UVCCM kanda ya ziwa kuasi - haitambui matokeo ya uchaguzi uvccm sasa kuunda umoja mpya( UMVCCM)

Kwa watu makini CCM bado nzuri sana kiitikadi kuliko chama chochote nchini, matatizo yake ya utekelezaji yanahitaji kupingwa na wale wanaoamini ubora wa CCM wakiwa ndani ya CCM na siyo nje ya CCM (CDM siyo mbadala wa CCM). ndiyo maana wana matumaini ya kukirudisha chama kwenye misingi yake halisia na kuchangia ujenzi wa demokrasia (ikiwemo kuvikuza vyama visivyoaminika sawa sawa kama CDM) na kujenga taifa lenye maendeleo, umoja na amani.

Mungu ibariki Tanganyika, mungu ibariki CCM imara.
wewe ulipokea ngapi mkuu??
 
niliwahi kuwashuri CCM waarishe uchaguzi huu kwa muda ili wapate muda wa kushughulikia matatizo yao ndani ya chama lakini hawakunisikiliza, saana waliniona punguani.kwa ubishi wao huo, sitshangaa CCM kuingia 2015 kwa maafungu.
 
Mtaishia kusemasema na kuitana halafu mnarudi kwenye rushwa maana mmezoea CCM....Kama mnaguswa kweli tangazeni kuachana na CCM tuwaunge mkono na kama vyama mbadala hamvioni basi anzisheni chama kipya watanzania tumechoka tutawaunga mkono
 
Hawa vijana wanalia tu kama samaki ndani ya bahari wakati machozi yanachukuliwa na maji.Mapambano dhidi ya RUSHWA HAYAWEZEKANI UKIWA NDANI YA CCM.
lazima mliondoe jiwe na boriti ndani ya macho yenu ili muweze kueleweka kwa watz.Rejea kauli ya JK juzi

''CCM INASEMWA VIBAYA NA RAIA/JAMII'' ameona,amethibitisha na amekiri hilo.

JAMANI NJAA,NJAA,NJAA NI MBAYA; ''NJAA NI MWANA MALEGEZA NA SHIBE NI MWANA MALEVYIA''

hawakukosea wahenga na hili linajidhihirisha kwa vijana wanaojipendekeza kuwa ni ccm wapenda haki wakati mioyo yao na nafsi zinawasuta.

UKIWA NA NJAA HATA WAZAZI WAKO UTAWAKANA TU....HAPO NDO VIJANA WA TAIFA HILI TULIKOFIKIA.
 
Kwani CCM ni mama yenu? Wacheni unafiki nyie, kwa vitendo vya rushwa ya wazi wazi iliyotolewa na mafisadi kusimika mtandao wao mnahitaji nabii toka anga za juu awambie kuwa hilo chama halifai?
 
Mwanzisha mada,

Je walioshinda uchaguzi walitoa rushwa?

Sijaona popote wanalaumiwa walioshinda naona malalamiko tu kwa wasiohusika!

Kaeni mtafakari acheni kukurupuka!

Uroho tu wa madaraka! Acheni unafiki.
 
Lakini, UVCCM Kanda ya Ziwa, Kwa nini kugomea uchaguzi? Kama hamkubaliana na falsafa HIZI za CCM, ya nini Kung'ang'ania huko? Ng'atukeni huko, tena hapo Mlipo si Kizota hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom