Wewe ulisema wengi wanafata kwa sababu walizaliwa kwenye familia za dini hizo, na iwapo wangezaliwa kwenye dini nyengine basi wangekuwa waumini wa dini nyengine.
Kwa mantiki hiyo hayo ni kufata mkumbo tu.
Na kama unafata mkumbo tu, unajadili na mwengine ili iweje?
Tatizo lao dini zao haziwafundishi kuchukia dini zingine, lakini "mapokeo" yao yanawafanya wazichukie dini zingine!!lile jukwaa sio kabisa mara buchanan sijui anakuja na posti ohhh mbuzi ala quran, nguruwe alalia quran
hata huwa siwaelewi
Mimi nadhani mambo ya dini huwafanya watu wajisikie wakosefu muda wote na ni dhaifu. Lakini pia dini kubwa duniani (ukiondoa Ubudha) zimejengwa katika misingi ya Uhasama wa Mashariki ya Kati. Wakristo wanaamin Ibrahim alimzaa Isaka ambaye ni chimbuko la wana Israel ambao ndiyo msingi wa ukombozi wa wanadamu kupitia Yesu Kristo ambaye ni uzao wa Daudi.
Lakini Waislamu wanaamini Ibrahim alimzaa Ishmael ambaye ndiye chanzo cha sehemu kubwa ya Waarabu ambao nao wao pia wanamuona Ibrahim kama baba wa Imani kama wakristo wanavyoamini. Wakati ugomvi wa waarabu na Israel ni wa Kihistoria na wala hauhusiani na dini hizi za Kiislam na Kikristo, waumini wa dini hizi mbili wanadhani ugomvi huo ni sehemu ya dini zao. Kumbuka Wafilisti ndiyo Wapalestina!!
Leo hii muislamu wa Tanzania anaamini kwamba anapoitetea Palestina (ingawa kuna wapalestina wakristo) dhidi ya Israel (ingawa Waisrael wengi 90% hawaamini katika Ukristo) anakuwa anautetea Uislam, na Mkristo naye anasisimka anapoitetea Israel kwa kuamini kuwa ni taifa teule la mungu.
Kwa hiyo Kwenye Jukwaa la dini huwa mitusi inaporomoka hovyo hovyo kwa sababu dini hizi mbili zimejengwa juu ya msingi wa kiuhasama na wao waliozisanifu (Siyo Mtume S.A.W au Yesu Kristo) nje ya msingi uliowekwa na waasisi wa dini hizi ambao ni upendo, amani, mshikamano, nia njema. Ndiyo maana salaam ya "Asalam aleykhum" ina mantiki katika kujenga hoja ya Uislam lakini ni waislam wangapi wanaoamini kwamba hata wasio waislam nao wanatakiwa kuishi kwa Amani? Kama yesu alikuja kuwakomboa wanadamu ni ukombozi gani unaotenga sehemu ya wanadamu hao mbali?
Sijakuelewa kabisa Kongosho. Mimi nilikuwa najaribu kueleza ni kwa nini kwenye jukwaa la dini kuna vurumai ya kurushiana matusi. Lakini sijaelewa ni kwa nini umeni quote na kuandika ulichoandika!!Kuna toafauti ya kukariri, kuelewa, kuchanganua
Unaona kitu unachotaka kuona
Na kama unataka kufahamu zaidi pitia historia za kidunia za dini
Ili uweze kuunganisha na misahafu
Hata dini zina stages of growth.
Mantiki ya hiyo red ilikuwa heshimu anachoamini mwingine, maana hata anayeamini kingine ni kwa sababu alijikurta katika mazingira hayo.
Sijakuelewa kabisa Kongosho. Mimi nilikuwa najaribu kueleza ni kwa nini kwenye jukwaa la dini kuna vurumai ya kurushiana matusi. Lakini sijaelewa ni kwa nini umeni quote na kuandika ulichoandika!!
Kuamini kwa sababu ulijikuta kwenye mazingira tu, ni kufuata mkumbo
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.
Ndio nimesikia
Lakini sijaona ni vipi inahusiana na post yangu ulo-quote hapo juu
uhusiano ndo huo hapo