UVCCM Kuanzisha Mapinduzi Forum (MF) sawa na JF?

Status
Not open for further replies.
Mkuu NM, waambie wajivue gamba kwanza kabla ya kuanzisha hiyo Mapinduzi Forum ambayo itapata wanachama wenye gamba tu na haitakuwa na umaarufu kama wa JF. Njemba hizi zinahaha ile mbaya kutafuta umaarufu wasiokuwa nao.
Kabla ya kuanzisha forums yao nawashauri yafuatayo:
Wakarabati magazeti na radio zao kama uhuru yawe na mvuto na sio kufungia maandazi na radio kua kituoa ambapo watu wanafungulia kusikiliza utabiri wa hali ya hewa na saa na badala yake yazungumzie matatizo na kero za wananchi na sio kuwalinda viongozi wa CCM na serikali na kuficha maovu yao.Waruhusu mijadala na midahalo huru ISIOCHAKACHULIWA itakaowashirikisha viongozi wake pia,waheshimu mawazo ya kila mtu bila kujali kabila lake,dini,jinsia ushabiki aunafasi yake katika chama au jamii na chama cha CCM kiondoe thana ya kua watatawala maisha na viongozi wake ni miungu watu (Hawakosei na hawapashwi kukosolewa)Waruhusu midahalo katika vyombo vyao vya habari kwa kushikisha pande zote(WASIKIMBIE MIDAHALO)Wakifanya hivyo watafanikiwa au hawatakua na umuhimu wa kuanzisha forum yao bali kujiunga"JAMIIFORUMS"Wakianzisha forums yao kwa kukiuka hayo niyoyataja na mengineyo forum yao haitatofautiana na vikao vya CCM .
Kuhusu mamluki na viwavi waliomwagwa Jamiiforums jia pekee ya kupambana nao ni KUWAIGNORE wanapoleta threads na posts za kipuuzi na kupambana nao kwa hoja wanapoleta hoja muafaka.
 
Waanzishe alaf watangaze tender ili tukawasaidie ktk kuji register,kushika mouse na kuwasha komputa,kisha kupost thread,najua watu wale ujuzi umewapita kushoto! Hata kwa michuzi sifunguagi,nliingia mara moja wakati kashaga analalama na ID yake,tangu apo nliapa kutorudi huko. Tunaisubiri mapindunz forum inaweza ikaja na ajira wakuu!
 
Watakao kwenda huko si watoto zao na wasiosoma kama wao. Let them start even nyumba kwa nyumba, wanavyombo vingapi vya habari hapa Tanzania? ccm inatumia vyombo vya serikali na vyomba vya binafsi kuwadanganya wananchi na mpaka sasa kikwete kashindwa kuwadanganya wananchi. Kila kitu kina mwisho na hata mkifanya tulale na nyie nyumba moja, hakuna atakubali mnachokisema.
1. Daly news
2. TBC
3. ITV
4. Safari na mizinguko ya jk
5. hotuba za jk
6. Vipindi vya live radio

Yote Haya wananchi wameshafunga masikio na hawawataki, kitu gani kigumu kusikia?

"Ukiwa na kinyesi usoni unatakiwa uweze kukisikia kinanuka sio mpaka mwenzako akukumbushe, poleni maskini wakubwa nyie"

"maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana"
 
kwani inaanza lini na ikianza naomba link fasta au kama kuna wataalam wa kuunda forums ndo kazi zenyewe hizo...mtajuaje kuwa wao ni wavivu wa kufikiri yaan jf ni kama tiGO inaanzisha wao wanafuata..
Maandalizi mema wazee wa magamba..
 
Mapinduzu Forum, their motto would be: 'where we dare squander masses property for our own interests'.
 
Umoja wa vijana wa ccm wana matatizo ambayo wasipoepukana nayo wao ndio watakuwa njia ya kuua kabisa baba yao ccm; tatizo lao ni kwamba tofauti na vijana wa zamani kama wakina Patrick Qorro [ ambae hata hawajui kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa umoja huo huko nyuma] hawa vijana badala ya kufikiri jinsi ya kuendesha jumuiya yao, mafisadi wanafanya kazi ya kufikiri kwa niaba yao!! Sasa basi kwasababu ya mapungufufu haya ndio maana wanashindwa hata kujua kuwa umaarufu wa JF hautokani na members wake kuwa vijana bali ni kwasababu JF haibagui umri wa wanachama wake na ndio maana michango ya wazee inawaelimisha vijana na wazee wanajifunza mambo mapya walioyakosa enzi za ujana wao toka kwa vijana. It is this symbiotic relationship ambayo inaipa nguvu JF. Sasa nyie UVVC anzisheni yenu ya hao vijana wenye magamba tuone mtakakofika!!
 
Wajinga ndio waliwao.........wajinga tu ndio watakao kubali kuliwa na mitandao ya kijinga itakayoanzishwa na ccm na vibaraka wake.......acha watumie mabilioni waliyoiba kuwarubuni watz lkn wajue watz wa sasa hawakubali uongo wa zaidi ya miaka 40 wa ccm...........
Jf songa mbele...tuko pamoja
 
Katika kile ambacho kinasemekana kuwafikia vijana wengi ambao ndiyo watumiaji wa mtandao wa mawasiliano UVCCM wamefikia mamuzi ya kuanzisha Mtandao wa kijamii utakao julikana kama MAPINDUZI FORUMS.

Uwamuzi huu umetokana na vuguvugu la matukio kadhaa yaliokitikasa chama hicho kongwe hapa nchini hivyo kuamua kuunda tume (task force) iliyoongozwa na katibu mkuu wa chama hicho Wilson Mukama pamoja na mambo mengine tume hiyo ilikinyooshea kidole mtandao maarufu wa kijamii Jamii furum kuwa ni hatari kwa mstakabali wa chama chao. Katika mapendekezo ya tume hiyo walipendekeza umuhimu wa kuwafikia vijana wengi kwa njia ya mitandao ya kijamii ili kurudisha mvuto kwa vijana ambao wameoneka kukosa mvuto kwa vijana.

Hali hiyo ndio imepelekea umoja huo kuamua kuwa na MF ili kuwafikia watu wengi hasa vijana.

Binafsi nawapongeza kwa wazo hilo lakini nilitegemea chama hicho kingekaa chini na kufikiria kwa uzito tatizo la kimsingi la chama hicho, tatizo la CCM ni kutokana na kuchafuka kwa ufisadi kiasi ambacho hakiwezi kutoka mbele ya jamii hasa vijana kifua mbele kupinga ufisadi hivyo kuwa na mtandao wa Mf kitakiweka chama hicho kwenye wakati mgumu zaidi ikiwa makombora ya mitandao mingine kama FB, Twitter na JF wanashindwa kuyahimili kiasi wamebaki kulalamika je wataweza kuhimili makombora yatakayoelekezwa kwao na uchafu wao, nani kawandanganya JF huwasifia CDM tu? Ni mara ngapi CDM na viongozi wake hutupiwa makombora mazito? Wamuulize Zitto, Mbowe na Dr. Slaa. Unaporuhusu mijadala ya kijamii wasidhani ni mahali watakaposifiwa tu, na hapo ndipo naona mtandao huo wa MF Utawapindua badala ya kuwajenga
 
All i know ni kwamba hata siku moja huwezi kuiga original idea na ndio maana counterfeits or dawa za kuiga (out of patent) hazitapata heshima kubwa. on the same line, hata uweke kiwembe kwenye coca cola au tusker, watu watakunywa tu

I advice JF administrators to be more stringent na watu wanaoharibu forum na wakizidi kureveal their true IDs if possible, in addition as this has been declared a war of its kind, we need to protect our Tanzania morals and priviledged endapo tutahisi kwamba fulani ametumwa

we dont need the likes of MS kuja kutuharibia hewa and on the same note as a move towards cleansing bullshit in our forum tuanze na restrictons zaidi

But if worse comes to worse, basi tutajiunga na mapinduzi forums na kwenda kuitia najisi, kwani hakuna lisilowezekana kwenye cyber world
 
Kwa kifupi sana ni kwamba wamechemka mbaya, JF haikutafuta watu wala kujitangaza mahali popote ila matendo na sauti ya kuu na ya chini chini ndio iliyojazwa mioyoni mwa wapenda maendeleo, so kuna tofauti kubwa sana kati ya JF na hio mimba ambayo bado haikazaliwa! Hivi jirani akianzisha genge la mboga mboga na wewe unaanzisha lako au unafungua kitu tofauti? For sure, they wont make it! au hakutakuwa na hoja za maana zaidi ya mipasho na majungu, Hivi kweli CCM watakua na mada gani inayohusu nini? wizi? NO!!
 
waanzishe tu hicho kimeo chao. Sisi tutazidi kuwazodoa. Watu wenye kutumia ubongo kufikiri wala hababaishwi na propaganda za kifisadi. Mie nadhani wangekuwa na akili endapo wangeunda jopo la kuzifanyia kazi kero zote zinazojadiliwa JF. Wangekuwa wanachukua hatua za makusudi. Lakini waanzishe Mapinduzi Forum, Jamhuri Forum, Muungano Forum, Azimio Forum, Uhuru Forum, Kujivua Gamba Forum na kadhalika lakini Jamii Forums ni zaidi ya forum.
Wanahangaika tu. Waanzishe tukajiunga ili kuwachora.
 
Tutawafata huko huko kwenye hiyo mapinduzi forum tuwatie kitanzi cha mwisho na kuwafutilia mbali kwenye medani za siasa za Tanzania.

Tunaisubiri kwa hamu hiyo mapinduzi forum
 
Mimi naunga mkono sana CCM kuwa na forum yao, pia ningependa chadema wawe na yao kama vile ambavyo professional bodies nyingi zinazo kwa sasa

Napenda hivyo ili jamii forums ibaki kwa wale griti thinkaz wenye kudare talk openly bila kuogopa victimizations za vyama vyao....

Nawatakia heri hasa wale waliotumwa kuja kuchafua hewa huku kwamba waende wakajenge kwao, huku waache wenye mapenzi mema
 
all i know ni kwamba hata siku moja huwezi kuiga original idea na ndio maana counterfeits or dawa za kuiga (out of patent) hazitapata heshima kubwa. On the same line, hata uweke kiwembe kwenye coca cola au tusker, watu watakunywa tu

i advice jf administrators to be more stringent na watu wanaoharibu forum na wakizidi kureveal their true ids if possible, in addition as this has been declared a war of its kind, we need to protect our tanzania morals and priviledged endapo tutahisi kwamba fulani ametumwa

we dont need the likes of ms kuja kutuharibia hewa and on the same note as a move towards cleansing bullshit in our forum tuanze na restrictons zaidi

but if worse comes to worse, basi tutajiunga na mapinduzi forums na kwenda kuitia najisi, kwani hakuna lisilowezekana kwenye cyber world

i commend you on ths, bravo!
 
Nasubiri ianzishwe NIIPIGE PINI nitahakisha haipati wateja wenye akili timamu labda hao wasiojitambua kuwa wanakufa na lichama lao! Wanajf tupo vitani! Vita ni vita mraa tutahakikisha magamba liseva lao halifanyi kazi!

Taaluma yangu yote nataka kujitolea kuwaokoa watz dhidi ya sera mufilisi za lichama hili! Mungu ibariki tz, mungu ibariki jf
 
kwa hiyo mtuachie JF yetu mwende kwenye forum za vyama vyenu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom