Uwekaji wa password kwenye simu kwa wapenzi/kwenye ndoa

...simu ya kwake. hata alifungia kufuli
cell-phone-lock.jpg

ni sawa tu, si ya kwake? ...Invasion of privacy yana kikomo chake bana.
Hata mimi sipendi na wala sitaki kuulizwa yaliyomo kwenye simu yangu.
Hata mwili ni wake....na pesa ni zake...marafiki ni wake...ndugu ni zake ila mnashea!!Tatizo ndo lije kua simu?!
 
Mimi na mume wangu tunashare PW mpaka za e mail nini simu. Hata kama haizuii mtu kucheat inatufanya tu feel good and confident with one another. Mimi hata nikute meseji kwenye e mail za hubby ya msichana kama si ya mapenzi na ninamjua wala sijali na wala siijibu. Kikubwa ni kuto misuse simu na e mail za wenza wetu.

Nina hakika wale ambao mmewekewa PW mnajisikia vibaya. Kwa hiyo enyi wanaume wenye kuweka mi PW hacheni huo mchezo mnanyima amani wenzenu.

Hata kama mnacheat si muwaambie hao wanawake kuwa mumeoa wasiwasumbue ovyo!
 
Jamani kuna umuhimu wowote simu za wapenzi wawili kuwana na password? let say mke na mme au mtu na mchumba wake wanaulazimu wa kuweka password?

yap! Kunaulazima ilimrad kila mmoja atakuwa anamuheshimu i mean anamuamin mwenzie kwan simu kuwa na password kunatatzo gan? Haina shda anaweza kutoweka password na bado akawa ANAMULIKA MWIZI WA MAPENZ so chamsing ni kuheshimiana na kuhaminiana full-stop
 
If you can't give me such a small thing like PW to your phone, can you give me a PW to your heart?
 
Haitakiwi kusema kweli wala haipendezi ... ila kuna wakati wenza wengine anafuatilia mambo madogo madogo anataka kujua kila simu kila message hata kama si mbaya mpaka kichwa kinakuuma kila siku mnagombana sababu ya simu... Hapo hamna jinsi kuepusha shida its better uweke pin...
 
If you can't give me such a small thing like PW to your phone, can you give me a PW to your heart?

Nafikiri kwa vile Moyo pia una chamber nne (2 ventricles & 2 Auricles) utaulizwa unataka PW ya chamber gani? kwami kila chamber ina mtu!!!
 
Watu bwana kwa vimisemo vya kujustify vitendo viovu!!!!! msemo mzuri thou

Gaga sikutegemea unaweza kuni-attack personally badala ya point niliyoielezea. Sishangai kutofautiana mawazo maana mm ni mwanaume na wewe ni mwanamke (I suppose), kuna mambo-hasa ya mahusiano tunaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa. Mi napinga suala la kufuatiliana ktk vitu kama simu, mail inbox, fcbk nk kwasababu mwisho wake sio ule wenggi tunaotarajia. Kuna askari wa NYPD-USA amejiua (check yahoo news) kisa ni messages za facebook alizoziona alipotembelea page ya mpenzi wake. Sam Wanjiru mwanariadha wa Kenya amekufa jana kwasababu ya mambo haya haya ya kufautiliana. Wengi tunapenda kufuatilia wenzi wetu bila kujua tukiupata ukweli tutafanya nini.

So narudia kama unataka kuachana na mpenzi wako, tafuta sababu kwenye simu na communication media nyingine utaipata. Kimsingi hakuna tija ktk kuchunguza simu ya mwenza wako, maana unaweza usione kitu kwenye simu ukadhani mambo ni shwari, kumbe mwenzio yupo na housegirl wako na hawahitaji mawasiliano ya simu maana wote wapo nyumba 1. Ukitaka kumjenga mwenzako, mwamini hata kama unaona kwa wakati huo haaminiki, hiyo itamjenga kuliko ya kugombana nae kila siku sababu ya msg-hii inajenga ufa kati yenu. Mwisho, nimewasikia wanawake wangi wakisema "kama anafanya mambo yake, afanye mbali nisijue", so mtu akiweka password, maana yake anajali hisia zako!
 
