Uvumi wa kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura Tunduma

imeandikwa na ikunda erick; tarehe: 22nd october 2010 @ 06:38
kauli ya mgombea urais wa tanzania kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), dk willibrod slaa, kwamba kuna makontena yameingizwa nchini yakiwa na karatasi za kura zilizokwishapigwa, ni ya uongo.

Akiwa singida oktoba 18, mgombea huyo alidai kuwapo taarifa hizo lakini alipobanwa na polisi, akashindwa kuthibitisha na badala yake akasema aliipata kupitia simu aliyopigiwa na katibu wake wa tunduma, mbeya.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchaguzi, rajab kiravu, makontena hayo yalifunguliwa na polisi mbele ya dk slaa na kubaini kuwa yalikuwa na vipodozi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana dar es salaam, kiravu alisema madai ya mgombea huyo ni ya uzushi, na yanayoleta taswira mbaya kwa wananchi.

Kiravu alisema oktoba 18, akiwa kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni singida, slaa alidai kukamatwa lori mji mdogo wa tunduma , likiwa na karatasi kutoka afrika kusini zenye kura za ndiyo kwa ajili ya ccm.

Alisema taarifa hiyo ilifanyiwa uchunguzi na vyombo vya usalama ambapo polisi, wahusika wengine akiwamo mgombea huyo walifanya upekuzi kubaini ukweli wa madai hayo na kubaini kuwa ni uzushi.

"gari hilo lilipekuliwa na polisi, wahusika wengine, akiwamo mlalamikaji, dk. Slaa, na hakuna karatasi zilizokutwa, bali gari hilo lilikuwa na vipodozi," alisema kiravu.

Alisema kwa kipindi kirefu, nec imejizuia kutoa kauli zinazoleta ubishani na wagombea au vyama, ila kwa uzito wa kauli ya uzushi ya dk. Slaa, tume inawaomba wananchi wapuuze uzushi huo.

"mkuu wa majeshi nchini alishazungumzia hili na kukanusha uzushi huo, ila kwa kuwa dk. Slaa alitaka tume itoe kauli kuhusu suala hilo, nec inasema imesikitishwa na kauli hiyo ya uzushi yenye taswira mbaya kwa wananchi," alisema kiravu.

Alisema dk slaa alipoulizwa alikopata taarifa hizo za uzushi wa karatasi za kura, akajibu kwamba alipigiwa simu na katibu mtendaji wa tunduma.

"sisi hatuna kingine cha kusema kuhusu uzushi wa dk. Slaa, bali tunawaambia wananchi waupuuze… na mtu mzima ukiambiwa mwongo inatosha," alisema kiravu.

Aliviomba vyama vya siasa na wagombea kuheshimu na kuzingatia sheria ili kuepusha uchochezi na vurugu kabla na baada ya uchaguzi.

"kabla ya kutoa kauli ni vyema wagombea au vyama wakazipima kuona uzito na ukweli wake, tusiwapotoshe wananchi kwa uvumi, ni hatari," alisisitiza kiravu.

Katika hatua nyingine, kiravu alisema mwongozo wa maadili ya uchaguzi mwaka 2010, uliosainiwa na vyama na wagombea wote wanaoshiriki kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, hautekelezwi kwa dhati.

Alisema katika mwongozo huo sehemu ya pili kipengele 2.1 (a), kinatoa maelekezo kwa vyana vya siasa na wagombea wake, ambapo kinawataka kuhakikisha wanahamasisha na kuwasisitiza wanachama na wafuasi wao wasifanye fujo.

Kiravu alisema kwa kipengele hicho na vingine, hakuna hatua za dhati zinazofanywa na vyama hivyo na badala yake wanatupiana lawama.

Aidha, alisema baadhi ya dini na viongozi wao wamekuwa wakiingiza siasa katika dini na wakati mwingine kuwaonesha waumini wao kuchagua kwa misingi ya dini.

Akirejea kwenye maadili ya uchaguzi, kiravu alisema sehemu ya 2.2(j) inakataza vyama vya siasa au wagombea kuomba kupigiwa kura kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia au rangi.

"suala la udini halitatusaidia, sisi sote ni watanzania, tulishakubaliana hatuna udini wala rangi, sasa tusiwavuruge wananchi," aliongeza kiravu.

wandishi gani walikuwepo? Tunaomba picha za slaa akichungulia makasha!
 
Karatasi za Jk zilitengenezwa nchini Afrika Kusini, lori lililobeba mzigo lilipita Botswana, Zimbabwe hadi Zambia.

Kufika mpakani mwa Zambia na Tanzania, mwenye lori alijua madhara makubwa atakayopata akivuka mpaka na kuingia Tanzania, hivyo aliuza mzigo kwa lori tupu lililotoka Zambia likiwa njiani kuingia Tanzania.

Vijana wa UWT na CCM walipewa namba za lori ambalo lilibeba karatasi toka SA na walikuwa Tunduma wakilisubiri, bila ya kupewa taarifa kuwa mzigo tayari ulikuwa ndani ya gari lingine.

Taarifa za kupatikana kwa karatasi ndani ya lori lingine, zilimshitua sana mkuu wa polisi wa mkoa wa Mbeya, na ndiyo sababu aliitisha kikao cha haraka cha usalama cha mkoa kupata maelezo kutoka kwa vijana wake waliokuwa mpakani kuupokea mzigo kutoka SA.

Inashangaza tukio la hatari linatokea mpakani, badala ya kuelekea kwanza kwenye lori na kuchunguza na kupata ukweli wa kuwepo kwa hizo karatasi, wanakimbilia kwenye vikao?

Ndani ya kikao walihojiwa wahusika, kuhusiana na tukio hilo, pili waliaandaa taarifa ya pamoja jinsi ya kujibu na kuzima hoja zozote zitakazoibuliwa na wananchi.
 
Asante;

Nafikiri ungeipost kama new thread!!!

Yale mambo ya EPA nk yalianza hivi hivi..nakila mtu alisema uzushi, wongo , nitakwnenda mahakamani...and everybody knows what came after!!
 
Back
Top Bottom