UWEZO WA WATANZANIA: Judge Augustino Ramadhani - Anasoma Hukumu Nairobi Kenya

Arusha Mambo

Senior Member
Jan 27, 2011
174
150

Muhimu:
Arusha Mambo italeta sehemu ya hukumu inayosomwa na Judge Agustino Ramadhani jijini Nairobi, hukumu hiyo inayofuatia tukio la Kiongozi wa juu katika Serekali ya Kenya NANCY BARAZA la kumtishia mlinzi (Korokoroni) Silaha baada ya kutakiwa kufuata utaratibu wa kupekuliwa kabla hajaingia kwenye jengo lililokuwa linalindwa na Mlinzi huyo.

Judge Agustino Ramadhani anasoma hukumu hiyo kwa ufasaha wa hali ya juu,
tunawakilishwa kwa Ubora usiopimika, Wakenya wanamsikiliza kwa umakini Mkubwa huku akichambua vifungu vipya vya kisheria vya Katiba ya Kenya na vifungu mbalimbali vya Sheria za Kimataifa.

Hukumu hiyo itawajia mara tu baada ya kusitishwakwa kikao cha Bunge Mjini dodoma.

Ili kusikiliza bonyeza hapa:
http://tunein.com/tuner/?StationId=158711&

Redio ikifunguka usiache ku
LIKE na kutuma maoni yako kwa info@arushamambo.com
 
Jopo la wanachama saba likiongozwa na Jaji Mstaafu wa Tanzania Mh. Agustino Ramadhani limesema Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza alifanya makosa kwa kumchuna pua na kumtisha na silaha Mlinzi wa Village Supermarket mjini Nairobi.

Jaji Ramadhani bila utani amesema Jaji huyo akiwa kama Kiongozi wa juu alikiuka Maadili na amependekeza kwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki amvue madaraka Jaji huyo pamoja na mchango wake mkubwa alioutoa katika mabadiliko ya Katiba ya Kenya na Serekali, amesisitiza kuwa kwa kitendo alichokifanya hastahili kuwa katika nafasi hiyo.

Mheshimiwa jaji ametuwakilisha vizuri sana hasa kwa usomaji wa hukumu hiyo na uelewa wa sheria aliouonyesha.
 
kwa tanzania hao majaji wanaotoa hukumu za upendeleo wa kichama lini nao wataundiwa tume?
 
huyu mzee ni noma yaani kampiga chini Jadge Mwenzake bila aibu, tena nasikia huyu Nancy ndio alikuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya Katiba ya Kenya kwenye Kipengele cha Haki za Binadamu halafu yeye mwenyewe ndio akawa wa kwanza kuzivunja, sheria inakata mara mbili aisee,

tumuombe asaidie ile kesi ya Lema, mbona rufaa hatuisikii?
 
Jaji Augustino Ramadhani ni competent huwezi kufananisha na Majaji vilaza anaoteuwa ,,,Msaniii.....ambao hata Tume ya Utumishi wa Mahakama haiwajuwi
 
Hawa majaji wetu kumbe wanafanya kazi vizuri nje ya nchi tu.
 
nadhani kinachomsadia sana huyu mzee ni kujitahidi sana kuwa Mcha Mungu. Hili linamuondolea hata dharau na majigambo, anaheshimu sana watu.
Mimi namuona hivyo!
 
sio majaji tu hata madoc ,na wataalamu wengine kama giologist wengi wameend kwenye migodi zambia kongo zimbabwe yaani unaweza kuwsili mgodi uliopo zambia ukafikiri upo tz .
hawa wanasoma kwa kodi yako na ya yule then hawapewi kazi au mshahaa kiduchu huko nasikia wanakula usd
kwa maelfu
 
nadhani kinachomsadia sana huyu mzee ni kujitahidi sana kuwa Mcha Mungu. Hili linamuondolea hata dharau na majigambo, anaheshimu sana watu.
Mimi namuona hivyo!

Nadhani huo ni uadilifu na ni sifa kuu ya kuwa jaji...sio Majaji was Siku hizi Hawana maadili ....wanashinda mitaani ....Nadhani pia ni Madhara ya serikali kutowapa Makazi stahiki....na hata clubs Kama leaders ambapo wanastahili kustrarehe wanapiga twanga pepeta ....
Majaji waliomtangulia Augustino Ramadhani ...Kama ...Saidi,Nyalali etc pia walikuwa waadilifu......Jaji mkuu Tatizo ni huyu aw sasa .....theye mwenyewe ni kilaza na Majaji wapya wingi wao vilaza....Majaji Wenye misimamo hawapewi kesi ngumu.....kesi zote za karibuni za serikali wanapewa Majaji wapya walipe fadhila...za uteuzi..
 
Jopo la wanachama saba likiongozwa na Jaji Mstaafu wa Tanzania Mh. Agustino Ramadhani limesema Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza alifanya makosa kwa kumchuna pua na kumtisha na silaha Mlinzi wa Village Supermarket mjini Nairobi.

Jaji Ramadhani bila utani amesema Jaji huyo akiwa kama Kiongozi wa juu alikiuka Maadili na amependekeza kwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki amvue madaraka Jaji huyo pamoja na mchango wake mkubwa alioutoa katika mabadiliko ya Katiba ya Kenya na Serekali, amesisitiza kuwa kwa kitendo alichokifanya hastahili kuwa katika nafasi hiyo.

Mheshimiwa jaji ametuwakilisha vizuri sana hasa kwa usomaji wa hukumu hiyo na uelewa wa sheria aliouonyesha.

Muache amalizie, lakini akirudi tu nyumbani ajiandae kutuambia ni Zimwi gani linawatisha majaji wetu kutoa hukumu za haki na mapendekezo yenye maslahi kwa UMA wa watanzania?? na tutaka atoe majibu yake bila kumuogopa mtu kama anavyofanya uko ugenini.
 
hivi majaji vilaza ni kina nani hakuna mtu anamajina yao, tuijue jamani hiyo mizigo iliyoko mahakama kuu, nasikia wengine hata kiingereza ni shida
 
nadhani kinachomsadia sana huyu mzee ni kujitahidi sana kuwa Mcha Mungu. Hili linamuondolea hata dharau na majigambo, anaheshimu sana watu.
Mimi namuona hivyo!

Si wewe tu, Jaji Augustino Ramadhani hana makuu na cheo kwake hakikumfanya ajione tofauti na wengine kama ambavyo tunawaona viongozi wengine wanavyojikuza. Jaji Ramadhani ni mpole sana na yuko very humble. Kabla hajastaafu alikuwa anaweka siku maalumu kwa wiki ya kusikiliza watu wenye shida. Huwa napenda anavyopiga kinanda kanisani.
 
Nadhani huo ni uadilifu na ni sifa kuu ya kuwa jaji...sio Majaji was Siku hizi Hawana maadili ....wanashinda mitaani ....Nadhani pia ni Madhara ya serikali kutowapa Makazi stahiki....na hata clubs Kama leaders ambapo wanastahili kustrarehe wanapiga twanga pepeta ....
Majaji waliomtangulia Augustino Ramadhani ...Kama ...Saidi,Nyalali etc pia walikuwa waadilifu......Jaji mkuu Tatizo ni huyu aw sasa .....theye mwenyewe ni kilaza na Majaji wapya wingi wao vilaza....Majaji Wenye misimamo hawapewi kesi ngumu.....kesi zote za karibuni za serikali wanapewa Majaji wapya walipe fadhila...za uteuzi..

Jaji wa sasa ni kilaza? mbona ana nywele nyeupe au ndio yaleyale ya Edo?
 
Manabii wasiokubalika kwao! Ni kwa nini wanapofanya kazi huku kwetu wanafanya kwa unafiki wa kisiasa kuliko taaluma yao?
 
Muhimu:
Arusha Mambo italeta sehemu ya hukumu inayosomwa na Judge Agustino Ramadhani jijini Nairobi, hukumu hiyo inayofuatia tukio la Kiongozi wa juu katika Serekali ya Kenya NANCY BARAZA la kumtishia mlinzi (Korokoroni) Silaha baada ya kutakiwa kufuata utaratibu wa kupekuliwa kabla hajaingia kwenye jengo lililokuwa linalindwa na Mlinzi huyo.

Judge Agustino Ramadhani anasoma hukumu hiyo kwa ufasaha wa hali ya juu,
tunawakilishwa kwa Ubora usiopimika, Wakenya wanamsikiliza kwa umakini Mkubwa huku akichambua vifungu vipya vya kisheria vya Katiba ya Kenya na vifungu mbalimbali vya Sheria za Kimataifa.

Hukumu hiyo itawajia mara tu baada ya kusitishwakwa kikao cha Bunge Mjini dodoma.

Ili kusikiliza bonyeza hapa:
http://tunein.com/tuner/?StationId=158711&

Redio ikifunguka usiache ku
LIKE na kutuma maoni yako kwa info@arushamambo.com

Nasisi tungeunda ya kwetu na Jaji kutoka nje kwa ajili ya Dk.Ulimboka
 
Jopo la wanachama saba likiongozwa na Jaji Mstaafu wa Tanzania Mh. Agustino Ramadhani limesema Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza alifanya makosa kwa kumchuna pua na kumtisha na silaha Mlinzi wa Village Supermarket mjini Nairobi.

Jaji Ramadhani bila utani amesema Jaji huyo akiwa kama Kiongozi wa juu alikiuka Maadili na amependekeza kwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki amvue madaraka Jaji huyo pamoja na mchango wake mkubwa alioutoa katika mabadiliko ya Katiba ya Kenya na Serekali, amesisitiza kuwa kwa kitendo alichokifanya hastahili kuwa katika nafasi hiyo.

Mheshimiwa jaji ametuwakilisha vizuri sana hasa kwa usomaji wa hukumu hiyo na uelewa wa sheria aliouonyesha.

Amesoma hukumu au ripoti ya tume? kumbuka alikuwa hasikilizi kesi, bali alikuwa kiongozi wa tume iliyoundwa kuchunguza tukio hilo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom