UVCCM: Usalama wa taifa haumsaidii rais, unavuruga nchi kwa maslahi yake

Wewe ndio Salva Rweyemamu? hebu tuondolee kiwingu, huna uwezo na hautokuwa nao wa kutufundisha sisi tumuite kwa jina lipi Mkwere, kama inakukera nakushauri nenda kapoteze muda wako kwenye website ya ccm uangalie miradi ya chama, huko utakutana na taarifa ambazo unapenda kuzisikia, hapa umepotea njia, hatupo hapa kumpaka mafuta Mkwere wakati ndugu zetu wanakufa njaa kwa kukosa milo mitatu.

ndugu, huwezi jua na mimi naweza kuwa mwanachadema wala si CCM lakini tukubali kwanza kujikosoa kabla hatujakosoa wengine. Ni wachache sana wanaofanikiwa katika siasa kwa kukwepa hoja za msingi au kwamba matusi ndio hujenga. dhana hapa ni kuwa wapinzani tusionekane hatuna hoja au tunafafana na wale tunaowashambulia.
 
JE HAWA VIJANA WA UVCCM WAPO CCM KWA KUVUTIWA NA UTENDAJI WA CHAMA AU NDO WAPO KWA MATARAJIO YA KUTAWALA BAADA YA BABA ZAO MAFISADI KUTOKA!!!!???koz sidhani kama kijana mwenye akili timamu anaweza kusimama mbele ya vijana wenzake na kusema bila haya kuwa yeye ni CCM Pasipo na maslahi yake binafsi ila wajue kuwa siku zote ukweli hautakufa kama hawaamini wataona,,hivi sasa wanahisi DR SLAA NA CDM YAKE NDIO CHANZO ila hata wakifa mzimu wa watanzania wenye tabu na njaa na waliokata tamaa utazidi kuwafuata.
 
ndugu, huwezi jua na mimi naweza kuwa mwanachadema wala si CCM lakini tukubali kwanza kujikosoa kabla hatujakosoa wengine. Ni wachache sana wanaofanikiwa katika siasa kwa kukwepa hoja za msingi au kwamba matusi ndio hujenga. dhana hapa ni kuwa wapinzani tusionekane hatuna hoja au tunafafana na wale tunaowashambulia.

Kwanza mimi sio CHADEMA usinifungamanishe na chama ambacho mimi si mwanachama wake, kama una hoja ya msingi hebu nioneshe ni wapi nilipotukana, na kama sijatukana usinifundishe mimi jinsi ya kuwakilisha hisia zangu, kama una mtoto nyumbani huyo ndio mtu sahihi kumfundisha mitazamo yako na yale uyapendayo. siko hapa kumfurahisha mtu au kikundi fulani cha watu, nipo hapa kusema kile ninachoamini, ambacho ni ukweli daima. au signature yangu ndio inakutia kiwewe!?
 
Ndio maana na mimi naona post hii ni mazingaombwe sidhani kama UVCCM wangeanza kuijadili au kuitupia lawama TISS kwa mambo ya kisiasa na si ya usalama wa taifa.UVCCm ni chombo au taasisi ya kisiasa kwa ujumla wake wote kama ina jambo lingepelekwa kwa mwenyekiti wake JK ili likashughulikiwe kiserikali.


Nduka, lakini si ni9 ukweli wa wazi kuwa kama kweli wana ushahidi TISS haimsaiddi rais... si watumie marungu waliyonayo bungeni?!!!
CCM ndiyo yenye wabunge wengu, tena this time wengi ni vijana!!! It would have been wise to lobby for real reforms!!

Haya ni mazingaombwe hadharani ambayo wamezoea kuyatoa, lengo ni ku-divert burning issues out of discussion!! Stuka!!
 
Si wewe tu unayejua mengi kuhusu kikao hicho hata mimi nina chanzo changu cha kuaminika ndani ya kikao hicho ajenda ya TISS haikuwepo na itakuwa imepikwa kwa lengo lilelile la kuifanya nchi ielekeze macho na masikio yake kwenye migogoro ya kisiasa badala ya kutuhudumia wananchi.

Kwa bahati nzuri najua walichokisema UVCCM na wala si hiki kilichowekwa hapa, na kwa kuwa mleta mada na wachangiaji wote wanaujua ukweli huu kinachofanyika hapa ni kupoteza muda tu.
 
BLUE..hata chizi alitegemea hii kutoka kwa mwanakijiji mkombozi wa wa tanzania anayepigania uhuru kutoka nje ya nchi.

RED.. Kwa bahati nzuri watanzania walio wengi hawakupenda hayo mabadiliko, ndio maana hawakuinunua ilani ya CDM.
Nina wasiwasi na wewe!! Itabidi nifuatilie kila comment yako humu jamvini.
 
bila TISS jk angetangazwa mshindi wa urais?
hao uvccm wanashangaza sana
Walihaha bila kona kuhakikisha kuwa JK anashinda. Ina maana UVCCM wanataka kutema BIG G kwa utamu wa karanga za kuonja? Leo hii wanaishutumu TISS wakati ndiyo iliyowapa CCM ushindi!
 
kama wewe sio sehemu ya jawabu,basi ujue wewe ndio sehemu ya tatizo" nimeipenda hii......... UVCCM hawawezi kujitoa katika moja ya washauri wa Rais kwani ni moja ya jumuia za CCM. Kama UVCCM wanaona sio sehemu ya majibu ya kisiasa yanayotokea ndani ya CCM basi nao ni sehemu ya tatizo na ndio hapo UVCCM wanataka kucheza rafu mbaya kwenda TISS.


hawa umoja wa vilaza wa ccm(uvccm)wamepoteza dira na hii yote kwakuwa wao wenyewe ni zao haramu la wazazi wao baba zao na mama zao w
ccm ya wazee,wataongea kila neno lakini mwisho wa siku hawatatatua tatizo kkuwa huyo mkwere wanaemtetea ndio sehemu ya tatfizo.
"kama wewe sio sehemu ya jawabu,basi ujue wewe ndio sehemu ya tatizo"
 
Mtoto wa mbwa ni mbwa mdogo,uvcc ni vifisadi vidogo vinataka kutuchezea akili
vipotezeeni havina mpango,vinatafuta cheap popularity
 
TISS imekuwa kama dust bin/ dump/ shimo la takataka. Siasa zote za maji taka zinatupwa TISS.
 
Kwanza KIKWETE ameanza kuwa Mmbea....Si vizuri kwa Mheshimiwa Raisi kuanza kuongea Umbea wa kuwashawishi wananchi wasiikubali Chadema...wakati Hakuna Kiongozi hata Mmoja wa Chadema aliyepita Majumbani kuwapeleka Wananchi Barabarani Kuandamana....na kusikiliza maneno ya Dr. Slaa...

Kikwete amejipotezea UWEZO wa kuwa Rais kama kuna mtu anaona kwa Jicho kama LANGU...Rais HAPASWI Kukaa mbele ya Kamera na KULALAMIKA kama MlalaHOI! Na WATU hawaangalii Upande wa Pili wa Sarafu,KWAMBA WANANCHI HAWALAZIMISHWI KUANDAMANA au Kusikiliza HOTUBA ZA CHADEMA......................Wanaenda Wenyewe! Ni dalili ya KUCHOKA NA MAISHA NA UONGOZI ULIOPO. NA Badala ya Mtu Kama RAIS Kuliona Hilo...

Analalama tu katika TV na Wapambe wake wanaopata Ubunge wa Viti Maalumu kwa KUJIPENDEKEZA Kwao wanaungana Kulaumu CHADEMA. Pengine Mfumo wetu wa ELIMU Hautufundishi Kufikiria kabla ya kusema au Unatufundisha ila kuna watu Wanaamua tu Kusema Kabla ya Kufikiri.


Japo UVCCM Wameliona Hilo but Nao Ni wanafiki Tu! Hasa pale wanapoacha RK aendelee kuchezea UVCCM kama anavyochezea Makochi ya Ikulu.......
Hakuna Marefu yasiyo na Ncha!
 
JE HAWA VIJANA WA UVCCM WAPO CCM KWA KUVUTIWA NA UTENDAJI WA CHAMA AU NDO WAPO KWA MATARAJIO YA KUTAWALA BAADA YA BABA ZAO MAFISADI KUTOKA!!!!???koz sidhani kama kijana mwenye akili timamu anaweza kusimama mbele ya vijana wenzake na kusema bila haya kuwa yeye ni CCM Pasipo na maslahi yake binafsi ila wajue kuwa siku zote ukweli hautakufa kama hawaamini wataona,,hivi sasa wanahisi DR SLAA NA CDM YAKE NDIO CHANZO ila hata wakifa mzimu wa watanzania wenye tabu na njaa na waliokata tamaa utazidi kuwafuata.

Hao UVCCM wana ganga njaa tu ndugu yangu.
 
Unapotaja jina la Jk unamuona kwanza kama mwislamu au Rais wa nchi? Je unaweza kusema mwislamu anaiharibu nchi? huoni hapo utakuwa unagusa hisia za waislamu wengine wasio na hatia? Kwa nini umpatie mtu jina la bandia la dini yake au jina la kabila lake wakati wa kujenga hoja? Unataka kusema kuanzia leo mbowe naye tumwite mchaga? acha haya hayajengi nchi.

hata mwalimu kumwita mchonga haikuwa kosa kwani kabila lake ni mzanaki, mchonga lilitokana na jinsi meno yake yalivyokuwa yamejipanga hivyo lililenga meno yake sio wazanaki.Jina la Mchonga hata kama ni la utani lilikuwa halihisishi mtu mwingine kama ilivyo kwa kabila, jinsia, rangi au dini.

kumbuka kumpa Rais jina la utani ni jambo la kawaida lakini zingatia hisia za jamii.

Kwa hiyo kumuita mwana CCM nalo ni kosa? mbona Nyerere alikuwa anajiita mzanaki bila kificho? mimi sioni kosa kuitwa Mkwere, wengine Mh kabla hatukujua ni kabila gani, sasa kabila lake linajulikana kitaifa si fahari kwa kabila lake?. Kwa hiyo tuzuie majina kama JK vile vile!!
tuache kuchanganya mambo, kama ni mkwere ni mkwere, kama ni muislamu ni muislamu, kama ni mwanaume ni mwanaume, kama ni CCM ni CCM. Hakuna kati ya haya niliyoyataja yana Tusi ndani yake.
 
Maudhui ya taarifa hii ni kama imetoka kwa mwanachadema ambaye alikaa pamoja na Dr Slaa wakipata bia ndipo stori za TISS na UVCCM zikajitokeza. Dr Slaa aliota CCM muda wote lakini hii isitufanye wote tukashindwa kuchambua ukweli wa thread za kichochezi kama hii. TISS inaweza kuwa na mapungufu kama ilivyo kwa taasisi zingine zote lakini tuitendee haki penye kuhitajika haki.

This is interesting!Ombwe la Fikra ndilo chimbuko la Ombwe la uongozi,slave mentality nk

Kuchambua!Ungeonyesha mfano,sasa umechambua nini hapo? Is TISS better? Do we have records to show this at this point? Are we not getting ahead of ourselves here asking for a fair judgement for failed institution which we have yet to see do anything worth judging?

Halafu Uchochezi tafsiri yake ni nini?Hebu toa tafsiri ili usije ukaonewa,I agree with you kwenye uchambuzi wa hoja bila Ushabiki but you have failed misarably to deliver the same! Give us a break!





 
Tutajie basi japo majina ya wanausalama wachache ambao ni wakurugenzi wa mashirika, wakuu wa mikoa, wilaya mbona kama unaongeza mazingaombwe?

Nilishawai kuandika kuhusu hwa jamaa TISS, ni kwamba CCM ni kama bango tuu ila wanaoiaribu hii nchi ni hawa jamaa

Mfano:- CCM inatambua bila hawa jamaa awawezi kuingia madarakani na ndio maana kila mkoa kwenye uchaguzi wanakuwepo.
Pili-Hata kumchagua Rais ndio hao wanahusika na ndio maana utakuta marais wote nchini wanaongozwa na wao hawawezi kumweka mtu kama slaa au magufuli cause utakua mwisho wao wa kutukuzwa. Tatu ukikumbuka hawa jamaa ni inteligencier ya mwalimu na wengi wao waliku darasa la saba au hawakusoma kabisa so walipopata mwanya wakajisomesha ili kuja kushika mashirika yote hapa nchini na baadhi ya private sector kujipenyeza kwa ajili ya usalama wa taifa so, utakuta all CEO katika mashirika yote ya uma ni wao na baadhi ya private sector mwanajf utajidanganya kuuomba uCEO kwenye sector za umma na ukapata bila kuwa mwanausalama.
Nne utakumbuka wakati alipokua nyerere mashirika yalikua yanaongozwa na Raia wenye elimu na ujuzi na ndio maana yalikua active so, baada ya nyerere zikafanyika propaganda mpaka wakaweza kuyamiliki mashirika yote ya uma na ndipo kufa kwa mashirika mengi yakaanza hapo.
Tano- Jiulize mikataba yote mibovu lazma wao waipitie hata kuwaleta mainvestors matapeli wao ushiriki mfano EPA na kampuni zake zote zilizoshiriki utakuta ni wao
Sita- Rais awezi kuja kuhutubia taifa bila wao kuhusoma hotuba na kuihakiki, Rais uandaliwa bajet kubwa na safari ukiwa na msururu wa wanausalama ilimradi wapate posho.
SAba- ulishawai kusikia wapi mjadala wa bajeti ya hawa watu? hata kujadiliwa bungeni? wizara zote zinaendakuomba fungu pale lakini hawa warecommend tuu tunataka kiasi fulani na akina mahesabu.

so wanajf mtasumbuka sana kuilaani CCM lakini ccm kwa ujinga wao wanatumiwa kama chambo tuu ila wahusika wanaoisumbua hii nchi ni wao.
Na ukiwa mfuatiliaji sana wanakumaliza hata slaa ataongea sana ila anakikomochake cause baadhi yao walishakula kiapo cha kutunza siri sifahamu kama slaa ameshakula kiapo ila ukishafikia grade kama ya slaa lazma usign hicho kiapo.

Nchi inaendeshwa na TISS na sio chama hata mweke chama gani TISS ndio inayoongoza nchi kupitia mgongo wa chama

Wana jf huu ndio mchango wangu kaa chini na tafakari.
 
Tutajie basi japo majina ya wanausalama wachache ambao ni wakurugenzi wa mashirika, wakuu wa mikoa, wilaya mbona kama unaongeza mazingaombwe?

Bernard Membe na Mizengo Pinda unawafahamu vizuri? au umetumwa kuja kusumbuwa watu wenye akili zao timamu na sio vipeperushi? for ur information hapa watu makini huwa hatuongei na mbwa, bali tunaongea na anaewafuga mbwa. peleka ripoti kwa wanaokutumia waambie hapa mnawekeza kitu ambacho hamtokuja kuvuna chochote zaidi sisi tutakuwa tuna upload document zote za uchafu wenu. endeleeni muone tunatoa bomu moja baada ya lingine.
 
wana JF, mi nafikiri tujitahidi kutumia lugha nzuri tunapomkosoa Mhe. Rais, tabia ya kupenda kumuita mkwere ni dalili ya ukabila, kwa sababu kama anakosea katika kutimiza majukumu yake au kama ana udhaifu ni wake binafsi si kwa sababu ya kabila lake. mimi si mkwere lakini sisi vijana tukendelea na tabia ya kumsema mtu kabila lake akikosea, tunaweka mazingira mabaya ambayo mtu atakuwa anachaguliwa kwa kabila lake
Point!!!
 
Ni kweli Usalama wa Taifa hawamsaidii Kikwete, kwani Tanzania hakuna Usalama wa Taifa. Hakuna kitu kama hicho. Kama kipo, basi ni kwa ajili ya kazi nyingine, siyo kwa ajili ya Usalama wa Taifa kama unavyofahamika kimataifa. Kimataifa Usalama wa Taifa unahakikisha raslimali za taifa zinalindwa, kampuni feki hazipati tenda, mitandao ya mafisadi haipati uongozi n.k. Huo ndio usalama wa taifa kama unavyojulikana duniani kote.

TANZANIA puuuuuuuuuuuuuuuuuu! Kwa nini? TISS ni CCM, kwa ajili ya CCM na usalama wa CCM siyo wa Taifa. TISS inashughulika na CCM, siyo na Usalama wa Tanzania. Tanzania haiwahusu, siyo kazi yao. Kuwa fisadi utakavyo, fanya fujo kadri inavyowezekana, fanya ujambazi na unyang'anyi mpaka basi, uza madawa ya kulevya; kama uko CCM kwa TISS wewe siyo hatari, huna athari kwa CCM wanayoilinda. Ila ukitaka kuwajua bwana, kuwa balozi wa nyumba kumi wa CHADEMA ... wewe oooooooooooooh ni hatari sana...............
 
Back
Top Bottom