UVCCM wataka mafisadi wafukuzwe uanachama

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Geofrey Nyangóro

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), Martine Shigela amepokea mapendekezo ya vijana wa Tawi la Matangini, Kimara jijini Dar es Salaam kwamba wtuhumiwa kwa ufisadi akiwamo waliokuwa mawaziri na wabunge wa sasa, kufukuzwa uanachama ili kurejesha imani ya chama hicho kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kusomewa risala hiyo Shigela alisema anaungana na vijana hao kwa asilimia mia moja na kwamba viongozi wasio na maadili ni mafisadi na mwisho wao umekaribia.

Shigela alisema chama hicho hivi sasa kina mafisadi na wamekuwa wakikiuka maadili kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa na kwamba kinachofanyika sasa ni kuangalia namna ya kukisafisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini.

Kuhusu maandamano ya Chadema alisema umoja huo haupaswi kukaa kimya na wao wana haki ya kuandaa maandamano kupinga Chadema isifanye maandamano kushinikiza uchaguzi wa Meya Arusha, urudiwe.

Awali akisoma taarifa hiyo yenye kurasa 11 katika mkutano wa tawi, uliofanyika juzi Kimara Matangini, Katibu wa UV-CCM wa tawi hilo Asenga Abubakar alisema vigogo hao wamechangia kuiweka CCM katika hali mbaya kutokana na tuhuma za ufisadi.

"Kama tunakipenda chama, lazima tuseme ukweli na chama kijivue gamba kama alivyosema Mwenyekiti Rais wetu Dk Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kusherehekea miaka 34 ya CCM.

"Tunashauri uchunguzi wa kina ufanyike katika ushiriki wao katika mikataba ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, Dowans, mkataba wa madini wa Buzwagi, ununuzi wa Rada na Ndege ya rais kwani ni aibu kubwa kwa baadhi ya watu hawa kuendelea kuwa wajumbe wa kamati kuu na ile ya maadili, achilia mbali uanachama wa CCM,"alisema.

Vijana hao walishauri chama kuunda kitengo cha uchunguzi juu ya mwenendo wa wanachama wao na vigogo na kusema kweli juu ya majibu na matatizo yanayoikabili CCM.

Alisema idadi ya watu wanaokichukia chama imezidi kuongozeka na hilo ni kutokana na wananchi kutoridhishwa na mambo yanayotokea katika uongozi wa juu wa chama hicho.

Kuhusu uongozi wa juu vijana hao waliwatupia lawama kuwa kitendo chao cha kubadili majina ya wagombea na kuwaacha wagombea wanaokubalika kwa wananchi ni chanzo cha wananchi kuichukia CCM.

Akizungumzia hali ya kisiasa Abubakari alisema ni mbaya na imevurugwa wakati wa kura za maoni.
 
Ni kweli inawezekana lakini mbona ni marafiki zetu sana? tena ni wamoja wa vikao vikubwa vya chama mtawatoaje?
 
Mimi sielewi hawa makatibu wa CCM na UVCCM upeo wao wa kufikiri na kutunza kumbukumbu ukoje.
Kila mara utasikia wanatoa kauli tata,mbaya zaidi nyingine zinapingana na zile walizotoa awali.
Hivi hawana msimamo?
 
unapotaja mafisadi unakuwa umemtaja hadi kikwete,..hawa vijana hawajipendi
 
Hizi toto ziko cheza na fire bana....Mbona wanapingana na baba yao ambae amewahi kusema hawa sio mafisadi kwa kuwa mahakama haijasema hivyo? Au wao tayari wamekuwa mahakama? Shigela ndo Chief Judge nini?

CHICHIEMU kwa kujigeuka bana, mpaka wanatia raha.....

Anyway, wakitaka wawatimue chamani waanze na yule anaewakumbatia na kuwafagilia kila kona kuwa wao ni watu safi kwa kuwa mahakama haijathibitisha kuwa wao ni majambazi...........I Think you know the man
 
Jinsi sinema hii inavyoendelea, nabashili kuwa sasa umekaribia muda wa kuanza kufukuzana kwenye chama chao!!
 
UVCCM waache unafiki, hawawezi kuwafukuza wala kuishinikiza CCM kuwafukuza mafisadi kwa kuwa wao wenyewe wamejaa na wanafadhiliwa na kusimamiwa na mafisadi:

1. M/Kiti wa bodi ya wadhamini wa UVCCM ni Edward Lowassa?mtanzania gani kwa sasa ana imani nae kama sio fisadi?

2. Kamanda wa UVCCM ni Kingunge Mwiru, mzee aliacha kuamini siasa za ujamaa na kuwa Fisadi mkuu (Bepari) nani asiyejua kampuni yake ilikuwa inachukua viingilio pale ubungo na kuipa manispaa kwa siku millioni lakini mara baada ya kupokonywa tenda manispaa yenyewe ikawa inakusanya zaidi ua million 5 kwa siku

3. Kamati kuu yenyewe ya chama imejaa mafisadi, mfano Rostam Azizi, Andrew Chenge ambaye ndio m/kiti wa kamati ya maadili ya chama

wawe wa kweli sasa wataanzia wapi kuwafukuza?Sitta alijaribu kuwachemsha akiwa spika walivyokwenda katika kikao cha halmashauri kuu wakata kumvua uanachama, hii si dhahiri kuwa wanwalinda mafisadi?inahitaji Degree kulitambua hilo?
 
Mimi sielewi hawa makatibu wa CCM na UVCCM upeo wao wa kufikiri na kutunza kumbukumbu ukoje.
Kila mara utasikia wanatoa kauli tata,mbaya zaidi nyingine zinapingana na zile walizotoa awali.
Hivi hawana msimamo?

huwezi kuwaelewa kaka! Wao wenyewe hawaelewani. Misimamo wanayosoma sio waliyojadiliana na kukubaliana bali ni yale waliyotumwa! Kwavile kila fisadi anawatu wake ndio maana misimamo haifanani. Badala wakae wajadiliane within the area ya maadili ya chama, wanakaa na kusoma yale waliyotumwa! Thats y chama kimekufa na sasa kila mtu anatafuta pakushika.
 
[/SIZE] Wakae wajadili matatizo ya maji huko kimara na matatizo ya matuta na foleni hapo kimara mwisho. Swala la anayejiita meya hapa Arusha watuachie wenyewe. Tumepigwa mabomu na risasi na ukiachilia mbali wenzetu waliofariki, kuna ndugu zetu wengi walipata ulemauu wa kudumu. Wanaishi kwa misaada na hii yote ni kwasababu ya ccm na uchu wao wa madaraka. Tunasubiri siku 21 ziishe Arusha ilipuke tena maana tumeamua hakuna kulala hadi kieleweke!
 
Najiuliza atae baki ni nani?..................anyway..............Waache watusafishie njia........
 
Geofrey Nyangóro

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), Martine Shigela amepokea mapendekezo ya vijana wa Tawi la Matangini, Kimara jijini Dar es Salaam kwamba wtuhumiwa kwa ufisadi akiwamo waliokuwa mawaziri na wabunge wa sasa, kufukuzwa uanachama ili kurejesha imani ya chama hicho kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kusomewa risala hiyo Shigela alisema anaungana na vijana hao kwa asilimia mia moja na kwamba viongozi wasio na maadili ni mafisadi na mwisho wao umekaribia.

Shigela alisema chama hicho hivi sasa kina mafisadi na wamekuwa wakikiuka maadili kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa na kwamba kinachofanyika sasa ni kuangalia namna ya kukisafisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini.

Kuhusu maandamano ya Chadema alisema umoja huo haupaswi kukaa kimya na wao wana haki ya kuandaa maandamano kupinga Chadema isifanye maandamano kushinikiza uchaguzi wa Meya Arusha, urudiwe.

Awali akisoma taarifa hiyo yenye kurasa 11 katika mkutano wa tawi, uliofanyika juzi Kimara Matangini, Katibu wa UV-CCM wa tawi hilo Asenga Abubakar alisema vigogo hao wamechangia kuiweka CCM katika hali mbaya kutokana na tuhuma za ufisadi.

"Kama tunakipenda chama, lazima tuseme ukweli na chama kijivue gamba kama alivyosema Mwenyekiti Rais wetu Dk Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kusherehekea miaka 34 ya CCM.

"Tunashauri uchunguzi wa kina ufanyike katika ushiriki wao katika mikataba ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, Dowans, mkataba wa madini wa Buzwagi, ununuzi wa Rada na Ndege ya rais kwani ni aibu kubwa kwa baadhi ya watu hawa kuendelea kuwa wajumbe wa kamati kuu na ile ya maadili, achilia mbali uanachama wa CCM,"alisema.

Vijana hao walishauri chama kuunda kitengo cha uchunguzi juu ya mwenendo wa wanachama wao na vigogo na kusema kweli juu ya majibu na matatizo yanayoikabili CCM.

Alisema idadi ya watu wanaokichukia chama imezidi kuongozeka na hilo ni kutokana na wananchi kutoridhishwa na mambo yanayotokea katika uongozi wa juu wa chama hicho.

Kuhusu uongozi wa juu vijana hao waliwatupia lawama kuwa kitendo chao cha kubadili majina ya wagombea na kuwaacha wagombea wanaokubalika kwa wananchi ni chanzo cha wananchi kuichukia CCM.

Akizungumzia hali ya kisiasa Abubakari alisema ni mbaya na imevurugwa wakati wa kura za maoni.

Kumbe nyie hamjaelewa.... kwao fisadi ni Mwakyembe,Sitta,Ole Sendeka na Mama Kilango soma hapo na umuangalie nyendo zake shigella ndo utajua analengawakina nani. El fin
 
Ah hao wenyewe wanasapoti mafisadi itakuaje wanataka mafisadi wafukuzwe uanachama ...hiyo ni kama wanajifurahisha..
 
sasa hapa kuna utata " wanaokosa maadili NI mafisadi" (according to Shigela) that means kuna watu wanaokosa maadili CCM then wannakuwa mafisadi! sio kwamba wamekuwa mafisadi then so wamekosa maadili!kazi ipo
 
Hizi toto ziko cheza na fire bana....Mbona wanapingana na baba yao ambae amewahi kusema hawa sio mafisadi kwa kuwa mahakama haijasema hivyo? Au wao tayari wamekuwa mahakama? Shigela ndo Chief Judge nini?

CHICHIEMU kwa kujigeuka bana, mpaka wanatia raha.....

Anyway, wakitaka wawatimue chamani waanze na yule anaewakumbatia na kuwafagilia kila kona kuwa wao ni watu safi kwa kuwa mahakama haijathibitisha kuwa wao ni majambazi...........I Think you know the man
Yes, I know him very well, he must be sucked
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom