UWEZO Education research??!!

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,028
Wan Jf

kwa mtu anayeijua kwa undani taasisi hii naomba anijuze. Inafanya kazi kama zile za Haki Elimu??!!!!! data zao nikizisoma zinanishangaza kabisa!

mwenye detail please
 
Uwezo Tanzania ni mradi wa miaka minne unaofanya utafiti kuona ujifunzaji wa watoto wetu mashuleni. Wazo la mradi huu lilikuwa-adopted kutoka India ambapo huko kumefanyika utafiti kama huu unaojulikana kwa jina la ASER na kuleta mafanikio makubwa. Wanazuoni wetu walikwenda huko na kujifunza jinsi wenzetu walivyofanikiwa katika utafiti wao na kuja ku-introduce idea hii katika East Africa.

Mradi huu uko katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na kwa pamoja unaitwa Uwezo East Africa Initiative. Utafiti huu unafanyika kwenye kaya, mashuleni na kwa viongozi wa mitaa na kata,badala ya mashuleni tu kama zililvyo tafiti nyingi zilizowahi kufanyika. Hili linasaidia kupata makundi yote ya watoto ukizingatia kuwa ukifanya utafiti shuleni tu hutapata takwimu zenye uhakika kwa kuwa kuna watoto wenye umri wa kwenda shule lakini hawapatikani darasani na wakati mwingine walimu watakuchagulia wanafunzi wanaofanya vizuri ili waonekane wanafanya kazi barabara. Kwa kufanya utafiti nyumbani tunapata watoto wanaosoma, walioacha shule kwa sababu mbali mbali, ambao hawakuwahi kuandilkishwa kabisa, walemavu waliofichwa au kushindwa kupelekwa shule kutokana na sababu mbalimbali nk.

Mradi huu umefanikiwa sana, data zake ni za uhakika kwani hakujawahi kufanyika utafiti wa aina hii katika Tanzania wa kupita kaya hadi kaya. Ndiyo maana unaona jinsi takwimu zake zilivyoweka kuchokonoa yaliyomo na kuweka bayana uozo ambao umejificha kwa miaka mingi wakati tafiti nyingi zinazofanywa na serikali na vyombo vyake zikiimba nyimbo za sifa wakati wote.

Uwezo kazi yake ni kufanya research tu, lakini kwa Haki Elimu pamoja na research wana mambo mengine kama advocacy, governance na mengine mengi, lakini wote wana lengo la kuona kiwango cha elimu Tanzania kinainuka.

Nikiwa kama mmoja wa District Coordinators katika utafiti huu wa Uwezo ninakuwa ni shuhuda wa kwanza katika yale yanayoongelewa kwenye ripoti ya Uwezo, japo selikali yetu inaonesha kutoipenda sana kwa sababu wanazozijua wao lakini huo ndiyo ukweli wenyewe na ukweli wakati wote huwa unauma.

Watanzania wenzangu tufungue macho hali si shwari sana.

Hayo ni machache kati ya mengi niliyoweza kukueleza leo juu ya project hii ya Uwezo, sijui kama nitakuwa nimetii kiu yako. Samahani kwa uandishi mbovu na karibu tena.
 
Pia ungeeleza na uhusiano wa Mradi huo na Taasisi ya Twaweza, ambayo mwanzilishi wake ni Bw. Rakesh Rajan ambaye pia ni mwanzilishi wa Haki Elimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom