Uzalendo Umemshinda Dr. Hamisi Kigwangallah!

Kawaambia kweli, maana kaona Uzini kamujibu wa Raza mmetumia millioni 60 kwa kujipatia kura 281 yaani kila kura moja mliyopata imewagharimu TZS 213,523 na mmeangushwa vibaya sana, mmpepata aslimia 5 tuu, (yes 5%) ya kura walizopata CCM, wamewagaragaza kwa asilimia 95.

Sasa huko Arumeru yuko mzee mamvi, aiseee, poleni na mapema. Ni kama kuchukuwa fedha za umma mkazi flash maliwatoni.

Vyama vya siasa vinavyopata ruzuku toka serikalini vinatakiwa kutoa mahesabu jinsi vilivyotumia hiyo ruzuku. Kushiriki kwenye chaguzi ndogo ni njia mojawapo ya kuhalalisha matumizi ya ruzuku au unataka warudishe pesa serikalini? Mbali ya yote kutumia milion 60 haina maana zilipelekwa nje ya nchi, bali ziliingia kwenye mzunguko (money circulation) mfano kulipia malazi, vyombo vya usafiri, vipaza sauti hivyo kuchochea ukuaji uchumi wa sehemu husika. Ujio wa uchaguzi mdogo Meru ni fursa kubwa sana kwa wenye mahoteli na nyumba za kulala wageni kama watakuja wapiga debe nje ya Arusha.....Karibuni wote hata Kigwangala

 
Hivi Faiza Foxy amebadili ID siku hizi?

Tiba

Amejifungua si unakumbuka jinsi mimba yake hiyo ilivyokuwa inamteza humu jf na kuwa na bifu na kila mwana cdm. Matenity leave yake itaisha mwezi ujao.
 
Pia unakua na akili kama za tambwe hizza.

Du! nimeipenda sana hiyo, kumbe Tambwe hizza naye mtu yupo bado, mbona hajawashauri ccm waache kuwapokonya wachimbaji wadogo sehemu zao huko Nzega, ila mimi nahisi huyu jamaa,japo ni dr.kuna mbegu ya Tambwe hizza ilitumika
 
Sera za kijinga za Ccm za uwekezaji,ziwezekeza jimbo la Nzega kwa mgeni,TUTARAJIE NINI?

gazeti la mwananchi la leo 24.2.2012 igunga watoa kilio chao kwa magufuli na kafumu .kutekeleza ahadi ya kujenga daraja la mbutu ambayo walitoa katika uchaguzi mdogo mwaka jana ,
 
Ungekuwa unamfuatilia Kiranga hata usingeweza kufikiri kwamba Kigwangallah ni mtu serious.
 
Nina imani moja kwamba ndani ya ccm hakuna aliye msafi wote wametenda dhambi!!!!!!!!! Na hakuna jema toka ccm, na ukombozi wa kweli wa TZ ni baada ya kifo cha ccm!!!! Mungu Ibariki Tanzania, uiepushe na tamaa za mafisadi.......
 
Maandiko matakatifu yanatueleza kuwa si wote wanaosema bwana bwana ni watakatifu, lakini wote mtawatambua kwa matendo yao! Kigwangala ni tapeli, mwizi. Mpaka jina lake kaiba la mtu. Saidi Bagaile ni noma sana mazee!
 
Mleta uzi hoja yako haina mashiko. Kigwangala ni mwanasiasa, sasa wewe ulitegemea katika mazingira hayo aseme nini kama sio kupigia chapuo chama chake? Nilidhani ndani ya uzi wako labda kuna hoja makini inayomshushia hadhi yake kama kiongozi makini kijana, kwa hili hoja yako haina mashiko unless hujui politics za dunia ya tatu zinavyokwenda.
 
Kawaambia kweli, maana kaona Uzini kamujibu wa Raza mmetumia millioni 60 kwa kujipatia kura 281 yaani kila kura moja mliyopata imewagharimu TZS 213,523 na mmeangushwa vibaya sana, mmpepata aslimia 5 tuu, (yes 5%) ya kura walizopata CCM, wamewagaragaza kwa asilimia 95.

Sasa huko Arumeru yuko mzee mamvi, aiseee, poleni na mapema. Ni kama kuchukuwa fedha za umma mkazi flash maliwatoni.

Zomba uwezo wako wa kufikiri nahisi kama una walakini. Hivi unajua pale Misri wakati wanaandamana kumtoa Mubarak walikufa watu wangapi? acha hela zilizopotea.
Songea watu wanne wameuawa na polisi wenu unajua thamani yao???
Wale waliouawa Arusha na aaskari wenu unajaua thamani yao??
Mnauana wenyewe kwa wenyewe, tuombe tu Mwakyembe apone, ila ikiwa tofauti sijui kama unaijua thamani yake.
kwenye kutafuta haki ya wengi (taifa) fedha ni kitu kidogo sana. CDM imetumia 60m huko uzini mnapiga kelele, zile bilions za EPA, KAGODA, MEREMETA, acha ambazo mnailipa IPTL kila siku haziwaumi???
jaribu kupanua wigo wa ufikiri wako la sivyo na wewe utaingia kwenye kundi la chiligati aliyesema bashe sio raia wakati bado ana cheo UVCCM.
 
demokrasia ina gharama kubwa,hata ikatokea mkafa wabunge wote lazima uchaguzi ufanyike.Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia ndani ya mfumo wa vyama vingi.Fikra mgando ni ombwe kubwa la uongozi,heri uchi wa nyama kuliko uchi wa akili,poleni sana watu wa magamba.Nzega bado hawajalipwa haki zao mara baada ya kunyang'anywa ardhi na kupewa wakoloni,ziko wapi harakati zako ulizozianzisha,au ndiyo unajaribu ku-cope toka wana CCM mara baada ya mkwara wa Ridhiwan,kuwa mbona unawageuka hutaki kuwasaidia wakati wao walikusaidia kupata ubunge!Mpiganaji makini kama Che-Guevera haangali rangi ya bendera katika mapambano ya harakati za Mtanzania maskini.
 
Naomba mchangiaji huyu anieleze wakati chadema wakitumia milioni 60 ccm walitumia ngapi isije ikawa ule usemi kuwa "Nyani haoni kundule" maana inaelekea kama wewe siyo msajili wa vyama vya siasa basi ni karani wake ndo maana una data. Naomba msaada ktk hili mheshimiwa sana.
 
Wewe una chuki zako binafsi tu, Kigwangalla ni jembe la ukweli na 2015 tutamshauri achukue fomu agombee Urais kabisa maana anatetea raslimali za Tanzania kwa moyo wa dhati wala siyo unafiki, na anatetea makundi yanayokandamizwa kama vile madaktari, walimu, polisi na sisi vijana kuliko mbunge yeyote yule. Go HK, Go HK, tuko nyuma yako!
Naamini mnakumbuka kuwa uchaguzi 2010 jimbo la Nzega H. Kigwangala alishindwa kwenye kura ya maoni lkn alipitishwa tu kwa mizengwe. Baada ya kushinda uchaguzi mkuu akaanza kazi kwa mbwembwe tukahisi kuwa tumewapata angalau wabunge vijana wawili (January na Hamisi) kutoka chama hicho dhalima ambao wangekuwa watetezi wa wanyonge na vijana kumbe hamna kitu!
Juzi tumemuona Kigwangala akiwatetea madaktari kipindi cha mgomo na hata alidiriki kujaribu kupinga ongezeko la posho ya wabunge kumbe danganya toto.
Eti leo bila aibu Hamisi anawashauri CHADEMA wasimsimamishe mgombea Arumeru Mashariki eti ni uharibifu wa fedha! Kama kweli ana uchungu na fedha za watanzania mbona hajawashauri mafisadi wakubwa wa CCM wa EPA, Richmond, Kagoda, IPTL nk?
Leo nimeamini kuwa huyu Kigwangallah ni mnafiki namba moja na hafai na ndani ya CCM hamna kiongozi hata mmoja anayeweza kusimamia maslahi ya Taifa hili, ila 2015 siyo mbali!
 
Katika wabunge waliopo madarakani sasa nani anatetea vijana zaidi ya Kigwangalla? Nani amekubali kuwekwa ndani kwa maslahi ya wapiga kura wake na serikali ikasikia, ikakiri kosa lake na kuwarudishia wananchi wa Nzega mgodi wao?
demokrasia ina gharama kubwa,hata ikatokea mkafa wabunge wote lazima uchaguzi ufanyike.Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia ndani ya mfumo wa vyama vingi.Fikra mgando ni ombwe kubwa la uongozi,heri uchi wa nyama kuliko uchi wa akili,poleni sana watu wa magamba.Nzega bado hawajalipwa haki zao mara baada ya kunyang'anywa ardhi na kupewa wakoloni,ziko wapi harakati zako ulizozianzisha,au ndiyo unajaribu ku-cope toka wana CCM mara baada ya mkwara wa Ridhiwan,kuwa mbona unawageuka hutaki kuwasaidia wakati wao walikusaidia kupata ubunge!Mpiganaji makini kama Che-Guevera haangali rangi ya bendera katika mapambano ya harakati za Mtanzania maskini.
 
Back
Top Bottom