Uwiiiiiii shetani amelalia watu vichwani

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
7,484
5,142
Nimeona nilete hii hoja huku kwenye wengi badala ya kuipost kwenye jukwaa la dini ili meseji ifike kwa wahusika kirahisi. Ni hivi, mbona mada za dini kule kwenye jukwaa husika hazina wachangaiaji wengi? Member wenye access ya jukwaa ni wengi ila mada zikipostiwa utakuta zina wachangiaji hata 10 saa nyingine hawafiki! Mfano mzuri ni mada ya imani na miujiza aliyoposti dada/kaka mmoja (nimemsahau jina) toka juzi hadi muda huu ina michango 3 tu! Hii ni hatari kubwa kwa kizazi cha leo kwani shetani ameamua kuwatawala na kuhakikisha mnabanwa na mada za ulimwengu huu na kuona mada za kiroho kama hazina mshiko! Amelaaniwa yeye ambae hatangulizi mambo ya kiroho mbele......., nimefikisha ujumbe na ukumbuke mjumbe hauwawi!!!
 
message delivered. ubarikiwe kwa kuona hilo.
 
Huko kwenye jukwaa la dini visinizio kibao ohoooooo ni kashfa kwa imani ya watu, mara ohooo kila mtu na imani yake. N.k.
 
Mada za sasa hivi kule inabidi mtu asikurupuke kwani kwenye mambo haya ya imani inabidi mtu kuwa makini sana unapojibu hoja za watu, kwa kule ni wepesi sana kuanzisha mada lakini ni vigumu sana kujibu hoja ukakinaisha wengi. Utaona hivi karibuni baada ya kupigiwa kelele na wadau wengi kuwe na nidhamu na marekebisho ya uchangiaji uwe wa kiheshima pamekuwa shwari kidogo na watu wengi wamejirekebisha na hawajibu kwa kukurupuka kama huku kwenye majukwaa mengine.

Pia nadhani hako kashetani kapo kweli kazini.
 
Kama ni mada inayokuhusu kwa nini usichangie??
Mwehu akikupiga na yai vinza unataka urudishe??
Wewe changia, akikutukana mpishe kama huoni
Hata rudhia siku nyingine.

Wengine wapo kwa ajili ya ku-undermine imani za watu
Wengine hawana kabisa imani
Tunashindwa kujua kwamba tukiangalia kwa undani
Hakuna au wachache sana waliochagua imani ukubwani
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.

Mi nadhani tukiheshimu hili
Litatusaidia kuheshimu imani za wengine
Kule huwa napita tu ni matusi tu nashukuru sijawahi kuchangia chochote.
 
Wasichangia jukwaa la dini labda ni kwa sababu hawaamini hizo dini, na uwezekano mkubwa ni kuwa hawaamini na huyo shetani
 
Tunashindwa kujua kwamba tukiangalia kwa undani
Hakuna au wachache sana waliochagua imani ukubwani
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.

Kwa hiyo mnafata tu bila ya kutafuta ukweli umesimama wapi?
Na ikiwa ni hivyo, majadiliano na watu wanaofata mkumbo tu, yana faida kweli?
 
Siku zote huwezi linganisha utamu wa nyama na chumgwa
Haitaleta maana
Linganisha chungwa kwa chungwa na nyama kwa nyama

Anayeamini na asiyeamini mjadala pekee naouona wanaweza wakashare ni kuulizana kwa nini unaamini na kwa nini wewe huamini

Ikishaningia kwa waaminio kujadili mambo wanayoyaamini sioni ni kwa point gani asiyeamini anaweza akachangia zaidi ya kuheshimu mijadala yao. Wanakuwa wanaongea lugha tofauti kabisa hapo.

Sasa kwa anayetaka kuutafuta huo ukweli wa aidha kuna haja ya kuamini au la aende kwenye mijadala hiyo itampa majibu ya maswali yake.

Sidhani ni sahihi kusema 'Uamini kwa kufuata mkumbo' ni sawa sababu hulazimishwi na wala hukataliwi kutafuta kweli unayoitaka.

Ita apple by apple theory.

Kwa hiyo mnafata tu bila ya kutafuta ukweli umesimama wapi?
Na ikiwa ni hivyo, majadiliano na watu wanaofata mkumbo tu, yana faida kweli?
 
Kama ni mada inayokuhusu kwa nini usichangie??
Mwehu akikupiga na yai vinza unataka urudishe??
Wewe changia, akikutukana mpishe kama huoni
Hata rudhia siku nyingine.

Wengine wapo kwa ajili ya ku-undermine imani za watu
Wengine hawana kabisa imani
Tunashindwa kujua kwamba tukiangalia kwa undani
Hakuna au wachache sana waliochagua imani ukubwani
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.

Mi nadhani tukiheshimu hili
Litatusaidia kuheshimu imani za wengine
Umewahi kusikia kuhusu 'independent investigation of the truth?'
 
Kama ambavyo sio kila anaeenda kanisani anaamini anachofundishwa kule na kujaribu kuyafanyia kazi kwenye maisha yake , na sio kila asieenda haamini/hafuati maandiko ndivyo ilivyo hiyo ya uchangiaji. Yote ni maamuzi ya mtu binafsi. Hamna haja ya kuchangia ili nionekane sijalaliwa na shetani kichwani, ila kuna haja ya kufanya yale yanayoniridhisha mimi mwenyewe na Mungu wangu.
 
Nakubaliana na wewe
Usichangie kwa sababu hujisikii kuchangia
Lakini si kwa sababu watu wengine watakutukana
kwa hiyo unaacha kuchangia kuepusha shari

....mnabanwa na mada za ulimwengu huu na kuona mada za kiroho kama hazina mshiko!...
Hili nalo linahitaji mjadala....mpaka upo wapi?....mambo ya kiroho yanaishia wapi na yale ya ulimwengu yanaanzia wapi?...hasa ukizingatia 'ukweli' kuwa Mungu ndiye 'muunba wa vitu vyote'!
 
Nakubaliana na wewe
Usichangie kwa sababu hujisikii kuchangia
Lakini si kwa sababu watu wengine watakutukana
kwa hiyo unaacha kuchangia kuepusha shari

Hehehe kutukanwa mbona hata chiti chati kupo aisee?
Mi siku nikiogopa kutukanwa wakati hayo matusi yanapita kama ufanyavyo upepo ntafungia vioo ulimwengu wote.
 
Siku zote huwezi linganisha utamu wa nyama na chumgwa
Haitaleta maana
Linganisha chungwa kwa chungwa na nyama kwa nyama

Anayeamini na asiyeamini mjadala pekee naouona wanaweza wakashare ni kuulizana kwa nini unaamini na kwa nini wewe huamini

Ikishaningia kwa waaminio kujadili mambo wanayoyaamini sioni ni kwa point gani asiyeamini anaweza akachangia zaidi ya kuheshimu mijadala yao. Wanakuwa wanaongea lugha tofauti kabisa hapo.

Sasa kwa anayetaka kuutafuta huo ukweli wa aidha kuna haja ya kuamini au la aende kwenye mijadala hiyo itampa majibu ya maswali yake.

Sidhani ni sahihi kusema 'Uamini kwa kufuata mkumbo' ni sawa sababu hulazimishwi na wala hukataliwi kutafuta kweli unayoitaka.

Ita apple by apple theory.

Wewe ulisema wengi wanafata kwa sababu walizaliwa kwenye familia za dini hizo, na iwapo wangezaliwa kwenye dini nyengine basi wangekuwa waumini wa dini nyengine.

Kwa mantiki hiyo hayo ni kufata mkumbo tu.

Na kama unafata mkumbo tu, unajadili na mwengine ili iweje?
 
  • Thanks
Reactions: bht
Mimi nadhani mambo ya dini huwafanya watu wajisikie wakosefu muda wote na ni dhaifu. Lakini pia dini kubwa duniani (ukiondoa Ubudha) zimejengwa katika misingi ya Uhasama wa Mashariki ya Kati. Wakristo wanaamin Ibrahim alimzaa Isaka ambaye ni chimbuko la wana Israel ambao ndiyo msingi wa ukombozi wa wanadamu kupitia Yesu Kristo ambaye ni uzao wa Daudi.

Lakini Waislamu wanaamini Ibrahim alimzaa Ishmael ambaye ndiye chanzo cha sehemu kubwa ya Waarabu ambao nao wao pia wanamuona Ibrahim kama baba wa Imani kama wakristo wanavyoamini. Wakati ugomvi wa waarabu na Israel ni wa Kihistoria na wala hauhusiani na dini hizi za Kiislam na Kikristo, waumini wa dini hizi mbili wanadhani ugomvi huo ni sehemu ya dini zao. Kumbuka Wafilisti ndiyo Wapalestina!!

Leo hii muislamu wa Tanzania anaamini kwamba anapoitetea Palestina (ingawa kuna wapalestina wakristo) dhidi ya Israel (ingawa Waisrael wengi 90% hawaamini katika Ukristo) anakuwa anautetea Uislam, na Mkristo naye anasisimka anapoitetea Israel kwa kuamini kuwa ni taifa teule la mungu.

Kwa hiyo Kwenye Jukwaa la dini huwa mitusi inaporomoka hovyo hovyo kwa sababu dini hizi mbili zimejengwa juu ya msingi wa kiuhasama na wao waliozisanifu (Siyo Mtume S.A.W au Yesu Kristo) nje ya msingi uliowekwa na waasisi wa dini hizi ambao ni upendo, amani, mshikamano, nia njema. Ndiyo maana salaam ya "Asalam aleykhum" ina mantiki katika kujenga hoja ya Uislam lakini ni waislam wangapi wanaoamini kwamba hata wasio waislam nao wanatakiwa kuishi kwa Amani? Kama yesu alikuja kuwakomboa wanadamu ni ukombozi gani unaotenga sehemu ya wanadamu hao mbali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom