Uwezekano wa kuhama Mfuko wa Hifadhi ya Jamii

kajumula.

Member
Jun 29, 2012
34
0
Kuna taarifa kuwa kuna sheria za mifuko ya jamii zinazokusudiwa kanzishwa lengo ikiwa ni kumbana mteja- mwanachama wa mifuko hiyo. Nijuavyo mimi mifuko hii ilianzishwa ili kumuudumia mteja aliyejisajili, na mifuko hii inawajibika moja kwa moja kwa wateja wake. Swali ni je ikiwa kuna sheria zinakusudia kumbana mteja kiasi kwamba akisha jiunga na mfuko mmoja wapo kati ya hiyo mifuko hataruhusiwa kuhama,au kusitisha mkataba mpaka kwa kiwango cha mda flani na kwa kutimiza kiwango fulani cha mchango wake....mimi naona si sawa..Je sheria hizi ni kwa manufaa ya nani na zinakusudia nini?

WATANZANIA TUSIKUBALI..
 
Nashindwa kabisa kuelewa ilikuaje mhimili wenye mamlaka ya kutunga na kupitisha sheria kuipitisha sheria hii.ina maana sheria hiyo ilipitishwa bila kujadiliwa???maana ni wazi kabisa imewekwa kuwanyonya wananchi waliokuwa wakifaidika na mfuko huo.
 
Kiswahili cha watanzania nakipenda sana lakini waliotafsiri pension= mifuko ya jamii(i hope i got it right) kwa maoini yangu hawakuona utatanishi unaoweza kuletwa na Direct translation(kwa kiswahili ni nini?) iwe bodybags?
 
Ndugu wana Jf ningeomba kwa mwenye taarifa anifahamishe iwapo inawezekana kuhama kutoka mfuko mmoja wa hifadhi ya jamii kwenda mwingine bila kubadili mwajiri mfano toka nssf kwenda ppf .
 
Ongea na HR wako, mtoe mtonyo, zeni atakuandikia barua ya kufukuzwa kazi, afu unaenda fwata mafao yako ya kujitoa.
 
Unaweza hama pale tu unapoacha kazi kampuni moja na kuhamia kampuni nyingine
 
kwa sasa bado hakuna mfumo wa kuhamisha mafao kutoka mfuko mmoja kwenda mfuko mwingine, cha kufanya we kachukue SPECIAL LUMPSUM / GRATUITY ila hayo ya transfer nadhani SSRA bado hawajafika mwafaka
 
Kwa mujibu wa ssra walizema inawezekana ila kiuhalisia ni ngumu sana mpaka labda uache kazi ujiunge mfuko mwingine hapo ndio inawezekana.
 
Hao SSRA ni wasanii tu,sijaona kazi wanayoifanya
 
ukitaka kujitoa watakupj gharama za kujitoa ambazo ni nusu ya mafao yako yote. SSRA wanalinda mifuko yenye wizi isikimbiwe na watu
 
Hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa wakuu.

Ningependa kufahamu iwapo kuna uwezekano wa mtumishi aliyejiunga na mfuko mmoja wa hifadhi ya jamii kuhama na kujiunga na mfuko mwingine iwapo atagundua mapungufu katika mfuko aliyopo.

Mfano. mtumishi aliyejiunga na mfuko wa PPF anaweza kujiondoa na kujiunga na PSPF? Kama jibu ni ndiyo, upi utaratibu wake?
Nimeulizwa swali na kijana wangu nami kwa kuwa si mtaalamu sana katika hilo, na nafahamu familia ya JF kubwa mno na yenye utaalamu na uzoefu tofauti tofauti hivyo naomba ushauri wenu wadau. Karibuni...
 
Mpaka wakati huu nacomment haikubaliki!!!. Chukua withdrawal benefit yako sepa nayo, register upya kwenye mfuko mpya kama ni contract umebadili. Kama unaendelea kazini basi BIG NO
 
Wadau,

Naombeni msaada juu ya hili,mm ni mtumishi wa Umma ni mtumishi mpya,kwa bahati mbaya sikupata maelezo ya kutosha juu ya mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii nimejikuta nimejiunga na mfuko ambao hauna mafao bora hivyo nataka kuhama kuhamia mfuko mwingine,swali langu je inawezekana kwa mtumishi wa umma kufanya hivyo,kama inaezekana taratibu zikoje?
 
Back
Top Bottom