyuma katika mambo ya internet.

NI sawasawa na watu wanaoisimamia wamefungwa katika kile kinachoitwa na rafiki yangu Kiranga kuwa ni time warp na hawawezi kutoka humo na matokeo yake wanatuzungusha mle mle. Lakini kinachoudhi zaidi ni kuwa tovuti hii ndio imegeuka kuwa ni tovuti ya Ikulu! NI kama hawa kina Salva, Premi (huyu mdada tena nina kesi naye nyingine.. na atajibu siku moja) wanaishi katika sayari nyingine hivi. Tovuti hii ya serikali ingekuwa inasimamiwa na Wizara ya Habari na utamaduni badala ya Ikulu! Ingekuwa ni mahali ambapo mtu akitaka kujua kuhusu Tanzania au mahali pa kuanzia kuhusu utendaji wa serikali ya Tanzania au vyombo vyake mbalimbali angeweza kwenda hapo.

Halafu cha kukera zaidi badala ya kuwa na tovuti mbili zenye lugha mbili tofauti (Kiswahili na Kiingereza) basi wameamua kuchanganya tu mumo kwa mumo; kuna nyaraka za Kiingereza, zipo za kiswahili zote zimesambazwa ukurasa mzima bila kufuata mpangilio wowote wa kimantiki au maudhui. Wenyewe wanaita "Online Gateway"! my foot!

3. Katika tovuti zao zote na habari zote zilizopo inaonekana hawa jamaa wa Ikulu (Mawasiliano) hawajawahi kukaa chini na kusema waanze kuweka kumbukumbu za taarifa mbali mbali za serikali yetu kwenye mtandao hasa taarifa ambazo zimekuwa declassified na ni haki ya wananchi kuzijua (nyingi zimepita tayari miaka 30 ya kawaida ya kuzizuia). Kuna mambo mengi ambayo wasomi wetu wangeweza kuyapata kwa kupata taarifa hizo mbalimbali za mwanzo wa jamhuri yetu, kwanini Ikulu isiziweke hadharani kwa mtandao ili kila mtanzania aweze kuzipitia?

Inaonekana katika fikra zao historia ya Tanzania imeanza wakati wa Mkapa! Hebu angalia:

- Picha zilizopo kwenye tovuti hiyo ya tanzania.go.tz kuhusu Rais ni za mwaka 2007!
- Press Release waliyonayo (as of leo) ni ya Aprili 8, 2010. Ina maana kwa haraka haraka hawa jamaa hawajatoa press release kwa mwezi mzima. Kwa taifa kama la kwetu idara inatakiwa kutoa press release kila siku iendayo kwa Mungu ya nini Rais kafanya au nini kimetokea Ikulu.
-Ukienda kwenye hotuba za marais wanazo kuanzia awamu ya tatu tu! Kwa maneno mengine awamu ya pili au ya kwanza haina nafasi katika Tanzania yao hii mpya. Hivi hawaoni kuwa historia yetu ni ya moja kwa moja tangu Nyerere hadi leo hii? Hata kama hawampendi Nyerere au kutaka kumkumbuka na hata kama wanaona Mwinyi hakuwafaa hawawezi kamwe kufuta historia zao. Tunahitaji watu pale ambao wataweza kuunganisha historia nzima kwa manufaa ya watanzania. Ingesaidia sana wanafunzi katika shule na vyuo vyetu wanaofanya utafiti mbalimbali au hata kwa waandishi na watafiti wa mambo mbalimbali.

4. Kilichonitibua hata hivyo zaidi ni upotoshaji wa wazi unaofanywa na idara hiyo linapokuja suala la hotuba za Rais. Nimefuatilia kwa muda mrefu (tangu hotuba ile ya Kikwete kuhusu Muungano Bungeni) hadi sasa na nimegundua kuwa kina Salva, Premi, na wenzao wanaamini kabisa kuwa hotuba ya Rais ni ile iliyoandaliwa na siyo iliyotolewa!

Katika mawazo yao potofu, ile hotuba iliyoandikwa ndiyo rasmi na ile iliyotolewa siyo rasmi na hivyo utaona kuwa katika tovuti ya Tanzania hotuba za Rais zilizowekwa siyo zote ndizo zilizotolewa na Rais. Wamekuwa wakiweka mtandaoni hotuba zilizopangwa kutolewa lakini SIYO zilizotolewa.

Mfano mzuri ni hotuba ya mwaka jana ambapo Rais alizungumzia suala la asilimia 30 za bajeti kutafunwa na mafisadi wakati akifungua jengo la PCCB. Japo alizungumza hadharani hilo kwenye hotuba yao kina Salva hilo hakuna!

Mfano mwingine ni hii hotuba ya juzi kwa Mbayuwayu, Watanzania wengi wanakumbuka mfano huu wa Kikwete na porojo nyingine alizozitoa. Ile ndiyo ilikuwa hotuba rasmi. Lakini kina Salva katika hekima yao ya milele wameamua kuweka hotuba ambayo Kikwete alikuwa aitoe!

Ukweli ni kuwa hapa wanapotosha watu kwa sababu wanatuweka hotuba ambayo Kikwete mwenyewe hakuitoa. Wakati umefika waache hili, kama Rais wao hawezi kukaa makini na kusoma alichoandikiwa kama Obama basi ni watoe hotuba zake kama zilivyo, kama walivyokuwa wakimfanyia George Bush kwani hizo ndizo hotuba rasmi! Nakumbuka vizuri hili kwa sababu katika ile hotuba ya kutetea Muungano Kikwte alisema mengi sana na mengi yaliyokuwa yakushagaza zaidi lakini ndugu zetu hawa katika hekima yao isiyo na mwisho wakaonelea wasitoe hotuba ile bali watoe kile "alichopaswa" kusema.

Ndugu zangu, kuna mgogoro wa mawasiliano na wakati umefika Salva na Premi waachie ngazi wawape watu wengine nafasi ya kufanya kazi ya mawasiliano ya Ikulu kwa uhakika, ufanisi na ukweli.

Majibu toka 'high office'

aaah,,mmmh,,yeh yeh...unajua kijana unayosema ni sahihi kabisa,,izi tovuti zetu hazifanyi kazi inavyotakikana,,,na unajua tulikuwa bize kwanza na kuhakikisha mafisadi wanapelekwa mahakamani,,,naaaaa pia kujenga shule za kata,,,,eeeh kujenga barabara kuunganisha mikoa yote kasoro kigoma,,,,,kujenga daraja la umoja,,,,kuandaa mkutano wa sulivan na ule wa uchumi wa dunia,,kuandaa ujio wa raisi bush,,,na kuandaa ujio wa timu ya real madrid-tena unajua hawa real madrid wana uwanja mzuri sana nilipata kufunga safari kwenda kuutembelea ni mzuri kwakweli kushinda hata ule wa sokoine mbeya

sasa kijana kati ya zahanati na tovuti kipi muhimu....nihangaike kuhakikisha tuna zahanati kila kata au nihakikishe kuna tovuti kila kaya? sema wee unatakeje? we mwenyewe umeona jinsi mbayuwayu walivosumbua hapa katikati,,,utapata wapi muda wa kuangalia tovuti,,,ivi ni watu wangapi wa KAWAIDA wanajua kutumia komputer...achana na iyo kujua kutumia internet,,,sisi tunahangaika kuleta fiber optic cable ili mawasiliano yawe bora nyie mnapiga kelele za tovuti,,,ivi wewe bila tovuti utakufa? nakuuliza utakufa?

sikia bwana mdogo,,,,ikiwa unaona tovuti ni muhimu sana anzisha serikali yako iwe inashulikia masuala ya tovuti tu,,,sawa?
 
Lakini tatizo hasa nini, nina uhakika tukiwauliza wao watasema ni "pesa"...

wenye uwezo wanajua kuchambua bajeti wafuatile bajeti za vifungu vya mambo ya ICT kwenye idara na wizara. Nahakika tutashangaa. Pesa zinatengwa vifaa vinaunuliwa kwa tena kwa bei kali ya tender. lakini No OUPUT

Yaani kwa hii thread na hivi matayarisho ya bajeti yanaendelea tume wasaidia kuwaongezea watu ulaji. wataoongeza maombi ya pesa ili bajeti iwe kubwa ili wakidhi kiu ya jamii forum . lakini mwisho wa siku ni yale yale.
 
Back
Top Bottom