Uturuki kuijengea Tanzania Chuo Kikuu

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
RAIS wa Jamuhuri ya Uturuki, Abdulah Gul, amesema nchi yake itajenga chuo kikuu nchini kuendeleza uhusiano kati yake na Tanzania.


Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba wa ushirikiano kati ya Uturuki na Tanzania, Gul alisema pamoja na mambo mengine waliyokubaliana vipaumbele vitakuwa katika elimu, kilimo, biashara pamoja na afiya.


Mkataba huo ulitiwa saini jana na Waziri wa Kilimo na Chakula Steven Wasira kwa upande wa Tanzania, huku Waziri wa nchi Muastafa Saed Yavizicioglu akitia sahini kwa upande wa Uturuki.


Utiaji saini huo ulishuhudiwa na rais Gul wa Uturuki pamoja na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.


Rais Gul pia alisema shirika la ndege la uturuki litaanza safari kati ya Istanbul na Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya sekta ya anga.


Alisema ili kuhimarisha uhusiano huo watafungua ubalozi wao nchini Tanzania katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu.


“Katika kuimarisha ushirikiano tatafungua Ubalozi wetu hapa, na nimeambatana na balozi wenu mtarajiwa, balozi hebu sisimama wakuone, anaitwa Dk. Sander Gurbuz” alisema Gul


Mpaka sasa Tanzania inatumia ubalozi wa Uturuki uliopo nchini Kenya katika kufanya mambo yanayo zihusu nchi hizi mbili.


Akitoa shukurani zake kwa rais Glu, rais Kikwete alisema hatua iliyofikiwa itaongeza kasi ya ushrikiano kati ya Tanzania na Uturuki ushirikiano ambao awali ulikuwa unakuwa polepole.


Alisema ushirikiano huo utasaidia Tanzania kupitisha sauti yake katika nchi tajiri ulimwenguni kwa sababu uturuki ni moja ya nchi zinazo unda umoja wa nchi tajiri duniani (G8).


“kuna vikao vingi vya nchi tajiri ambavyo hufanyika mara kwa mara, tunategemea Uturuki itakuwa sauti yetu hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mtikisiko wa uchumi Duniani, kuziasa nchi nyingine zisipunguze misaada kwa Afrika” alisema Kikwete.


Pia alisema anamatumaini kuwa Uturuki itasidia katika kulinda usalama katika nchi za kiafrika, akitolea mfano Somali.


“Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, japo haijapata uanachama wa kudumu, naamini wana nafasi kubwa katika kutusaidia kwenye usalama wa nchi zetu za kiafrika” alisema Kikwete


Rais huyo wa Uturuki amemwalika rais Kikwete kufanya ziara katika nchi yake.


Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo wa mashirikiano, waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wasira alisema makubaliano hayo yatasaidia sana kuinua sekta ya kilimo na chakula.


Alisema makubliano hayo yatasaiia kwenye Utafiti, maunzo, pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.


“Makubaliano haya yatasaidia sana katika kubadilishana taarifa za vituo vyetu vya utafiti kwa, kufundisha watalamu wetu nchini Uturuki, pamoja na wawekezaji kuja kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo” alisema Wasira


Ziara ya rais wa Uturuki nchini ilianza jana, ambapo aliambatana na ujumbe wa watu zaidi ya 150 wakiwemo wafanyabiashara.


Wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania walikutana juzi katika hateli ya kempsiki jijini na kufanya mazungumzo.


Rais Gul ambaye ambaye aliambatana na mkewe Hayrunnsa Gul, juzi alitembeleya shule ya Feza iliyopo jijini Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Uturuki.


Gul baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo ya ushirikiano alifanya mazungumzo na rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abedi Karume katika hotel ya kempsiki, ambapo waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia.


Rais huyo wa Uturuki pamoja na ujumbe wake walimaliza ziara yao ya siku mbili jana, aliondoko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere majira ya saa 9 kamili alasiri na Ndege aina ya Airbus.


Alisindikizwa na mwenyeji wake rais Kikwete aliye ambatana na mkewe mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Peter Pinda pamona na badhi ya mawaziri
Source: Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom