uvumilivu...

my bro hivi inamaana wewe unataka ukutane na malaika? una yaweka wapi mapungufu ya kibinadamu?
hapana sio malaika. mimi kama binadamu wote nina mapungufu kadhaa lakini ni wajibu wangu kutoyatumia kujustify manyanyaso kwa mpenzi wangu, mf. naweza kunywa bia kiasi (< 4/day) lakini nikilewa na kufanya vituko na mambo ya aibu kila siku/wiki je utaweza kuvumilia kwa miaka mingi. hii ndio ninachomaanisha. binafsi naweza kuvumilia infidelity once or twice (with counselling), lakini ukicheat mara kwa mara au kuleta utitiri wa wanaume itabidi niondoke maana hapo sio fair to me
 
nivea no matter ni repetitive kiasi gani wewe unapaswa kujua unalichukuliaje hilo? kwamfano hakunaga silaha nzuri kwa kosa ambalo ni repetitive kama kulipuuzia kisha kukaa kimya hii ni aina ya uvumilivu ambayo sikuzote humfanya mtu kuwa mnyenyekevu na mwenye heshima kwa mwenzi wake, na ni nzuri sana inapotumiwa na mama pasi kusahau maombi kwa Mungu.
gfsonwin hapao kwenye red sio makosa yote unaweza kukaa kimya nakupotezea mfano. nimume wako wandoa takatifu,kazaa nje mara ya 1ukavumilia,mara ya pili ukamkanya nakuangalia tatizo tuseme ukawashirikisha wanaohusika bado akaendelea na tabia hiyo hiyo,hakujirekebisha ,hao inajidhihirisha wazi kuwa anatembea nje ya ndoa bila kinga hiyo ni hatari ,je haitakulazimu kumwambia nahamia chumba cha pili????????????????UVUMILIVU UNATEGEMEA NA NDOA /MAHUSIANO NA MATATIZO YANAYOVUMILIKA!
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,hongera kwa mtazamo wako chanya na mahusiano,ila,utapata tabu sana kueleweka hasa kwa mabinti wa miaka 21-30.Lakini pia kwa faida ya wengine na uhalisia ni kwamba,ni jambo gumu sana pengine kuliko ugumu wenyewe watu kuelewa maisha na matukio yake na yanayoyafanya haya tuyafanyayo kama mtu hatajihangaisha kujua upendo ni nini?Ukijua upendo umejua yote!
Eiyer nilichogundua mdogo wangu ni kwamba somo ni gumu sana kivitendo ila najiuliza hivi mbona wengine wanaweza kwanini wengine washindwe?mmh.............namshukuru sana Mungu kuzaliwa kijijini na kukulia kijijini pengine ndio maana niko hivi hofu ni kwa wanangu waliozaliwa mjini kila kitu ni dihybrid progeny.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin hapao kwenye red sio makosa yote unaweza kukaa kimya nakupotezea mfano. nimume wako wandoa takatifu,kazaa nje mara ya 1ukavumilia,mara ya pili ukamkanya nakuangalia tatizo tuseme ukawashirikisha wanaohusika bado akaendelea na tabia hiyo hiyo,hakujirekebisha ,hao inajidhihirisha wazi kuwa anatembea nje ya ndoa bila kinga hiyo ni hatari ,je haitakulazimu kumwambia nahamia chumba cha pili????????????????UVUMILIVU UNATEGEMEA NA NDOA /MAHUSIANO NA MATATIZO YANAYOVUMILIKA!
nivea nafikir mimi nilivyokuzwa na kuish ni tofauti sana, manake mimi huwa naangalia amani ya nafsi yangu zaid kuliko kuangalia magonjwa na vingine. sina maana kwamba nina underestimate madhara ya magonjwa hapana bali ninaangalia kwanini amani yangu iondolewe na mtu?

hivi ni nani aliyekwambia kuwa kosa la mume ama mke kuzaa nje ndio kosa kubwa sana lisilovumilika ukilinganisha na makosa mengine? Jamani sijui nikoje mimi na hasa mental equip yangu labda ni kwasababu ya niliyoyapitia ndo maana. Yapo makosa ambayo kweli siwez kuyavumilia na kwanu ni kosa moja tu la kunitishia ama kuhisi tu at anypoint huyu atanitoa uhai. hilo tu mengine yote navumilia manake najua nitapita.
 
