Hivi karibuni kesi maarufu ya akina Zombe ilimalizika kwa serikali kubwaga vibaya. Wapo walioona kuwa mahakama haikutenda haki kwa ndugu wa wafia. Lakini binafsi naamini suala halikuwa mahakama bali ni uwezo wa wanasheria wa serikali.
Leo katika gazeti la daily news, kesi ya Liyumba imeripotiwa. Kwa akili ndogo kabisa hata bila kuhitaji taaluma ya sheria utaona kuwa upande wa mashtaka unafanya utani maana ushahidi wao umejaa mapungufu makubwa. Km na mashihidi watakaofuata watatoa ushahidi wa aina ile basi muda si mrefu Liyumba atarejea kazini.
Kama hawa ndio wanasheria wanaotegemewa nchini, nini mustakbali wa nchi yetu?