Uvaaji huu ni sahihi?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Wapendwa uvaaji wa suruali huku shati umechomekea kwenye chupi ni sahihi?
Kuna brazameni mmoja nilimwona kaulamba safi ila shati kachomekea kwenye chupi sasa bahati mbaya au nzuri ile chupi ikapanda juu kupitiliza mkanda nilishangaa sana je hii ni style mpya kwa mnao ulamba maana mi kuchomekea mpaka nipate mwaliko sehemu. Nakumbuka enzi zile tunakua kulikuwa na chupi zinaitwa VIP zile zilikuwa na tabia moja zinakatika kwenye maungio na kuwa kama andasketi alafu wkt unatembea inapanda juu mpaka kifuani bila wewe kujua kama chupi ipo kwenye garden love. Je ni stahiki mtu kuchomekea kwenye chupi?

Upande wa madada siku hizi kuna magauni flani hivi wao wanaita madela kama sijakosea wao wananunua dela kuuubwa utakuta nae anachomeka kwenye chupi upande wa kushoto na kulia kwa uchunguzi wangu mdogo nikabaini kuwa wanapenda maumbila ya nyuma yanajulikana kama wowowo yatune kiana nae aonekane mashaallah Mungu kamjalia maana toka nianze uchunguzi sijaona wale walio jaliwa hayo mawowowo wakifanya hivyo.
 
Pole kaka,

Ndo ukubwa huo...Jifunze kufurahia michezo ya wajukuu kama sie wenzio....La msingi wasidhurike..!!

Ila kweli uvaaji wa siku hizi ni utata mtupu!
 
as long as umependeza haijalishi

Noooooooo! hapa ndo ladies mnapokoseaga, ni kweli unaweza ukawa umependeza lakini hayo mapambo ya 'ndani' ni maalumu kwa watu wawili tu, labda kama ni 'biashara' inaweza kueleweka lakini kwa mtu ambaye ni respectiful, hapana!
 
kuna siku ndani ya daladala kavulana kakawa kanahangaika kupandisha suruali juu, wakati mwenyewe ndo aliyeamua kuvaa kata K. Kila mtu alikuwa anamshangaa ndani ya gari, maana hayo mambo tumeyazoea kuyaona from our 'sisters', kwa mvulana ilikuwa ni kiroja cha siku
 
Aisee zile chupi za VIP kwa kweli zilikuwa ni bikini za kiume kusema ukweli! Halafu ukiivaa baada ya siku mbili tu, unakuta kale kamkanda kanakokatiza huku 'chini' kutokea kwa nyuma kanakuwa keusiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, agrrrrrrr!!!!!!!!!
 
Aisee zile chupi za VIP kwa kweli zilikuwa ni bikini za kiume kusema ukweli! Halafu ukiivaa baada ya siku mbili tu, unakuta kale kamkanda kanakokatiza huku 'chini' kutokea kwa nyuma kanakuwa keusiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, agrrrrrrr!!!!!!!!!

Nimecheka kwa sauti kha!!!
 
Dah!naomba nikusalimie kwanza Broda!
Naona leo umekuja na jipya,kwa upande wa wanaume siwezi kusema chochote coz hiyo stail inaniboa sana unakuta kichupi chenyewe kichafu alafu ndio kajidai kuulambia lol!
Hii ya wadada nayo inaniachaga hoi tu coz wengi ni wale wa huku kwetu uswazi hata mapaka leo huwa sijui 7bu ni nn?
Saa ingine unakuta mpaka wa na wamama wanachomekea hizo dela kwa chupi,labda ni stail!
Japo kwa upande wangu sion km ni sahihi coz inakuwainaonyesha mpaka chupi ilipoishia yani wala haipendezi!
Ngoja tusubiri wavaaji labda watatujuza 7bu ni nn au ni stail na tutajua.
 
Bila kuachia WO WO WO utajuaje kama lipo?

Biashara matangazo babu eeeh!

Hivi imeshajaribu kufuatilia na kuwasemaesha wanawake wa aina hiyo? Unawez akuta maharage ya mbeya ukajipatia!
Kwani kuna mwanaume anakaataa ya bure? eti ma Brother....???
 
wapendwa uvaaji wa suruali huku shati umechomekea kwenye chupi ni sahihi?
Kuna brazameni mmoja nilimwona kaulamba safi ila shati kachomekea kwenye chupi sasa bahati mbaya au nzuri ile chupi ikapanda juu kupitiliza mkanda nilishangaa sana je hii ni style mpya kwa mnao ulamba maana mi kuchomekea mpaka nipate mwaliko sehemu. Nakumbuka enzi zile tunakua kulikuwa na chupi zinaitwa vip zile zilikuwa na tabia moja zinakatika kwenye maungio na kuwa kama andasketi alafu wkt unatembea inapanda juu mpaka kifuani bila wewe kujua kama chupi ipo kwenye garden love. Je ni stahiki mtu kuchomekea kwenye chupi?

Upande wa madada siku hizi kuna magauni flani hivi wao wanaita madela kama sijakosea wao wananunua dela kuuubwa utakuta nae anachomeka kwenye chupi upande wa kushoto na kulia kwa uchunguzi wangu mdogo nikabaini kuwa wanapenda maumbila ya nyuma yanajulikana kama wowowo yatune kiana nae aonekane mashaallah mungu kamjalia maana toka nianze uchunguzi sijaona wale walio jaliwa hayo mawowowo wakifanya hivyo.

bangi tu!
 
kama wowowo ipo,ipo tu.na kama hakuna,hakuna.mambo ya kuchomekea kwenye chupi ili yaonekane ni kujisumbua tu.coz,mwenye nacho hata avae gunia,itaonekana.
 
mhh hii inaendana na muhusika na malezi au makuzi, huwezi kuta mwanamke mwenye staha zake kachomeka ki hivo... kwa wanaume inaeleweka nahisi muhusika anataka akichpmekea isitoke shati ndiio maana anaweka ndani ya chupi
 
Fidel nilidhani na wewe ni brazameni la kileo kumbe sio?

Mi mgumu wa wagumu Lizzy na huwa sichuniki kirahisi mtoto nimezaliwa enzi za utawala wa mzee Julius natekeleza sera ya ujamaa na kujitegemea kwa matendo na chomekea siku za sikukuu tu napo kwa mwaliko maalumu kwa mwaka mara moja au mbili
 
Back
Top Bottom