Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 918
nimeshtushwa sana na habari hii, inaonekana serikali ya awamu ya nne haijajifunza kitu chochote kutoka makosa ya uuzwaji wa nymba za serikali uliofanyika wakati wa awamu ya tatu. kweli tuna safari ndefu sana!!
Kuuza nyumba za serikali si suala geni - Tibaijuka
Na Mwandishi wetu
2nd June 2011
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema kwamba suala la wananchi kuuziwa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siyo geni nchini na kwamba limekuwepo kwa muda mrefu.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipoombwa na NIPASHE kutolea ufafanuzi taarifa iliyoandikwa na gazeti hili jana kwamba, kuna mikakati iliyopangwa chini ya kamati maalumu ya wapangaji wa nyumba za NHC jijini inayotaka wapangaji wa nyumba hizo kuuziwa kwa bei sawa na bure,kwa hoja kwamba wamekaa kwa muda mrefu katika nyumba hizo.
Hata hivyo, NIPASHE nakualika pale Diamond Jubilee Juni 4 mwaka huu, saa tatu asubuhi ambapo nitakutana na wadau wote wa nyumba katika mkutano mkubwa utakaohudhuriwa na mimi na wasaidizi wangu wizarani, bodi ya NHC ,wapangaji wa nyumba za NHC na wadau wengine wote, uje utapata majibu, alisema.
Alisema katika mkutano huo, ndipo ufafanuzi wote utatolewa na msimamo wa serikali kuhusiana na ombi hilo utaelezwa. Jana gazeti hili liliandika kuhusu nyumba za Shirika la Nyumba nchini NHC ambazo ziko katika hatari ya kuporwa kama uporaji uliofanywa na serikali ya awamu ya tatu kwa kisingizio cha kuwasaidia watumishi wa serikali, hali iliyomweka Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwenye mtego mkubwa.
Safari hii mikakati imepangwa chini ya kamati maalum ya wapangaji wa nyumba za NHC wakijenga hoja mufilisi kwamba wanastahili kuuziwa nyumba za shirika hilo kwa bei sawa na bure kwa kuwa wamekaa muda mrefu kwenye nyumba hizo.
Uchunguzi huru wa NIPASHE na vielelezo mbalimbali vilivyokusanywa juu ya njama hizo, unaonyesha kuwa chini ya kamati hiyo shinikizo sasa linaelekezwa kwa Waziri Tibaijuka ili asaidie kulazimisha NHC kuuza nyumba hizo kwa wapangaji wake kwa bei ya chee kama walivyofanyiwa watumishi wa serikali wakati wa awamu ya tatu
CHANZO: NIPASHE