Uzembe ulisababisha maafa mbagala

grndossy

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
311
80
Uzembe wa polisi ulisababisha uharibifu mkubwa uliosababishwa na waislamu waliovamia KKKT usharika wa Mbagala. Nasema haya kwa sababu polisi waliweza kudhibiti shambulio la kwanza la wavamizi hawa kwa mabomu ya machozi badala ya kuimarisha ulinzi katika eneo hilo waliondoka na kuacha eneo hilo katika ulinzi mdogo sana wa walinzi wa kampuni ya ulinzi wanaolinda katika siku za kawaida huku wakijua hao wavamizi walikuwa mitaani wakirandaranda kwa makundi.

Wavamizi hawa walipoona polisi wameondoka ndipo walipokuja kwa makundi makubwa sana na wakawazidi nguvu wale walinzi wachache waliokuwa wamebaki katika eneo la kanisa hilo na ndio uharibifu huo mkubwa ulitokea na nusura kutoa hata uhai wa mchungaji kiongozi wa usharika huo pamoja na watumishi wengine.

Kama polisi wangetimiza wajibu wao sawa sawa tatizo hili kubwa namna hii lisingetokea au lingetokea kwa udogo sio katika magnitude hii.

 
Back
Top Bottom