Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Habari za mchana wana JF, Naomba kama kuna wataalamu humu wa masuala ya uzazi wa mpango wanisaidie kunijuza maanake sasa nina mtoto mmoja ila nlitka nikae kwa miaka 3 au 4 Mungu akipenda bila kuzaa. Ila kitu kimoja sikutaka kabisa mke wangu atumie hizi dawa na aina yoyote za majira za kufunga uzazi na viulevile sipendi kutumia kondom, nlichokuwa nahitaji kujua kama kuna uwezekano wa mwanaume kufunga lakini kwa njia salama zaidi

Please msaada wenu unahitajika sana.
 
Nakushauri nenda katika vituo vinavyotoa huduma ya uzazi wa mpango upate ushauri husika, kwa sabau kule wanasikiliza hadithi yako na kukushauri. Mwanaume akifunga uzazi, haimpunguzi nguvu za kiume hata...anakuwa rijali kama kawaida. Lakini ndio hataweza kutungisha mimba tena maishani mwake, kwani huo upasuaji wanafunga mrija wa kupitisha mbegu moja kwa moja.

Kama una mpango wa kuzaa tena baada ya miaka mi3, nakushauri tumia njia nyingine mtakayoshauriwa katika kituo cha kutoa huduma za uzazi wa mpango kwa hiyo miaka mi3, kisha mkishazaa mtoto mnayemuhitaji na hamuhitaji tena...ndio ufunge!
 
Nakushauri nenda katika vituo vinavyotoa huduma ya uzazi wa mpango upate ushauri husika, kwa sabau kule wanasikiliza hadithi yako na kukushauri. Mwanaume akifunga uzazi, haimpunguzi nguvu za kiume hata...anakuwa rijali kama kawaida. Lakini ndio hataweza kutungisha mimba tena maishani mwake, kwani huo upasuaji wanafunga mrija wa kupitisha mbegu moja kwa moja.<br>
<br>
Kama una mpango wa kuzaa tena baada ya miaka mi3, nakushauri tumia njia nyingine mtakayoshauriwa katika kituo cha kutoa huduma za uzazi wa mpango kwa hiyo miaka mi3, kisha mkishazaa mtoto mnayemuhitaji na hamuhitaji tena...ndio ufunge!
<br><br>Nashukuru sana DR Riwa kwa ushauri wako na wengine ambao mmechangi katika mjaadala huu nitajaribu kuwaona wataamu ili niuone hw they gona help me&nbsp;

nashukulu sana wandugu nitajaribu kuwaona Wakuu wa hiyo kitu ili nijue watanishauri nini. asante wanaJF wote mliochangia
 
Nakushauri nenda katika vituo vinavyotoa huduma ya uzazi wa mpango upate ushauri husika, kwa sabau kule wanasikiliza hadithi yako na kukushauri. Mwanaume akifunga uzazi, haimpunguzi nguvu za kiume hata...anakuwa rijali kama kawaida. Lakini ndio hataweza kutungisha mimba tena maishani mwake, kwani huo upasuaji wanafunga mrija wa kupitisha mbegu moja kwa moja.

Kama una mpango wa kuzaa tena baada ya miaka mi3, nakushauri tumia njia nyingine mtakayoshauriwa katika kituo cha kutoa huduma za uzazi wa mpango kwa hiyo miaka mi3, kisha mkishazaa mtoto mnayemuhitaji na hamuhitaji tena...ndio ufunge!

Riwa kaka kumbe hupo? mbona kule kwenye usafi tunakuita hutaki kuja? msaada wako hunaitajika kule kaka.

back to the topic, mtoa mada kwanza nakupa hongera zako kwa kile ulichokifikiria ni wanaume wachache sana wanaweza kudhubutu hayo uliyofikiria, pili kama Riwa alivyochangia nenda kwenye vituo vya afya watakusaidia, kama vipi tumieni kalenda itawasaidia.
 
Wana Jf doctor's,

Kuna mdogo wangu alienda Marie stopes mwenge kuomba ushauri kuhusu hizi njia za uzazi wa mpango basi alipewa ushauri yeye kwa ridhaa yake akachangua njia ya Loop/kitanzi kwa sababu aliambia haina hormones zozote sasa basi aliwekewa amekaa kama mwezi na nusu hivi kwanza period hakuona na alikuwa anapata maumivu makali chini ya kitovu na anatoka majimaji mengi kwa siku anabadilisha panties kama nne hivi ikabidi arudi kuwaeleza wakamcheki mimba akawa hana baada ya siku kama tatu hivi akapata infection akarudi tena marie wakampima ikagundulika amepatwa na fungus basi wakampa cipro antibiotic akiwa anatumia hizo dawa mauvimu yakazidi chini ya kitovu upande wa kushoto akijibonyeza maumivu yanazidi ilibidi usiku wa manane arudi marie wakamshauri atoe ile Loop/kitanzi kwa sababu haijampenda, na kweli baada ya kukitoa alijisikia ahuen maumivu yaliendelea kama siku mbili hivi na akijibonyeza anasika kama uvimbe sehem iliyokuwa inauma ndo yuko kwenye mikakati aakafanyiwe Ultra sound.

Je naomba kuuliza hivi hizi njia za uzazi ni salama kweli! naombeni ushauri maana mimi binafsi nilimwambia aachane nazo kabisa na je atajilinda vipi na hizi mimba sizizotarajiwa angalizo yuko kwenye ndoa...

Nawasilisha...
 
Side effects zipo lakini ni njia salama kabisa! Mdogo wako alipata reaction ya copper, Hizi loop hazina hormones lakini zina copper (shaba) kwa baadhi ya watu wako hypersensitive kwa copper. Mshauri atumie vipandikizi (implanon) nayo ni ya muda mrefu pia, kama hataki hormones pengine condoms ni alternative.
Natural family planning ni nzuri lakini failure rate yake ni kubwa.
 
Asante mkuu kwa ushauri wako I have learned something good here hiyo copper ndio ilimletea shida but wengine huwa inawapenda nasikia...thanks indeed...
 
IUD inaweza sababisha cyist (sijui ndio uvimbe) mwenye cervix au kutoboa uterus. Inashauriwa kufanya ultra sound after 6 weeks kumake sure haija move na mambo mengine. Usually unaspot for the first few month especially copper.
 
Karibuni kwenye ukurasa huuu mpya tujadili na kuongelea kwa undani zaidi
kuhusu njia zinazoweza kutumiwa na wanawake, wasichana kuzuia ujauzito. Karibuni sana.

Nilitaka kusema njia zitumikazo kwa uzazi wa mpango. Ila kuna wengi wengineo
ambao wako single kwa uchaguzi wao wa maisha, wanasubiri kuolewa, wako masomoni etc.
Kwa hiyo nikaona "uzazi wa mpango" si sahihi kutumia sababu bado hawajafikia kupanga uzazi. ..

Anyway kama wote tujuavyo njia bora kuzuia ujauzito ni moja tu Kutokufanya sex(mapenzi)
Ila njia hii ni wachache sana tena sana wanaoifuata. Ndio nikaona nianzishe uzi huu tujuzane na kufundishana
njia nyingine nyingi, na zipi za kutumia na kwa muda gani na ni nini madhara ya njia hizo za kuzuia ujauzito.

1. Condom.
Condom ni njia ya kwanza kabisa ninayoipendekeza kama sote tujuavyo inasaidia kuzuia
maambukizo ya virusi na pia kuzuia ujauzito. Ni vema kujifunza jinsi ya kutumia condom.
Ni rahisi sana kutumia condomo za kiume , Pia ni rahisi sana kutumia condom za kike .
080000-female-condom.jpg
female condoms. (tuta ongelea zaidi kuhusu hili as we go on )

2.EMERGENCY CONTRACEPTION. or ( morning after pill)
Hivi ni vidonge ambavyo vinatakiwa kuchukuliwa massa 72 . Baada ya kufanya sex bila protection ya aina ye yote. ila ni vema kuchukua mapema zaidi. wengi hupendekeza kuchukua ndani ya masaa 24 baada ya sex.. Hii ni back up system kama condom ikibasti, umesahau kuchukua vidongo. Na zaidi ni kwa wale waliolzamishwa kufanya tendo la ndoa bila ihari yao, au kama unawasiwasi u mjamzito na hauko tayari . Huwa inapatika kwenye maduka ya dawa baridi. Na inategemea ni muda gani umepita tangu umefanye sex. Kama ni ndani ya masaa kumi na mbili huwa unapewa kidonge kimoja tu basi .

3. Vidonge
Kuna aina nyingi ya vidonge vya uzazi wa mpango . vidonge hivi unatakiwa kuchukua kila siku kama ulivyoa agizwa
na doctor . Vidonge huwa havifanyi kazi kama umetapika tu baadaya kuchukua au kama una diarrhea. vidonge pia vina
Side effects mfano, kuongeza uzito, kuumwa na kichwa , na wengine huvimba matiti. Vidonge vina athari tofauti kwa
kila mtu.

4.Depo- Provera ( Injection )
Kama hutaki usumbufu wa vidongo , Injection ni njia nyingine unaoweza kutumia. Injection inazuia ujauzito
kwa miezi mitatu . Kila baada ya miezi mitatu unatakiwa kupata dozi tena.( Kwa hiyo mara nne kwa mwaka) . Injection
ina side effects pia, period huwa chache na nyepesi sana na baada ya kutumia injection kwa mwaka waeza usione tena Period yako. na kuna wengine ni kinyume kabisa nikimaanisa wanakuwa na period nzito lakini inatoka kama nukta , nukta , haiko mfululizo.Haya yote hutoka na vitu kama uzito wa mwili pamoja na Lishe .

5.Diaphragm/ Cervical cup
Hii ni njia nyingine ya kuzuia ujauzito . Lazima iwe saizi yako . Maana ikiwa kubwa au ndogo haitafanya kazi. Kwa hiyo
doctor atakaye kupa hii atakueleza maelezo yote jinsi ya kutumia . nieleze kidogo jinsi ya kutumia huwa inakuja na na gelly
inayoitwa spermicide. Hiyo unaweka kuzungungukana na pia katikati ya diaphragm au cervical cup, baada ya hapo unaikandamiza iliupate shape ya
kama pembe nne . unaingizaa ikulu kwa kutumia kidole au videle. Unaweza kuiweka masaa kadhaa kabla ya sex. ila unatakiwa kuiacha hapo kwa masaa sita baada ya kujamiiana. uzuri wa hii unatoa na kuiosha na kutumia tena na tena. Tatizo kubwa ya hii ni kuweka
inapotakiwa. Ila doctor atakaye prescribe hii atakupa instraction zote na pia atakuonyosha jinsi ya kuweka.
080000-diaphragm.jpg
hii ndiyo diaphragm. Na hivi ndivyo inavyokaa.

6. Implants
Hii njia huwa inatumia na wanawake wengi ambao Hawataki kupata ujauzito kwa muda mrefu. pia hutumiwa zaidi
na wanawake ambao hawataki usumbufu wa vidonge, diaphragm/Cervical cup au injuctions. inaonekana kama kama kijiti
kidogo sana cha plastiki. Huwa kinaweka chini ya nyama ya mkono "upper arm" ambapo ina release the contraceptive steroid .
Inazuia ujauzito kwa muda wa miaka mitatu mpaka mitano. uzuri wa hii kitu unaeweza kuondolewa saa yeyote ukiamua kupata ujauzito. Side sffects, mzunguku utabadilka, kuongeza uzito etc.
health-061012-implanon.jpg
Implanon/ Implants.

7. IUD (intra-uterine device) or T shape.
Hii ni kwa wale ambao Hawataki kufunga kizazi au wale ambao hawana mpango wa kuwa na mwana kwa muda mrefu zaidi . nikimaanisha kuanzia miaka mitano mpaka kumi na mbili . hichi ni kitu ambacho kina T shape kinaweka ndani ya uterus huwa unawekewa na health-care professional kama ilivyo Implants. uzuri wa hii pia ni kama ya implants . wanaweza kuiondoa muda wowote upendao. Ni vizuri kuangalia kila mara moja kwa mwezi kuona kama bado iko wima. ni rahisi sana kuangalia. Kidole tu.
Huwa utahisi maumivu baada tu ya kuweka . masaa machache baadaye hutahisi kitu , kawaida tu .

Kama nilivyosema hapo mwanzoni njia bora ya kutokupata ujauzito ni kutokufanya sex. lakini kwa dunia tunayoishi ni bora kupeana elimu kuliko ku protend kila mtu ni mtakatifu. Kuanzia njia ya pili mpaka ya saba haizuii maambukizo ya ukimwi bali mimba tu. kwa hiyo unaweza kutumia CONDOM pamoja na hizi contraceptives kwa pamoja..

Na nilitaka tu kuonyesha si lazima tu vidonge kuna njia nyingi nyinginezo za uzazi wa mpango pamoja na kuzuia ujauzito. Binafsi si
support abortion kabisa. kwahiyo nasema ni bora ku ZUIA kuliko KUTOA.

Asanteni na karibuni tena.
Afrodenzi
 
si vizuri kutoa mimba ,ila kama msichana man method hayo mi sikubaliani nayo naona ni vema kwa sababu mwanaume mwenyewe hukai nae mnashtua tu kiaina mkutane siku ambazo si za hatari sio vizuri kuexpose mwili kwenye madawa madawa ya uzazi meeeeeeeeeen
 
vipi kuhusu midoli?
kama mkiafiki nitajitolea kutengeneza midoli yenye sura na umbo kama langu halafu wewe afrodenzi unasambaza kwa wanaohitaji.
 
"Bora KUZUIA kuliko KUTOA"
Me likey. . .

Kama hii elimu ya uzazi ingekua inawaingia wengi na wakazingatia viumbe vingi sana visingeonja mauti kwa starehe za watu wengine.

Ntacopy hii kitu niweke kwa blog,
 
si vizuri kutoa mimba ,ila kama msichana man method hayo mi sikubaliani nayo naona ni vema kwa sababu mwanaume mwenyewe hukai nae mnashtua tu kiaina mkutane siku ambazo si za hatari sio vizuri kuexpose mwili kwenye madawa madawa ya uzazi meeeeeeeeeen

Nakubali nawe ila si kila mtu anaelimu ya mfumo wa uzazi..
 
Back
Top Bottom