Uzalendo upo wapi kwenu DAWASA kwa watu wa Kibaha?

ngomicom

Senior Member
Jul 6, 2012
123
19
Nisaidieni kufumbua maswali ninayojiuliza dhidi ya hawa dawasa na wananchi walipa kodi waishio Kibaha. Naamini wengi mnajua kuwa DAWASA huchukua maji hapo mto Ruvu, abadani ili maji hayo yafike Dar es salaam lazima yapite Kibaha. Kiukweli wananchi wa kibaha wanahangaika kupata maji sana, kibaya zaidi wachache wanaopata maji wanakatiwa maji eti kwa madai maji yanaenda kwa wakubwa hivyo wanakibaha wasiyatumie, Ajabu kweli, eti Wakubwa !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
wakati wote ni watanzania. Uzalendo upo wapi? Ukubwa wao upo wapi unaowazidi walipakodi?
 
Back
Top Bottom