UVCCM ruksa kujadili urais

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Imeandikwa na Anastazia Anyimike;
Tarehe: 29th October 2011


VIJANA wa CCM nchini wameruhusiwa kujadili urais wa mwaka 2015 na si kujadili nani atakuwa rais kutokana na chama chao.

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Steven Wasira, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Wazira ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, alisema si busara kuzuia mawazo ya vijana ambao ndio wanaoshika mhimili wa nchi, kuacha kujadili urais.

"Utaratibu wa chama chetu uko wazi, linapokuja suala la mgombea urais, kuna taratibu zake ndani ya chama, lakini hatuwezi kuzuia vijana kujadili urais, kwani ndio mhimili wa baadaye wa nchi.

Lakini hawatakiwi kumjadili mtu au sura ya mtu. "Unajua unapotaka kuzungumzia urais kwa kigezo cha sifa za rais, lazima utaangalia matatizo ya Tanzania ambayo ndiyo yanayotengeneza sifa za rais.

Tunataka urais kuwa ajenda na si sura ya mtu," alisema. Akizungumzia mgogoro wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Arusha, Wasira ambaye ni mlezi wa chama hicho mkoani humo, alisema mgogoro huo umemalizika baada ya kukutanisha pande mbili zilizokuwa zinavutana.

Alisema baada ya kukutana na wahusika, amebaini kuwa kukosekana kwa mawasiliano yanayozingatia kanuni ndicho kilikuwa kilio cha kujengeka kwa hisia ambazo zilikuwa zinachangia mtafaruku.

"Hakuna hata mtu aliyeeleza chanzo, tukabaini kuwa tatizo lilikuwa ni kukosa mawasiliano kati ya wilaya na mkoa, na hili lilichangia hisia zaidi kuliko jambo lenyewe. Baada ya kukutana na pande zote, sasa naweza kutangaza kuwa tatizo hilo limekwisha na sasa wanaungana kuimarisha chama," aliongeza.

Aidha, Wasira alikiri kuwa mtafaruku huo ni matokeo ya kushindwa katika jimbo la Arusha Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2010 na kuwa vijana walikuwa na maoni tofauti kutokana na kushindwa huko.

Katika uchaguzi huo, jimbo hilo lilichukuliwa na Godbless Lema wa Chadema.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, alisema mgogoro uliokuwa Arusha, haukuhusu mgombea urais mwaka 2015 na kuwa taratibu za kumpata zinajulikana ndani ya chama.

" UVCCM haina mgombea urais kwa ajili ya uchaguzi ujao, utaratibu ndani ya chama uko wazi, muda ukifika watu watatangaza nia na sisi tutampigia debe mtu atakayepitishwa na chama na si vinginevyo," alisema Shigela.

Ziara ya Wasira ilimkutanisha na UVCCM wilaya ya Arusha, wajumbe wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arusha Mjini, Baraza la Mkoa, Kamati ya Siasa na Baraza la Wazee katika vikao vilivyohudhuriwa pia na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda.

Katika siku za karibuni, Arusha iligeuka chimbuko la vita vya maneno miongoni mwa makada wa CCM, hulka ambayo ilisambaa hadi kwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho hasa kutokana na falsafa ya kujivua gamba.

Awali, mgogoro ulikuwa baina ya baadhi ya vijana wa wilaya na mkoa wa Arusha na Katibu wa CCM wa Mkoa, Chatanda, ambaye pamoja na viongozi na makada wengine, walituhumiwa kwa kilichoelezwa kuwa ni kusababisha chama hicho kipoteze ubunge wa Arusha Mjini.
 
mi naona waendele kujadili nan atakuwa rais ili wakomeshane kabisa, mwisho wa cku tunazika chama cha magamba
 
Aliyeangalia sifa na sio mtu ni Nyerere tu wandugu nje ya hapo tusidanganyane. uvccm kazeni buti kujadili watu vinginevyo ni hadaa tupu mtashtukia ni genda inatakiwa!!
 
IQ ya mtu unaipima kwa matamko mawili katika suala moja, jana alisema uvccm kuzungumzia masuala ya uraisi ni uhaini, leo uvccm wanaruhusiwa kuzungumzia uraisi, kesho je?
 
Anayetaka urais CCM atafute support ya Mkapa, kumbuka Nyerere ndio aliye msupport rais Mwinyi,akafanya hivyo tena kabla mauti hayajamkuka kwa kumpendekeza Mkapa. Ikaja zamu ya mwinyi akampendekeza rais Kikwete, na sasa 2015 ni zamu ya pendekezo la mkapa, na 2025 ni pendekezo la Mh. rais Kikwete.

Na awamu ya kwanza ilikua ya kanda isiyo ya pwani,awamu ya pili, tatu na nne zote zikawa ukanda wa pwani, sasa ni zamu ya ukanda usio wa bwani.

Huo ndio mtiririko...hamtaki acheni.
 
Anayetaka urais CCM atafute support ya Mkapa, kumbuka Nyerere ndio aliye msupport rais Mwinyi,akafanya hivyo tena kabla mauti hayajamkuka kwa kumpendekeza Mkapa. Ikaja zamu ya mwinyi akampendekeza rais Kikwete, na sasa 2015 ni zamu ya pendekezo la mkapa, na 2025 ni pendekezo la Mh. rais Kikwete.

Na awamu ya kwanza ilikua ya kanda isiyo ya pwani,awamu ya pili, tatu na nne zote zikawa ukanda wa pwani, sasa ni zamu ya ukanda usio wa bwani.

Huo ndio mtiririko...hamtaki acheni.
Umelewa gongo na bangi za week end wewe. Endelea kuweweseka tu!
 
Umelewa gongo na bangi za week end wewe. Endelea kuweweseka tu!

Gongo ndio kiini cha pombe yote haujui hilo...Pole...!

We si umetumwa unachangia kwa kutummwa sie tunaongea hali halisi subiri-time will tell
 
Suala hili halikuwa kwenye hadidu za rejea za kazi ya huyo fisadi Wassira. Yeye mwenyewe ni wakala wa mafisadi ambao ndiyo waliwatuma hao wahuni wanaojiita UVCCM kuropoka waliyoyaropoka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom