na kweli, watakua wametumwa hawa, hatoki mtu, kwanza wachukue passport yake kabisa ..hatoki mtu, wasije wakaleta story za Balali, oh sijui tukimtaka tutamrudisha, mara sijui amekufa.......HATUDANGANYIKI!Wanataka kutoroshana kijanja,ili asiwepo wa kuhojiwa kuhusu mabilioni yetu,asifukuzwe huyo tunataka kushuhudia anaozea jela pamoja na wenzake,
wanaleta janja ya nyani kula mahindi mabichi.
Hivi Rostam ndo fisadi pekee Tanzania nzima? Maana kila kitu Rostam Rostam....
maneno mazito sana hayo!kwanini afukuzwe? kwani jela za Tanzania zimejaa?
kwanini umfukuze raia mwenzako? wanaofukuzwa kwa makosa ni diplomats kwa sababu ya immunity! SHERIA itumike na nipo tayari kodi yangu itumike ipasavyo kwenye kutunza wafungwa magerezani!
wanataka kuleta mambo ya BALALI, "apotelee" nchi za nje!Ni vizuri sana kusoma alama za wakati..
CCM vijana wapo mbioni kumwondoa Rostan nchini kwa sababu issue zote za Ufisadi zinatakiwa kuzungumziwa na kama watamwondoa Roastam nchini basi ushahidi wote kuhusu EPA,Richmond, Dowans na upotevu wa mabillioni ya fedha yatakosa mshtakiwa au ushahidi, hivyo yatakwisha kama ile scandal ya Balali..
Mimi nitasema kama kweli wana nia nzuri Rostam ashtakiwe kwanza na kufikishwa mbele ya sheria ikiwa chama kinahakikisha yeye ni fisadi na ndio sababu kinamwengua.. Huwezi kumfukuza mtu kazi kisha ukashindwa kumfikisha mahakamani unless kuna sababu maalum..
CCM wanacheza kuduku na maisha ya Watanzania na wajinga wengi wataingia mtego huu. Matatizo ya CCM yapo ktk utendaji kazi na ndipo Rostam anapoingia kwani hizi siasa za chama haziwahusu wananchi..Mhujumu uchumi hafukuzwi bali kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria..
Na mizizi ya Ufisadi imefika mbali sana kiasi kwamba sidhani kama kuna mtu msafi ndani ya uongozi uliopo kwani majuzi tu nilipokuwa bara nimeshuhudia viongozi wa serikali na Wabunge wetu wakinunua maelfu ya ardhi za wakulima kwa kodi za wananchi..Kila mbunge ana mahekta ya ardhi kama mali zao binafsi tena wanaitana kwa makundi na hakuna anayeona uharamu wa vitendo hivi...
Tunaunda kundi la wakoloni weusi wenye kumiliki ardhi kwa kuwahadaa wananchi kuuza ardhi zao, badala ya wao kuwa washauri wazuri wa wananchi ktk kilimo kwanza.. Shame on you all!
Wamekula sasa hawana cha kumtumia kula zaidi ndio wanaongea pumba hizi kweli wana ccm wanakazi afukuzwe kwa nini wasisemwe ashitakiwe
Ili wote tusikie ukweli wa mambo, afukuzwe aondoke na siri zao wote mafisadi tu