So nia ya madhumuni ya wanandoa kuweka password ni kwamba anampenda sana mwenziwake? au ana msaliti mpenzi wake?

Kwenye ndoa kuna mengi, co mstari mnyoofu kama baadhi wanavyoweza kufikiri. Kuna kuchokana na kuchukiana kwenye ndoa. Watu wakichokana wanadiriki kuleta hawala hadi ndani ya nyumba wanayoishi na wanandoa wenzao. Point yangu ni kwamba ukiona password ujue mapenzi yamepungua-ila bado anamjali na kumheshimu mpenzi wake (ndo maana nikatumia neno 'care' na sio 'luv'). Kama mtu anadhani mambo kwenye ndoa ni mstari, asithubutu kuoa. Usiguse simu ya mwenzio, utaishi kwa amani-la sivyo, atanenepa yy ww utakonda!
 
Kwa hiyo hapo tumekubaliana wote kuwa PW ina uhusiano na cheating. Maana wengine wanapotezea main issue ambayo ni cheating. What is left is care but love is with someone else?

Na ndoa bila upendo si ndoa. If it is care I can be cared even more with my parents and relatives or I can take good care of myself if am financially sound! Sijaolewa/oa kufata care but love

Ndio maana hata mke wa Tiger Woods aliomba divorce japo nina imani alikuwa anapata care zote

Kwenye ndoa kuna mengi, co mstari mnyoofu kama baadhi wanavyoweza kufikiri. Kuna kuchokana na kuchukiana kwenye ndoa. Watu wakichokana wanadiriki kuleta hawala hadi ndani ya nyumba wanayoishi na wanandoa wenzao. Point yangu ni kwamba ukiona password ujue mapenzi yamepungua-ila bado anamjali na kumheshimu mpenzi wake (ndo maana nikatumia neno 'care' na sio 'luv'). Kama mtu anadhani mambo kwenye ndoa ni mstari, asithubutu kuoa. Usiguse simu ya mwenzio, utaishi kwa amani-la sivyo, atanenepa yy ww utakonda!
 
yap! Kunaulazima ilimrad kila mmoja atakuwa anamuheshimu i mean anamuamin mwenzie kwan simu kuwa na password kunatatzo gan? Haina shda anaweza kutoweka password na bado akawa ANAMULIKA MWIZI WA MAPENZ so chamsing ni kuheshimiana na kuhaminiana full-stop
Unaweka password ili iweje???
 
Yah!password ni muhimu kwa kulinda any kind of intruder,na wengi tunaweka confidential info kwenye simu. Mpenzi wangu anayo simu yake sasa yangu anatafuta nn?mie ni mdau wa mapassword kwenye simu tena strong password,kama hataki achape rapa
 
Kama mke wako huwezi kushare password yako ya ATM naye ujue hapo hamuishi kama mke na mme. Kama hamuwezi kushare simu zenu na content zake kuna tatizo.

Wapenzi wengi hasa wanapoanza mapenzi wakati wa uchumba, simu ni kitu cha kawaida na wanashare. Girlfriend wako au boyfriend wako akitaka kufanya kitu wakati mwingi hukupa simu umshikie. Sasa mkishaingia kwenye ndoa, miaka mitatu hadi mitano, simu inatiwa kufuli ya password.

Hapo hakuna maelezo mengine zaidi ya kuwa CHEATING is going on. Na ukishajua cheating is going on, asikudanganye mtu, kama huyo mke au mme unampenda, maisha hayataenda mpaka hiyo cheating isimame. Hakuna mbadala eti, sifatilii simu ya mke wangu/mme wangu wakati najua kabisa kuna tatizo! Matatizo yatajitokeza in another form, hakuna njia na tusidanganyane! Hakuna anayeweza kuishi na mke/mme kwa amani wakati anajua kuna cheating going on!
 
Hapo hapo je unaweza mwonyesha mke wako pw ya ATM?
Yap why not akiwa na shida na hela nitampa ATM kadi yangu including the password akachukue hela unless otherwise if unam-speculate mkeo utakuwa na wasiwasi kumpa password ya ATM yako.
 
Jamani kuna umuhimu wowote simu za wapenzi wawili kuwana na password? let say mke na mme au mtu na mchumba wake wanaulazimu wa kuweka password?

Password ni muhimu sana, labda kama ulikuwa mlokole au ustadhi au mtakatifu gani sijui toka siku ya kuzaliwa! si unajua wale wa zamani wanaweza kutafuta namba yako wakaanza kutuma msj za ajabu halafu zikafika kwenye mikono ya jamaa. Vilevile tuna wachumba zetu wa utani utani bora uwe na password kuepusha shari
 
Kwa hiyo hapo tumekubaliana wote kuwa PW ina uhusiano na cheating. Maana wengine wanapotezea main issue ambayo ni cheating. What is left is care but love is with someone else?

Na ndoa bila upendo si ndoa. If it is care I can be cared even more with my parents and relatives or I can take good care of myself if am financially sound! Sijaolewa/oa kufata care but love

Ndio maana hata mke wa Tiger Woods aliomba divorce japo nina imani alikuwa anapata care zote

Password ipo kwa ajili ya privacy. Privacy ni muhimu hata kwa wanandoa. Ndugu, uwe unasoma au unafanya kazi, kuna watu ambao una urafiki nao wa karibu sana kiasi cha kutaniana na kutumiana msg ambazo mtu mwingine anaweza ku-interpret vibaya. Yaani hamna na hamtarajii kuwa na uhusiano wa kimapenzi, ni urafiki tu. Sasa ili kuepusha mjadala usio na tija na mwenzio, unatumia PW. Vip simu ikiibiwa, unataka mtu aweze ku-access info nyeti kama account namba, PIN na hata message zako? Basi tuende mbele zaidi, tuwe tunafuatana maofisini na sokoni ili kujua kama kuna 'wadoezi' wa penzi letu!!??
 
Kama mke wako huwezi kushare password yako ya ATM naye ujue hapo hamuishi kama mke na mme. Kama hamuwezi kushare simu zenu na content zake kuna tatizo.

Wapenzi wengi hasa wanapoanza mapenzi wakati wa uchumba, simu ni kitu cha kawaida na wanashare. Girlfriend wako au boyfriend wako akitaka kufanya kitu wakati mwingi hukupa simu umshikie. Sasa mkishaingia kwenye ndoa, miaka mitatu hadi mitano, simu inatiwa kufuli ya password.

Hapo hakuna maelezo mengine zaidi ya kuwa CHEATING is going on. Na ukishajua cheating is going on, asikudanganye mtu, kama huyo mke au mme unampenda, maisha hayataenda mpaka hiyo cheating isimame. Hakuna mbadala eti, sifatilii simu ya mke wangu/mme wangu wakati najua kabisa kuna tatizo! Matatizo yatajitokeza in another form, hakuna njia na tusidanganyane! Hakuna anayeweza kuishi na mke/mme kwa amani wakati anajua kuna cheating going on!

Umenena mkuu wadau mpooooo naona jamaa kasisitiza kwamba PW ni ubatili...i mean kwamba ni CHEATING TU na hakuna cha ziada!!! mhh very interesting!!
 
Password ipo kwa ajili ya privacy. Privacy ni muhimu hata kwa wanandoa. Ndugu, uwe unasoma au unafanya kazi, kuna watu ambao una urafiki nao wa karibu sana kiasi cha kutaniana na kutumiana msg ambazo mtu mwingine anaweza ku-interpret vibaya. Yaani hamna na hamtarajii kuwa na uhusiano wa kimapenzi, ni urafiki tu. Sasa ili kuepusha mjadala usio na tija na mwenzio, unatumia PW. Vip simu ikiibiwa, unataka mtu aweze ku-access info nyeti kama account namba, PIN na hata message zako? Basi tuende mbele zaidi, tuwe tunafuatana maofisini na sokoni ili kujua kama kuna 'wadoezi' wa penzi letu!!??

Siamini kwamba PW kwenye simu inaweza mzuia mtu ku access information zako ..... kwa watu wa IT hiyo ni kazi ya sekunde moja tu na kila kitu kipo nje. Sina ushaidi na hili isipokuwa nilielezwa na one of IT guy.
 
Back
Top Bottom