Last edited by a moderator:
Ni somo zuri lakini tatizo letu ni wepesi wa kusahau.
Mambo yanapokuwa ndivyo sivyo huwa tunasahau haraka sana hili somo la uvumilivu.
 
nivea nafikir mimi nilivyokuzwa na kuish ni tofauti sana, manake mimi huwa naangalia amani ya nafsi yangu zaid kuliko kuangalia magonjwa na vingine. sina maana kwamba nina underestimate madhara ya magonjwa hapana bali ninaangalia kwanini amani yangu iondolewe na mtu?

hivi ni nani aliyekwambia kuwa kosa la mume ama mke kuzaa nje ndio kosa kubwa sana lisilovumilika ukilinganisha na makosa mengine? Jamani sijui nikoje mimi na hasa mental equip yangu labda ni kwasababu ya niliyoyapitia ndo maana. Yapo makosa ambayo kweli siwez kuyavumilia na kwanu ni kosa moja tu la kunitishia ama kuhisi tu at anypoint huyu atanitoa uhai. hilo tu mengine yote navumilia manake najua nitapita.
gfsonwin HEBU YAANGALIE NAYALE KUMI NILIYOYAKUMBUKA UNIAMBIE PIA ,KUZAA NJE YA NDOA NI KOSA KUBWA LA KUKOSA UAMINIFI NA NIKINYUME NA VIAPO VYA KANISANI/MISIKITINI SIO SWALA DOGOKAMA UNAVYODHANI KABLA YA NDOA SITILII MAANANI LAKINI BAADA YA DU NI KOSA TUSIPINGANE NA UKWELIWALA TUSIFUNIKE DHAMBI NA PAZIA HII INA MADHARA ILA INATEGEMEA NA UNAVYOYACHUKULIA MAMBO.ASANTE gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin,hongera kwa mtazamo wako chanya na mahusiano,ila,utapata tabu sana kueleweka hasa kwa mabinti wa miaka 21-30.Lakini pia kwa faida ya wengine na uhalisia ni kwamba,ni jambo gumu sana pengine kuliko ugumu wenyewe watu kuelewa maisha na matukio yake na yanayoyafanya haya tuyafanyayo kama mtu hatajihangaisha kujua upendo ni nini?Ukijua upendo umejua yote!
kuelewa somo nacho ni kipaji..........tatizo hatukai na wazazi wetu kutuelewesha zaidi juu ya ndoa.............na uvumilivu kwenye ndoa ukoje.

tunakaa na mashost na sometimes tunatiana ujinga mwisho wa siku ndoa inavunjika.............mimi nina mama yangu mkubwa nikikuelezea story ya huyo mama yangu wasichana wengi wa sasa hivi wasingeweza kuvumilia yale aliyovumilia mama yangu huyo na wakadumu kwenye ndoa mpaka kifo kilivyowatenganisha ( mume kufariki ).
 
MJ1 nafikir kama waliopita kwenye swala la ndoa naamini nami nilipita tena nimejifunza sana. Leo hii kila mtu ana heshima na swala la kuvumiliana tena halipo manake makosa yaliyobaki ni ya kawaida sana ambayo hayasumbui.

Nimelitambua hilo from post yako ya kwanza mamito and I salute you for that. What I meant kwa ....anapaswa kulielewa hilo. nilikuwa nacoment post ya King'asti juu ya kumweleza mwenzi yale ambayo huyapendi ndio nikacomment kuwa tena huyo mwenza aelewe from the word go.
 
gfsonwin umenikumbusha kisa cha ndugu yangu mwaka 2010 mumewe alimletea watoto 2 amezaa na mwanamke mwingie masikini mdada alichanganyikiwa lakini mwisho wa siku akakubaliana na hali akaamua kuwalea watoto cha kushangaza mwaka huu mwanzoni mwanamke mwingine akamletea fujo nyumbani kwake huku akiwa na mtoto akidai wa mumewe......mdada amesema amevumilia sasa amechoka.........kuna mambo mengine unaweza kujifunza kuvumilia na kuna mengine yanashindakan au kufika kikomo na itakuwa sio kuvumilia tena bali kujiumiza.......
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin HEBU YAANGALIE NAYALE KUMI NILIYOYAKUMBUKA UNIAMBIE PIA ,KUZAA NJE YA NDOA NI KOSA KUBWA LA KUKOSA UAMINIFI NA NIKINYUME NA VIAPO VYA KANISANI/MISIKITINI SIO SWALA DOGOKAMA UNAVYODHANI KABLA YA NDOA SITILII MAANANI LAKINI BAADA YA DU NI KOSA TUSIPINGANE NA UKWELIWALA TUSIFUNIKE DHAMBI NA PAZIA HII INA MADHARA ILA INATEGEMEA NA UNAVYOYACHUKULIA MAMBO.ASANTE gfsonwin
nivea ni kosa sawa na ni dhambi kwani ni uzinifu, lakini pia tunapaswa kuangalia impact yake in future, unajua sifuniki dhambi manake hadi umetumia caps inamaana umeonyesha msisitizo.

sasa kuna wakati mwanaume ni bora akazaa nje kuliko kukuletea mwanamke ndani mwako akakulaza chumbani na watoto yeye nahawara wakalala chumbani na asubuhi ukaachiwa chumba usafishe. ila bana katika jambo kama hili mvumilivu hupita kwa furaha nimeshuhudia haya jamani.
 
Last edited by a moderator:
Huu uvumilivu tunaoujadili hapa dada gfsonwin unaweza ukawa supported na ile dhana yetu ya pata raha ndani ya matatizo au?
 
......naweza kuvumilia yanayovumilika, yasovumilika nayakemea mara ya kwanza na ya pili, ya tatu nakaa kimya...yakiendelea najiondoa taratibu.

Yasovumilika kwangu sio lazima yafanane nawe. Mfano; Naweza vumilia Confession ya 'cheating' nikashindwa vumilia kudanganywa...:cool:
 
nivea ni kosa sawa na ni dhambi kwani ni uzinifu, lakini pia tunapaswa kuangalia impact yake in future, unajua sifuniki dhambi manake hadi umetumia caps inamaana umeonyesha msisitizo.

Sasa kuna wakati mwanaume ni bora akazaa nje kuliko kukuletea mwanamke ndani mwako akakulaza chumbani na watoto yeye nahawara wakalala chumbani na asubuhi ukaachiwa chumba usafishe. Ila bana katika jambo kama hili mvumilivu hupita kwa furaha nimeshuhudia haya jamani.
nimefika mwisho wa akili zangu nimemwachia mungu maisha na ndoa yangu ailinde mimi siwezi na anailinda kweli kweli ,things are sometimes inevitable only god can,thats why i love him
 
sasa kuna wakati mwanaume ni bora akazaa nje kuliko kukuletea mwanamke ndani mwako akakulaza chumbani na watoto yeye nahawara wakalala chumbani na asubuhi ukaachiwa chumba usafishe. ila bana katika jambo kama hili mvumilivu hupita kwa furaha nimeshuhudia haya jamani.
kha!! gfsonwin hiyo ni ndoa ya kweli au hadithi? yaani kakudharau mpaka kukuletea mwanamke mwingine. hakuna cha kuvumilia hapo ni kuondoka tuu.
 
Last edited by a moderator:
kuelewa somo nacho ni kipaji..........tatizo hatukai na wazazi wetu kutuelewesha zaidi juu ya ndoa.............na uvumilivu kwenye ndoa ukoje.

tunakaa na mashost na sometimes tunatiana ujinga mwisho wa siku ndoa inavunjika.............mimi nina mama yangu mkubwa nikikuelezea story ya huyo mama yangu wasichana wengi wa sasa hivi wasingeweza kuvumilia yale aliyovumilia mama yangu huyo na wakadumu kwenye ndoa mpaka kifo kilivyowatenganisha ( mume kufariki ).

my dearest sister sasa huyo mama mdogo watu watasema alikuwa mjinga labda ama hana kazi ama elimu etc. mimi naomba nikupe ushuhuda kidogo tu wa kwangu binafsi na nisemapo nimepita namaanisha.

mume waliwah kununua gari zuri sana sikuwa kulipanda zaid ya kimada aitwae ANA. nakumbuka enzi hizo nikienda salun sinza anakuja na pikipiki ya mume wangu ananitukana matusi ya nguoni na kunidoboleshea wanayofanya na mr ndani ya gari. sikuwah kumjibu hata siku moja wala kulia nillisema silii.

haikuishia hapo nyumba tuliyojenga alijua atahamia yeye akaja kunipa mchambo mtakatifu nikiwa nasuka nywele saluni moja mitaa ya sinza, kurudi home mr ukimweleza anakwambia kabisa wewe kwanini ulienda kusuka huo si unamfuta mwenyewe, ngoja akuumize. hapo napo nilivumilia.

kibaya zaid nilichukulia kama changamoto sikushtaki kwa nani wala nani na niliua hisia za hasira manake natoka kabila moja hivi so sikupende watu wachukulie kama sababu, wala sikumchukulia Rb. nikiwa navumilia bado mr alisafiri aliporudi alishukia kwake na zawadi zote za ulaya nakumbuka sitasahau. na baada ya siku kama 5 ndipo wanakuja wote home usiku nikamkaribisha. waliingia wote ndani hadi kwa rum, sikufichi walilala nikalala na watoto.

asbh wanaamka wanakuta hadi chai na supu iko mezani, walihisi nimetia sumu but niliwahakikishia kwa kula pamoja nao na watoto na nikafuta meza nkawaualiza mchana watakula nini. mtoto wa mume wangu ndiye aliyeuliza baba huyu ni nani? yule mwanamke aliapotaka kujibu tu ikawa kama mume wangu kaumizwa akamwambia tena kwa ukali wewe kahaba toka ndani mwangu. Nilishtuka kama naimepigwa shoti ya umeme. Mr alikasirika sana akataka kumpiga lakini nilimtetea yule mwanamke ili asije akaumizwa. mimi na wanangu tulilia sana.
yule ANA alitolewa ndani kama mwizi kwa mateke akiwa amejifunga kitenge changu kiunoni. na hapo bado mume wangu alikuwa na mtoto wa mashtuzi ambaye nilimkuta na niko nae hadi leo.

mume wangu alishangaa sana moyo wangu jinsi ulivyo, uvumilivu na upendo wangu kwake ulimbadilisha ndio maana nimwambiapo King'asti kuwa uvumilivu humbadilisha hata shetani kuwa malaika ni kweli nimeshuhudia. leo hii nina miaka zaid ya 10 na naifurahia ndoa. naamini hakuna binti ambaye anaweza kupita hapa ila mimi nilichoangalia ni nataka nini kwenye maisha yangu? na je kwanini nitaabishe amani yangu?

haikuwa kazi rahisi kuvumilia ila ni Mungu tu alinivusha sikuwah kushtaki hata siku moja kwa mama wala ndgu wa pande zote mbili wala kwa shosti zaid ya Mungu. niliia hadi mto ukalowa machozi nilisali hadi kung'ata sura za biblia nakumbuka zab 16&17. hadi leo hii hiyo biblia inaalama za meno ambazo nilizitia miaka kama 7 hivi iliyopita.

nihitimishe kwa kumtia mama mwenzangu moyo kuwa Mungu anaweza yote usimweleze mtu sema na Mungu. halafu omba amani uone yani muujiza hutokea punde.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom