UVCCM walitumwa kutoa tamko

Paulo

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
350
66
0712n.jpg

Wana JF naamini wengi wetu tulisoma lile tamko la vijana wa CCM kuwa wanataka mjadala wa Dowans urudishwe bungeni ili umma ujue mmliki wake ni nani. Swali likawa Je, nani kawatuma hawa vijana? Baada ya pekua pekua inaonekana kuwa Edward Lowassa ndiye aliyewatuma. Kwanini EL? Kwasababu EL ndiye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya UVCCM. Pili ndiye aliyekuwa anapiga debe Beno Malisa awe m/kiti hadi ikafikia stage pale mwanahalisi liliponanga kuwa mtoto wa Kikwete anataka kumhujumu babake likafungiwa. Pili EL amekuwa akipinga tangu mwanzo kuwa dowans si yakwake ila hakutaka kumsema. Tatu, hata Dr. Slaa mwenyewe hajawahi kumtaja EL kama ndo mmiliki wa dowans bali alimtaja yule bwana mkubwa. Nne, EL amekuwa akihudhuria matamasha mbalimbali kama njia ya kujirudisha kwenye jamii ili aweze kupita kilaini hapo 2015. Mfano hivi majuzi alihudhuria uzinduzi wa studio ya Mbasha, pia kabla yake alikua kwenye studio ya THT, na emekua akifanya fundraising ya makanisa. Pia hata kule arusha ambapo yeye ni mjume wa wadhamini wa CCM alionekana kutaka CDM na CCM wakae pamoja watatue tatizo la umeya. Pia amekua akiunga mkono katiba mpya na kusikika akisema watu wadai katiba kwa amani na upendo na tuepuke vurugu! Yaani amebadilika ghafla na sii bure yeye ndo emewatuma wale vijana waseme dowans irudishwe bungeni ili aweze kusafishwa. Ama wakuu mwaonaje kasi ya huyu jamaa?
 
Yani nikiiona hii sura na ya RA nahisi kutapika grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr:A S 20::A S 20::A S 20::A S 20::A S 20:
 
anaona hawezi kufa mwenyewe anataka either apewe mgao mkubwa wa malipo ya dowans kumzidi mkuu.AMEGOMEA GAWIO DOGO BCS YEYE ALIUMBUKA ZAIDI. NI NAMNA YA KUWATISHA WENZAKE ILI WAMPE MGAO MKUBWA. wakigoma atafanya lolote kwa kuwatumia uv-ccm ili KUWANASISHA WENZAKE MBELE YA UMMA.
 
tehe ... Marytina unasema mgao mdogo! Tena yeye ndo aliyekosa vingi kwasababu alikua PM. Ila jamaa anasauti sana ndani ya chama na hata Pinda mwenyewe huwa anamconsult mara kwa mara pale anapokwama.
 
Hili halina ubishi.. UVCCM walitumwa... na nani watajijua ila I believe walitumwa na mkubwa huko CCM. Hawana ubavu wa kukurupuka maana wamewekwa na haohao wakubwa..
 
Tehe..For us...Tanzanians we can't. Yes we can't I tell u. unlike Tunisians, Algerians, Egyptians, ....Yemen people who have got in the streets to demonstrate for changes, new hope, better pay .......the list goes on and on......
 
hiyo ni janja ya ccm, kuwaagiza wanachama waona jumuiya zao kutoa mawazo tofauti ili wawazubaishe wadanganyika aagh nimekosea watanzania kama kawaida yao na watanzanzania wawaone kumbe ni kweli wanatetea maslahi yao kumbe ni zuga
 
No sio janja ya CCM I tell u. Ni janja ya mtu mmoja ambaye ni kichwa sana ndani ya CCM anayeitwa EL. Ndo maana kesho yake Kamati kuu ilikaa na kutoa tamko tofauti. EL ni noma! He is the one who is screwing Tanzanians up!
 
Back
Top Bottom