UVCCM Maswa wataka Shigela atimuliwe

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
BAADHI ya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu, wamemtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kumfukuza kazi Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Martine Shigela, kwa madai ya kukidhoofisha chama.

Wakizungumza mjini Maswa na waandishi wa habari, walisema kuwa kauli zinazotolewa na Shigela, dhidi ya viongozi wastaafu zinalenga kukidhoofisha chama hicho hivi sasa kinapokabiliwa na migogoro mingi.
Walisema kuwa viongozi wastaafu wakiwemo mawaziri wakuu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa kukitaka CCM ijibu hoja za wapinzani hasa chama cha CHADEMA kinazozitoa katika mikutano yake ni ya msingi na si za kukitisha chama.

“Kauli za Sumaye na Lowasa zilikuwa sahihi katika kukielekeza chama chetu jinsi ya kujibu hoja za wapinzani hasa CHADEMA walizokuwa wanazitoa katika mikutano yao, hata siku moja huwezi ukafua nguo chafu gizani ni lazima uwe kwenye mwanga ili uweze kuona uchafu wote,” alisema John Makina.

Waliongeza kuwa Shigela, ametekwa na kundi moja la vijana ambalo linajiandaa kumtoa mgombea wa urais ndani ya CCM mwaka 2011 ndiyo maana anawapinga wanaokikosoa chama hicho .

Walisema kuwa Rais Kikwete aliahidi kukisafisha chama hicho kwa kujivua gamba na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo ni vizuri katika mabadiliko hayo na Katibu Mkuu wa UVCCM akaondolewa katika nafasi hiyo. Aidha, vijana hao walitoa angalizo kuwa iwapo Mwenyekiti wa CCM Taifa hatazingatia maombi yao hayo basi wako tayari kujitoa ndani ya chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani.
 
na Samwel Mwanga, Maswa

BAADHI ya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu, wamemtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kumfukuza kazi Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Martine Shigela, kwa madai ya kukidhoofisha chama.
Wakizungumza mjini Maswa na waandishi wa habari, walisema kuwa kauli zinazotolewa na Shigela, dhidi ya viongozi wastaafu zinalenga kukidhoofisha chama hicho hivi sasa kinapokabiliwa na migogoro mingi.
Walisema kuwa viongozi wastaafu wakiwemo mawaziri wakuu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa kukitaka CCM ijibu hoja za wapinzani hasa chama cha CHADEMA kinazozitoa katika mikutano yake ni ya msingi na si za kukitisha chama.
“Kauli za Sumaye na Lowasa zilikuwa sahihi katika kukielekeza chama chetu jinsi ya kujibu hoja za wapinzani hasa CHADEMA walizokuwa wanazitoa katika mikutano yao, hata siku moja huwezi ukafua nguo chafu gizani ni lazima uwe kwenye mwanga ili uweze kuona uchafu wote,” alisema John Makina.
Waliongeza kuwa Shigela, ametekwa na kundi moja la vijana ambalo linajiandaa kumtoa mgombea wa urais ndani ya CCM mwaka 2011 ndiyo maana anawapinga wanaokikosoa chama hicho . Walisema kuwa Rais Kikwete aliahidi kukisafisha chama hicho kwa kujivua gamba na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo ni vizuri katika mabadiliko hayo na Katibu Mkuu wa UVCCM akaondolewa katika nafasi hiyo. Aidha, vijana hao walitoa angalizo kuwa iwapo Mwenyekiti wa CCM Taifa hatazingatia maombi yao hayo basi wako tayari kujitoa ndani ya chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani.
 
Sasa hivi ndo inavyotakiwa. Piganeni wenyewe kwa wenyewe ila mnatakiwa kujua kuwa CDM nao wanajijenga.
 
kikwete, makamba, hiza, shigela... Hao vijana wa Maswa hawana macho?! Hata hao wakitoka lazima watafutwe wa aina hiyo kushika nafasi hizo. Sababu kumuweka mwenye akili timamu hapo ni sawa na mtu mwenye nguo safi nyeupe kukumbatiana na watu kumi waliofunikwa na matope.
 
Back
Top Bottom