Uwajibikaji wa Viongozi wakati wa Maafa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
article-0-0D98D8C300000578-714_964x577.jpg
article-2030720-0D99B5CC00000578-983_964x615.jpg
article-2030720-0D98BBD000000578-278_964x888.jpg

Rais Barrack Obama wa Marekani amekatisha likizo yake mara moja na kwenda kujumuika na kituo cha kuchunguza mwenendo wa kimbunga Irene na kuratibu mambo mbalimbali ikiwepo kuokoa maisha ya waadhirika na huduma mbalimbali.

Viongozi wetu wanapaswa kujifunza kutoka kwa hawa wenzetu, maana kwetu utashangaa janga zito kitaifa au kiutawala linatokea utaona kiongozi ndio anadandia ndege kwenda nchi za nje, na matokea yake viongozi waandamizi kila mmoja anafanya na kutoa kauli yake kama anavyoona na kufikiria kwa sababu rubani wa nchi haoni uzito wake na cruel wake wanabaki kwa mtindo wa paka akitoka panya anatawala.

Bahari ya Atlantic si shwari, ni bahari yenya hatari nyingi kuliko bahari nyingine zote katika dunia yetu, na nibahari yenye kina kirefu kuliko hata Pasific ambayo ni kubwa zaidi. Hata usafiri wa angani ndege na usafiri wa meli si huru kukatisha bahari hii ila kuna maeneo maalum yaliyoratibiwa kuwa salama kukatisha. Kama triangle circle karibu na visiwa vya Bermuda baada ya meli nyingi na ndege nyingi kuangamia ni eneo ambao vyombo vya majini havithubutu kutia pua. Afrika wangesema kuna majini.

Chimbuko la vimbunga linaloikumba Marekani si Marekani kwenye ila ni sehemu ya visiwa vya Kerubiani na kuna vimbunga vyenye mianzo tofauti kuendana pia na mieleko yake inakoishia. Kwa maana hiyo wataalamu wamevipa majito kutokana na utaratibu huo wa vianzio na mwelekeo wa vimbunga hivyo.

Bahati nzuri wenzetu wana vyombo vya uhakika na wataalamu wa hali ya hewa waliobobea, maandalizi ya kimbunga hiki cha Irene yalianza wiki mbili zilizopita na kujua ni upande gani kitaelekea baada ya kuzuka huko baharini Atlantic karibu na visiwa vya Sichelesis na Kerubian. Tofauti na kwetu hujui nini kitatokea zaidi ya kusoma ishara za wingu jeuzi na zito.
 
...........................Huu ni mfano mzuri kwa viongozi wetu,kikwete tulikuwa na maafa ya Gongo la mboto yeye akawa anarandaranda tu nchi za nje,juzi nchi imekumbwa na mgao wa kutisha na bado unaendelea yeye anapaa tu.
 
...........................Huu ni mfano mzuri kwa viongozi wetu,kikwete tulikuwa na maafa ya Gongo la mboto yeye akawa anarandaranda tu nchi za nje,juzi nchi imekumbwa na mgao wa kutisha na bado unaendelea yeye anapaa tu.

Uwajibikaji wa viongozi wetu ni tatizo kwani wamejenga thana ya kwamba wamewateua waandamizi wao na hivyo wanawajibika kwa kila kitu yeye ni kutalii, kufungua na kufunga makongamano na kukate tepe.
 
Ustaarabu ni kitu cha muhimu sana. Mtu aliyestaarabika anaogopa aibu, tatizo la linatokea eneo lake la kaz linamgusa. Huku kwetu ustaarabu bado, hatuogop aibu. Viongoz hawajastaarabka, watajfunza nin?
 
hawewezi kujifunza ndio maana Nghilly (mgombea ubunge TMK) alitushauri tumfunze huyu mk we re! Utamaduni huu uko kila mahali kwa wenzetu Uk juzi kwenye fujo mayor na PM walikatiza likizo zao na kurudi kushughulikia matatizo ya kwao, Obama pia nae amefanya hivyo. Kwetu Ilizama MV Bk Sumaye akaenda zake South Africa, Mkw er e nae aranda randa huku na huko wakati watu wanakaa gizani siku 5, mabomu yanalipuka na kuua raia wasiona hatia. Hawana uwajibikaji ni lazima ifike mahali nguvu ya watu iamue mustakabali wa nchi hii
 
Ustaarabu ni kitu cha muhimu sana. Mtu aliyestaarabika anaogopa aibu, tatizo la linatokea eneo lake la kaz linamgusa. Huku kwetu ustaarabu bado, hatuogop aibu. Viongoz hawajastaarabka, watajfunza nin?

Wakati wa kuomba kura wanagaragara mavumbini na kuwa karibu na walemavu, wakishapata kura hao huwaoni tena ni angani tukisha kuishia kwenye mahoteli ya kitalii nchi za nje wakti sisi tunahangaika na gizo la Ngeleja.
 
Wakati wa kuomba kura wanagaragara mavumbini na kuwa karibu na walemavu, wakishapata kura hao huwaoni tena ni angani tukisha kuishia kwenye mahoteli ya kitalii nchi za nje wakti sisi tunahangaika na gizo la Ngeleja.
<br />
<br />
ustaarabu sio asili yao ndio maana wanashndwa ku maintain. Huwa viongoz wetu wakat wa kampen wana pretend ustaarab, sis wananch hatuna muda wa kuwachunguza.
 
Ninachochangaa hii tabia ya viongozi watu imetoka wapi? Maana enzi za mababu zetu hata machifu walikuwa mstari wa mbele katika kupigania wananchi kama akina Mkwawa kuwa vitani na kuwindwa na jeshi la Wajerumani ni kielelezo tosha. Hata watoto wa Malkia wa Uingereza pamoja na maisha ya ufahari wajukuu wake wapo ndani ya kombati za jeshi. Sisi tunajivunia nini na starehe za mahotelini?
 
Back
Top Bottom