Uvivu na utapia-akili wa wabunge wa CCM...

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,234
531
Usingizi wa pono, utapia-akili, ufinyu wa fikra na kutokuweka mbele maslahi ya taifa wa "wabunge" walio wengi wa CCM umenisukuma kunukuu Taarifa ya Pili ya Tume ya Jaji Nyalali ya mwaka 1992; uk. wa 2, para 5:

Juhudi zilizofanywa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu J.K. Nyerere kati ya mwaka 1986 na mwaka 1987 za kufufua Chama Cha Mapinduzi, zilidhihirisha kwamba Chama kilikuwa kimejisahau. Kampeni hii ilionesha wazi kwamba viongozi hawakuwa karibu na wananchi na kwamba Chama kilishindwa kudhibiti viongozi wabadhirifu na kuzuia tabia mbaya ya baadhi ya viongozi ya kunyanyasa wananchi.

Kwa kutumia matukio ya leo tu Bungeni kwenye muswada wa BRELA na majibu ya hovyo kabisa ya wiki hii kutoka kwa Waziri wa Fedha na AG kweli CCM ni sikio la kufa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom