Gudboy
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 867
- 77
Maelezo ya Awali...
Njia za uzazi wa mpango hutumika na wanaume na wanawake kuzuia ujauzito kwa madhumuni ya kupanga uzazi ili kuwa na familia bora. Ni vigumu kusema kuwa kuna njia iliyo bora zaidi ya uzazi wa mpango kwa kuwa kila njia ina faida na hasara zake. Wote kati ya mwanamke na mwanaume wana maamuzi juu ya mipangilio wa kupata watoto.
Kufanya uchaguzi utumie njia ipi kwa ajili ya kupanga uzazi siyo kitu rahisi kwa kuwa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kufanya maamuzi yeyote. Lakini awali kabisa, inabidi ujifunze njia mbali mbali, ili kuweza kubaini ni njia ipi itakayokufaa pamoja na mwenzi wako kupanga uzazi. Mnaweza pia kuwasiliana na muuguzi au daktari anayeusiana na masuala ya uzazi wa mpango kwa ushauri, ili muweze kuchagua njia sahihi itakayowafaa.
Kabla ya kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango, inabidi ufikirie kuhusu mambo yafuatayo:
======
Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba.
Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.
Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.
Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.
Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)
Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono. Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya muda.
Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.
Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.
Tuangalie kwanza vifaa vya kuzuia mimba:
Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwaname na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndio isilifikie yai la mwanamke.
Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.
Kondom za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98. Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.
Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 95.
Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na caps. Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za mwanamme kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.
Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.
Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanamme haitapatanafasi ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.
Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwaname. Hapo diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.
Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia moja kuzuia mimba.
Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.
Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji.
Mbinu nyingine za kuzuia mimba
Kuna chembe chembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama homornes ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba.
Chembe chembe hizi kwa jina maalum progestogen yaani mchanganiyko wa oestrogen na progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa. Hufanya kazi kwa namna hii:
* Kwa kuzuia ovari kuangua mayai
* Kwa kuzuia mbegu za mwanamme kulifikia yai (kwa kufanya majimaji ua ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia mbegu ya mwanamme kupenya)
* Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha nyumba ya uzazi.
Tembe mchanganyiko - huwa ni kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chembe chembe za oestrogen na progestogen. Hii huzuia mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Tembe ni rahisi kutumia - Mradi tu unakumbuka kumeza vidonge kulingana na maagizo. Wakati mwengine pia huifanya hedhi, kupungua na kupunguza pia maumivu wakati wa hedhi.
Lakini athari zinazoandamana na utumiaji wa vidonge hivyo ni pamoja na kuchafukwa na moyo, kuongezeka unzani, na athari mbaya zaidi ni iwapo itatokea hali ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya kupitisha damu.
Vidonge vya Progestogen pekee (POP) - Aina hii ya Tembe huitwa pia "mini pill" na huwa ina chembe chemba za progestogen pekee. Huzuia mimba kwa njia kama zile zile zinazozuia tembe za mchanganyiko, na ina utendaji kazi wa kati ya asilimia 96 na 99. Hata hivyo kama una uzani wa zaidi ya kilo 70 uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua
Faida kuu ya kutumia vidonge hivi ni kwamba vina athari ndogo za kiafya. Lakini tatizo ni kuwa ni sharti tembe imezwe wakati ule ule kila siku , kama umechelewa basi isipitishe zaidi ya masaa matatu.
Sindano - Hii ni chanjo ya kuzuia mimba inayotengenezwa na chembe chembe hizo hizo za homoni ya progestogen. Tofauti na tembe, ambazo ni sharti kumeza moja kila siku, sindano pindi inapodungwa inakupa kinga dhidi ya mimba, kwa mda wa kati ya wiki nane hadi 12 kuambatana na aina inayotumiwa.
Hudungwa takoni, na dawa kuingizwa ndani ya mishipa ya damu na ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Faida kuu ya njia hii ya sindano, ni kwamba hutakuwa na wasiwasi wa kupata mimba unapofanya ngono, kwa mda wa angalau wiki nane au 12.
Lakini pia ina athari zake - ni kwamba huenda dawa hii ikavuruga mpangilio wako wa kawaida wa kupata hedhi, au ukatoka hedhi kiwango kisicho cha kawaida cha damu, au kwa mda mrefu, au hedhi ikapotea kabisa. Pia inaweza kusababisha kuongezeka uzani.
Homoni au Vidonge vya kupachika chini ya ngozi Hapa dawa kama ile ile ya tembe au chanjo, hutengenezwa na kuwekwa kwenye kifaa cha plastic mfano wa kijiti cha kiberiti. Hupachikwa ndani ya ngozi chini ya kwapa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.Hii ni njia ya mda mrefu ya kuzuia mimba. Inaaminika kuzuia mimba kwa aslimia 99 na inaweza kufanya kazi kwa mda wa hadi miaka mitatu.
Kuna aina nyenginezo za upangaji uzazi ambazo, ingawa kwa hali ya kawaida hazipendekezwi kwa vijana, si vibaya kuzijua.
Kitanzi au koili, ambacho kwa lugha ya kitaalam kinajulikana kama Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba, na hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.Vitanzi huanza kufanya kazi pindi kinapopachikwa. Hufanya kazi kwa njia mbili kuu. Kwanza, kwa kuzuia mbegu za kiume kutangamana na yai, na pili kuzuia yai kukubaliwa kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi.
Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.
Hata hivyo moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyengine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya mfuko wa uzazi.Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.
Njia asilia ya mpango wa uzazi:
Njia hii inahitaji makini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa wanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika mimba.
Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi, na kupima hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoufu mkubwa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Kwa vile ni ya kubahatisha haipendkezwi kwa vijana ambao hawako tayari kupata mtoto.
Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni, pindi tu kabla ya kufikia kilele cha kumwaga manii, ni moja ya njia za kuzuia mimba.
La sivyo kwani mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa uume huenda umeshachelewa!Vasectomy au Tubuligation, Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.
-Vasectomy ni njia ya kumfanya mwanamme asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.Mwanamme anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.
Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanamme kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto (zaidi).
Kitanzi cha Intra uterine system au IUS - Hiki nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe za homoni ya progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.
Kitakapopachikwa, progestogen pole pole huingia ndani ya mwili, na kuzuia mimba katika njia ile ile kama vinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa mda wa miaka 5, na kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 99.
-Kitanzi cha IUS ni kizuri kwa wale walio na matatizo ya maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kinapopachikwa (ingawa wakati wa kupachikwa huenda ukapata maumivu kidogo) baadaye husaidia kupunguza hedhi au hata kuisitisha kabisa, kutokana na homoni hizo za progestogen. Madhara ya njia hii nayo ni kama, kuongeza uzani, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu kusiko na mpango, na mabadiliko ya majira ya hedhi. Pia inaweza kuchopoka, hivyo itabidi kumwona muuguzi au daktari kila mwezi kuhakikisha kiko sawa.
Ni vyema kujadili juu ya aina mbalimbali za mpango wa uzazi ili kuchagua vyema. Daktari wako au muuguzi atakushauri ipasavyo. Hata hivo kumbuka njia hizi za kuzuia mimba hutumiwa zaidi kwa minajili ya mpango wa uzazi, hivyo basi haziwezi kukukinga dhidi ya maambukiko ya virusi vya Ukimwi, au magonjwa mengine yayayosambazwa kupitia ngono.
Ni busara kutumia kondom kila unapofanya mapenzi na mtu ambaye afya yake ya uzazi huifahamu - Hakikisha pia unaufahamu vizuri jinsi ya kutumia kondom na unajua jinsi ya kufanya ngono salama kwa jumla.
Threads zinazofanana
CONFESION: Madhara ya Vidonge vya Uzazi Wa Mpango...
Njia ya uzazi wa mpango wa asili (natural birth control)
Vikwazo vya Viongozi wa Dini kuhusu kampeni ya uzazi wa Mpango
Athari za kutumia njia za uzazi wa mpango za kisasa

- Afya yako kwa ujumla.
- Ni kwa kiwango gani njia husika ya uzazi wa mpango inafanya kazi.
- Unajamiiana mara ngapi?
- Matarajio ya kupata mtoto siku za usoni.
- Je ni nini faida na madhara ya kutumia njia husika ya uzazi wa mpango?
- Je unafurahia kutumia njia husika uliyochagua?

SWALI
Msaada jamani.
Wife anadai condom zina msumbua sana.
Akienda uwani anakuta mafuta mengi ya condom ukeni.na kama ikipasuka huwa inabakiza vipande ukeni.
Msaada jamani.
Kalenda pia imetushinda.
JIBU
Vizuizi vya Ghafla (Emergency Contraception)
Hii hutumika wakati mwanamke amefanya mapenzi kiholela kupitia kwa uke (vaginal sex) ili kumzuia kupata mimba. Inaweza kutumika pia kama njia za kizuizi zilizokuwa zimetumika hazikufaulu. Hufaa sana kama itachukuliwa kabla ya masaa 72 kutoka wakati wa mapenzi. Huhusisha kunywa dawa mbili za &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Hormone' zikiachana kwa masaa 12. Hizi dawa vidonge hufaa kwa asilimia 75-89 kuzuia mimba.
Njia nyingine ya kizuizi cha ghafla ni kuwekwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];copper T IUD' kwenye tumbo la uzazi kabla siku 7 hazijaisha kutoka wakati wa mapenzi (ngono). Hii njia hufaa asilimia 99.9 kuzuia mimba na inaweza kutolewa wakati wa muezi huo mwingine. Kama tayari ushaishika mimba njia hizi hazitakusaidia. Hii njia za ghafia hazifai kutumika kama desturi.
Povu na utando,
Povu na utando au vidonge vilivyo na kemikali ya kuua mbegu (manii) &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; spermicide huwekwe ndani ya uke si zaidi ya saa moja kabla ya kufanya mapenzi. Huwa zinafanya kazi kwa kuua manii. Huachwa papo hapo kwa masaa 6-8 baada ya kufanya mapenzi. Kemikali hizi (spermicides) zingine huwa na Nonoxynol-9 ambayo kukulinda kutokana na kisonono na Chlamydia. Nonoxynol-9 hatakulinda kutokana na ukimwi. Kemikali hizi (spermicides) hufaa kwa asilimia 74 kukulinda kushia mimba.
IUD (Intrauterine Device)
Hiki ni kifaa cha plastiki au shaba kilicho na umbo la &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];T' na huwekwa kwenye mji wa mimba/tumbo la uzazi (uterus) ili kuzuia manii kulifikia yai. Hukaa kwa muda wa miezi kadha hadi miaka 10. Hiki kufaa husaidia asilimia 98-99 kuzuia mimba. Kinapowekwa, huanza kazi yake papo hapo. Unaweza kupata kiharusi siku chache baada ya kuwekwa IUD. Kati ya mwezi wa 3 na 6 unaweza kutoa damu kidogo juu zaidi ya damu ya hedhi. Pia mwezi wako/wakati wako wa hedhi utakosa kubainika. Wanawake wengine hutoa damu kwa wingi.
Njia ya kutumia kizuizi
Kondomu za Wanawake/kike
Huu ni mrija mtegevu wa plastiki huvaliwao kwenye uke. Pande iliyafungwa husaliwa ndani karibu na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Cervix' na upande uliowazi huvaliwa tu nje ya uke. Hii njia ya kutumia kizuizi hiki huzuia manii kufikia yai. Hii kondomu yaweza kuvaliwa aghalabu masaa 24 kabla ya kufanya mapenzi na hufaa kwa asilimia 79-95 katika uzuizi wa mimba. Kondomu hizi hupatikana kwenye maduka ya dawa. Pia hospitali za mikoa na kliniki hupatiana kondomu hizi bure.
Diaphragm/Cervical Cap (Kiwambo-diaphragm)
Hii njia huzuia manii kulifikia yai. Kiwambo hiki huwa na umbo kama kikombe nayo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Cerival cap' huwa na umbo kama kastabini (thimble). Hizi hufunikia &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cervix' (mwanzo wa tumbo la uzazi) ili manii yasiingie kwenye tumbo la uzazi (womb). Zinafaa kuvaliwa/kuwekwa ndani ya uke kabla ya kufanya mapenzi. Kiwambo hiki hufaa kwa asilimia 80-94 kwa kuzuia mimba. Nayo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cervical cap' hufaa asilimia 80-91 kuzuia mimba kwa wanawake ambao hawajawahi pata mtoto, na hufaa asilimia 60-80 kwa wanawake ambao keshajifungua. Unafaa kumwona daktari au mtaalamu wa mambo yahusuyo uke ili
akuweke kiwambo au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];cap'.
Njia za Hormoni
Vidonge Vya Kumeza (Pill)
Kidonge hufaa kunywewa kila siku na huwa na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hormones' mili ambazo ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ostrogen' na progestin ambazo huzuia kifuko cha mayai kwenye uke kutoa mayai. Inapotumika ipayasavyo hufaa kwa asilimia 95-99.9 kuzuia mimba. Kama una miaka zaidi ya 35 na huwa unavuta sigara* au umewahi kuwa na historia ya kuvilia damu au kansa ya maziwa (matiti) au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];endometrial' daktari wake anaweza kukushauri usitumie kidonge hiki.
Vidonge hivi huongezea hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo, kukimbia kwa damu, kuvilia damu na kufungamana kwa mishipa ya damu. Kuna aina mbali mbali ya vidonge hivi na huwa na vipimo tofauti vya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];oestrogen' na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];progestin'. Unafaa kualiza shauri kutoka kwa daktari wako au kutoka kwa hospitali/kliniki kabla hujaanza kunywa vidonge hivi. Vidonge hivi hupatianwa bure katika hospitali za mikoa na kliniki nyinginezo.
The Mini Pill
Hiki kidonge (vidonge) hufaa kunywewa kila siku na huwa na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Hormone' moja (progestin) ipunguzayo na kuafanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito/mnene ili kuzuia manii kulifikia yai. Kidonge hiki pia huzuia yai uliloungana mbegu kukomaa (kujiimarisha) kwenye uke. Hiki kidonge hufaa sana kwa wanawake ambao hawawezi kunywa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];oestrogen' au kwa wale wana hatari ya kuvilia damu. Akina mama wanaonyonyesha wanaweza kukitumia kidonge hiki kwa sababu hakiadhiri utuaji wa maziwa. Kitumiwapo ipasavyo, hufaa kwa asilimia 95-99.9% kwa uzuizi wa mimba.
Sindano &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Depo-Provera
Depo-Provera ® huzuia utoaji wa mayai na hufanya ute wa ngozi ya ndani ya uke (cervix) kuwa mzito hivyo kuzia manii kupenyeza kwenye tumbo.* Pia hufanya tabaka (lining) la tumbo kunenepa hivyo kuwa vigumu kwa yai lililoungana na mbegu kujishikilia. Wanawake hsindano hii kwenye makalio (******) au mkono baada ya kila miezi mitatu. Hufaa kwa asilimia 99.7 kwa kuzuia mimba. Sindano hii haistahili kwa wanawake walio chini ya umri wa miaka 21 ila tu kama wameshawahi kujifungua au hawawezi kutumia njia nyingine ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Harmone' kwa sababu ya matatizo ya kiafya. Daktari wake/mtaalamu atakudunga sindano hii.
Njia za kitabia
Hii huwa mwanamume kuondoa uume wake kutoka ndani ya uke kabla ya kutoa manii ili kuzuia mbegu kufikia yai. Hii njia huhitaji uzuifu mwingi sana (kutokana na msongo) upande wa mwanamume. Hata kwa kutumia njia hii unaweza pata
mimba KABLA mwanamume hajatoa uume wake. Kabla hajatoa manii mwanamume anaweza kutoa manii mengine kabla ya kufika kileleni (pre-ejaculation) nah ii inaweza kusababisha mimba. Hivyo basi hii njia haifai sana kwa kuzuia mimba. Pia,
haitakulinda kutokana na maradhi ya zinaa. Kujinyima/kujifunga kutoka kufanya mapenzi wakati wa mwezi/hedhi au &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Fertility Awareness' ni njia nyingine, na inayofaa zaidi ya kuzuia uzazi kitabia.
Njia za kupanga uzazi milele
Kufanywa Tasa au Gumba kwa kutumia Upasuaji
Hizi njia za upasuaji huazimiwa kwa watu walio maliza uundaji wa familia au hawataki watoto.
Kufungwa mirija (tubal ligation/tying tubes') hufunga/hukata mirija unaobeba mayai ndiposa kuyazuia mayai kuingia tumboni la uzazi ambako yanaweza ungana na mbegu (manii).
&[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Vasetomy' (kufungwa kwa mrija ubebao manii kutoka wakati ufanyapo mapenzi.
Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Njia hizi haziadhiri uwezo wenu wa kufanya mapenzi. Kufungwa mirija hufaa kwa asilimia 95-99.5 % kwa kuzuia mimba. Hata hivyo hazifai katika kuzuia maradhi ya zinaa, kwa hivyo kama wewe si wa mke mmoja utafaa kutumia kondomu.
Family Planning Association of Kenya wana habari kuhusu mambo hayo kwa wanawake na wanaume. Unaweza kuwapigia simu kwa maelezo zaidi au uulize kwenye hospitali au kliniki iliyokaribu nawe. Wanaume wanaweza kufanyiwa upasuaji na warudi makwao lakini kwa wanawake itawabidi walazwe.
MKUU CHAGUA NJIA UNAYOIONA NI NZURI KWAKO KATI YA HIZI NJIA ZA KUZUIA MIMBA.
SWALI
Wasalaam
Hivi wakuu hili suala la uzazi wa mpango ni nani hasa anaetakiwa kufunga au kujizuia, maana hapa home tunawatoto wawili na kwetu tunaona imetosha ila mke wangu hataki kufunga analazimisha mimi ndio nifanye hivyo, nimejitahidi sana kumuelezea na kubembeleza kwao ilivyorahisi kufanya hivyo lakini amekuwa mgumu kuelewa.
Mara anasema basi tutumie condoms na mi siwezi kufanya hivyo wakati nipo kwenye ndoa sasa imebaki kubahatisha siku ambazo ni salama kwake mi inanikera sana mliwezaje wanandoa wenzangu.
Mnalichukuliaje hili swala, nyie mliwezaje kuwashawishi na wanawake wa siku hizi mbona mnakuwa viburi kiasi hiki.
JIBU
Kwanza ni muhimu ujitambue wewe binafsi vp uwezo ulionao unakutosha na unaweza kuwatunza vyema na hapo ndio unachukua uamuzi.
Pili, unamshirikisha mwenzio kuhusu wote kufunga uzazi sababu ni ngumu kumwambia mmoja funga wakati wewe bado risasi ziko ok,kama mnafunga fungeni wote,mimi niliamua na tukafanya maamuzi na wote tumefunga na hakuna tatizo.
SWALI
Mwanamke aliyetumia sindano za uzazi wa mpango humchukua mda gani kupata ujauzito pindi aachapo kutumia?
JIBU
Inatarajiwa aweze kurudi katika hali ya kawaida miezi mitatu baada ya kuacha kutumia (tangu sindano ya mwisho), kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.Hata hivyo baadhi(wachache) huchelewa kidogo kubeba ujauzito, uchelewaji huu hauwezi kuzidi miezi 24(miaka miwili).

Last edited: