Uwekaji wa password kwenye simu kwa wapenzi/kwenye ndoa

Habarini wana JamiiForums, heri ya Mwaka mpya.

Naomba kuuliza kuwa ni sahihi kuweka pattern kwenye simu kwa wale wanandoa au wachumba. Kwani kwa wanandoa ni tayari mmeshakuwa mwili mmoja na hakuna siri baina yenu mnatakiwa kuwa wazi kwa kila mnalofanya.

Na kwa wale wachumba tena hao ndo hawafai kabisa kufichana kitu kwani wao wanakaribia kuwa Mwili mmoja kwanini wanaweka hizo pattern kwenye simu.

Karibuni wakuu kuchangia.
 
Simu yangu kila unachotaka kufungua inakudai password, ata kuangalia saa inabidi ujue password, tena hazifanani
Cc Evelyn Salt
 
Last edited by a moderator:
kuna watu hodari wa kushika pattern za watu, yani ukichora mara moja afu ukaacha sim hapo, utajutaaa
 
Kwani wakati tunafungishwa ndoa tuliambiwaje?

Ni kifo tu kitakacho watenganisha, sio 'pattern' password.

Therefore, i may conclude that; 'Kila jambo lenye dalili za kutenganisha ndoa, lazima likemewe vikali, no matter how, by hooks and crooks'

Thanks.
 
pattern inategemea sana maybe kwenye ndoa watoto watundu, halafu hata aweke password mie sina habari nachojua ni marufuku kushika sim ya mwenzangu mana si yangu kisa cha kujitia bp za nini?
 
password inasaidia vitu vingi, kuna baadhi ya simu usipoweka password huko mfukoni ikijigonga gonga na paja mwisho wa siku inajipiga, sio password ni muhimu
 
Simu yangu haimuhusu mtu mwingine kila mtu ana privacy zake bila kujali mko kwenye ndoa na sitakiwi kufuatilia simu ya mwingine nachukia mtu anashika simu yangu alafu anakimbilia kuangalia vilivyomo.
 
Simu yangu haimuhusu mtu mwingine kila mtu ana privacy zake bila kujali mko kwenye ndoa na sitakiwi kufuatilia simu ya mwingine nachukia mtu anashika simu yangu alafu anakimbilia kuangalia vilivyomo.

ninawasi wasi nawewe
 
Back
Top Bottom