Uzalendo wa kweli ndiyo dawa pekee ya kuutokomeza ufisadi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kila Mtanzania ni mchunga wa mwenzake,uzalendo na uchungu juu ya nchi yetu ndiyo suluhisho la tamaa ya kujilikimbizia mali za umma kwa faida ya wachache.Kila mtu akijua wajibu wake na akatimiza wajibu taifa letu litasonga mbele kimaendeleo.Tatizo linalotukumbwa sisi Watanzania ni mfumo duni unaojaribu kukumbatiwa na CCM katika chaguzi zake.Ni kweli kabisa CCM bila pesa huwezi kuwa kiongozi,ndo maana Chama kinawatumia matajiri kiweze kujitetea kwa kutumia rasilimali pesa kuwanunua Watanzania waliochoka kiasi cha kusahau haki zao na kuuza utu wao kwa mlo wa siku moja.

Hali hii ya CCM kukielekea kifo chake inazidi kushika kasi na kuutahadharisha umma kuwa bila pesa CCM haiwezi ushindani.Mambo yalijitokeza kwenye chaguzi za wawakilishi wetu kwenye bunge la Afrika Mashariki kinadhihirisha kaburi la CCM limeshachimbwa kinacho subiriwa ni muda wa mazishi.Sipendi kuamini kuwa hii hali ndani ya chama ya kuwakumbatia wenye pesa haionekani kama tishio kwa mustakabali wa chama kwa wanachama wake na taifa kwa ujumla.Wawakilishi hawa wamejitokeza mbele ya media zetu na kukiri kukithiri kwa rushwa katika chaguzi mbalimbali,nashindwa kujua kwanini chama hiki hakijiulizi wapinzani wao wanapoingia kwenye chaguzi mbalimbali hawaulizwi mtatupa pesa kiasi gani?

Kitendo cha CCM kutokushtuka juu ya anguko lake,kinathibitisha ajali yake ya kisiasa imewadia.Utamaduni wakuwajibishana na misingi na miiko ya uongozi imetupwa mara baada ya kuzikwa kwa Azimio la Arusha.Kuzikwa kwa Azimio hili ndiko kulikopelekea kufa kwa misingi imara ya uadilifu na kuibua misingi dhabiti ya ufisadi ndani ya chama hiki kwa maazimio ya chukua chako mapema.Matokeo ya chukua chako mapema kimesababisha bunge kusahau kazi yake ya kuisimamia serikali na kuwa mtetezi wa maovu ya serikali.Kuna hoja ambazo wakati mwingine Spika wa bunge anazikwamisha kwa nia ya kukilinda chama chake,halikama hii haikubaliki ndani ya taifa letu.

Wamechelewa wapi wa bunge wa CCM,mpaka wana kumbuka blanketi kumekucha na kufoka.Ufokaji huu ni sawa na mbwa aliyelala usingizi anapohisi bosi wake amemstukia hubwekea hata kivuli chake.Ni miswaada mingapi imepitishwa kwa kutumia wingi wa kura za ndiyooooo ambazo leo ndizo zimepelekea CAG kugundua madudu yaliyosabaishwa na sheria mbovu za manunuzi ya umma iliyofanyiwa kipindi kisichozidi miezi sita tangu kuwa sheria.

Kuna haja ya wananchi kuwachagua wabunge wazalendo kwa taifa lao wasio jali matumbo yao na maslahi ya vyama vyao.Tunataka mbunge atayesema serikali hapa mmekosea bila kumung'unya maneno na bila kujali itikadi ya chama chake.Tunataka bunge lisiwe chombo cha kulalamika bali cha kutoa maamuzi magumu katika mambo yanayo lisababisha taifa letu kuyumba.Tanzania si mali ya CCM kama alivyosema mh.Filikunjombe.Kama kweli CCM inaamini ni chama cha Watanzania na wenyewe ni Watanzania imebaki nafasi finyu ya kubadilika,vinginevyo cha mtema kuni kilchonyoa kanga manyoya kimewadia.Mungu Ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
:target::A S 41::A S 41:


Siku zote tumuache Mungu aitwe Mungu,milango ya gereza iliyofunguka kwa Paulo na Sila ni kudhihirisha Mungu yupo
 
Back
Top Bottom