Fahamu jinsi ya kutunza ngozi, iwe yenye afya na inayovutia zaidi

Simply

Senior Member
Oct 13, 2012
130
30
Habari Wana JF

Nauliza mafuta gani au tiba mbadala au njia gani inafaa tumiwa kwa mtu anayefanya kazi juani(sun rays) muda mrefu ili kutunza afya ya ngozi?

============

1595594946057.png

Ngozi ya mwanadamu inahitaji matunzo ili iweze kuwa na afya na mvuto wake wa asili. Ngozi isipotunzwa vizuri huweza kupata magonjwa kama mapele, ukurutu nk. Ngozi za watu hutofautiana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kutokana na maumbile kuna ambao ngozi zao zina mafuta na wengine kavu.

Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema.

Hivyo basi matunzo ya ngozi pia hutofautiana kutokana na aina ya ngozi ya mtu. Inatakiwa ujue wewe una ngozi ya aina gani, je ni ya kawaida au ina mafuta mengi au ni kavu, ili uweze kujua unatumia nini kuitunza na kuilinda ngozi yako. Maana sio kila mafuta au vilainishi vya ngozi humfaa kila mtu.

Unashauriwa kabla ya kutumia chochote pata ushauri wa daktari wa ngozi (dermatologist). Vinginevyo inashauriwa ujaribu kiasi kidogo cha kipodozi au mafuta yoyote unayotaka kutumia kwenye sehemu ndogo ya mkononi ili kuona kama inakubaliana na ngozi yako au la.

Njia za kutunza ngozi

Mlo

Vitu unavyokula vina mchango mkubwa katika ngozi na afya yako kwa ujumla. Ili kupata ngozi nzuri iliyo laini, nyororo na inayong’aa inabidi uache vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa viwandani, wanga, mafuta na sukari na badala yake kula protini, matunda, mboga na kunywa maji kwa wingi.

Hakikisha unakunywa maji si chini ya glasi nane kwa siku na matunda pamoja na mboga kila unapopata mlo.

Matunda na mboga za majani husaidia oksijeni kuzunguka vizuri mwilini na kwenye ngozi kuliko mafuta au kipodozi chochote unachoweza kupaka.

Protini husaidia kujenga ulinzi zaidi katika seli za ngozi ambayo ngozi inahitaji kukabiliana na ukavu wa ngozi. Nayo maji husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini na kusaidia vinyweleo kupumua vizuri, hivyo kuzuia bakteria chini ya ngozi.

Muda wa kupumzika
wengi hawatambui umuhimu wa usingizi katika kutunza ngozi na kuzuia kuzeeka haraka. Usingizi ni muhimu kwa ngozi yako sana, hakikisha unapata muda wa kutosha kulala usiopungua masaa 8.

Kifiziolojia, ngozi inafanya kazi kubwa sana wakati wa mchana katika kutunza mwili, kukabiliana na mionzi ya jua, kukabiliana na vijidudu mbalimbali kama bacteria na virusi na kutizamia joto la mwili. Ngozi hujijenga wakati mwili umepumzika ili kuweza kuendelea kuchunga mwili wa mwanadamu ipasavyo.

Acha kujichubua
Kutumbua chunusi na vipele ni tabia tulio nayo sisi wanadamu. Mara nyingi matokeo yake huwa ni kuwa na makovu na wekundu. Kufanya hivi pia huchangia bakteria kusambaa na kuharibu ngozi hata katika maeneo ambayo hayakuwa na matatizo.

Japokuwa ni ngumu kutotumbua chunusi, ni vyema ikiwa italazimu ufanye hivyo, tumia kitambaa safi kutoa chunusi na wala sio vidole au kucha kwa sababu ya uchafu uliopo kwenye kucha na vidole. Yaani hatuwezi kuamini mikono yetu kwa asilimia 100.

Ukiwa na chunusi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya ya ngozi ili akupe tiba ya uhakika.

Usafi kwanza
Osha uso wako. Watu wengi hukimbilia kuosha nyuso zao haraka haraka na sio vizuri kusafisha uso juu juu kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa uchafu kubaki, hasa wanawake ambao wanatakiwa kutambua umuhimu wa nyuso zao. Basi ni bora ukatenga muda wa kutosha katika kuosha na kutunza uso.

Kusafisha uso mara zisizopungua mbili kwa siku ni vizuri kwa utunzaji wa ngozi yako ya uso.

Baada ya kufanya hivyo ni muhimu upake mafuta kiasi. Mafuta ni kwa ajili ya kulainisha na kung’arisha ngozi. Hata ijapokuwa una ngozi ya mafuta mengi, ni vizuri kutafuta mafuta ya ngozi yako.

Tunza vizuri macho yako
Watu wengi hupaka kiasi kidogo cha mafuta chini ya macho bila kujua faida tunazoziacha kwa kutokufanya hivyo.Kuna mistari (mikunjo) ambayo inaanzia kwenye jicho na ambayo muda mwingine husogea hadi kwenye maeneo ya karibu na nywele. Paka mafuta ya kutosha chini ya macho. Aidha, fanya ni kama unajimasaji kuanzia kwenye kona karibu na pua mpaka kwenye mfupa wa shavuni (cheekbone) kuzunguka jicho lote.

Barafu
Barafu ni moja kati ya vitu muhimu katika kutunza ngozi. Licha ya upatikanaji rahisi pia ina uwezo wa kutunza ngozi yako bila gharama.

Faida za kutumia barafu katika utunzaji wa ngozi yako ni kwamba; Ukiumia au kujichuna kwenye ngozi waweza kutumia barafu kupunguza wekundu na kupunguza mwasho katika eneo lile.

Sote tunajua unapochubuka au kuumia kuna mwasho ambao tunahisi katika eneo lile la jeraha. Ukitumia barafu itakusaidia. Pia barafu unaweza ukaitumia kupunguza ukubwa wa matundu katika ngozi hasa pale mtu alikuwa amekamua chunusi.

Barafu husaidia kuvuta ngozi ili isiwe imeacha matundu ambayo muda mwingine hayapendezi kuonekana. Ila kumbuka wakati wa kutumia barafu zungusha maeneo tofauti kwasababu huunguza pale inapoachwa sehemu moja. Pia ni vizuri kuweka aloevera katika maji utakayo gandisha kwa ajili ya barafu (hiari yako).

Tumia mafuta yanayofaa ngozi yako
Moja kati ya njia za kutapa ngozi laini na nyororo ni kutumia mafuta ambayo yametengenezwa kwaajili ya kupaka kwenye ngozi na sio ya nywele au ya kupikia.

Kutumia mafuta ya ngozi husaidia kung’arisha ngozi na muonekano mzuri ambao sio wa mafuta. Mafuta ya ngozi hayazibi vinyweleo vya ngozi, hivyo huruhusu ngozi kupumua na kutoa taka mwili kupitia vitundu hivyo na yanasaidia kupunguza uzajishaji wa mafuta katika uso hasa kwa wale wenye ngozi za mafuta.

Kumbuka kupaka mafuta mara mbili kwa siku katika uso safi; yaani baada ya kusafisha uso vizuri ndipo unashauriwa upake mafuta. Ukizingatia hilo utaona mabadiliko katika ngozi yako.

Sunscreen
Kwa wale wenye matatizo ya kuungua wakiwa kwenye jua asubuhi, ni muhimu wawe wakipaka mafuta ya kuzuia mionzi ya jua (sunscreen) inayopenya kwenye ngozi na kuharibu ngozi yako. Na pale unapokuwa nje, hakikisha unajizuia na jua kwanzia mavazi yako; vaa miwani ya kuzuia miale mikali ya jua na kofia pana inayozuia jua kupiga usoni.

Kwa wale ambao ngozi zao zimepata madhara ya vipodozi wanashauriwa kuacha mara moja kutumia vipodozi vilivyowapatia madhara na kumuona mtaalam wa afya ya ngozi ili aweze kuwashauri pia wapate matibabu.

Njia za asili za kutunza ngozi na kufanya usafi wa ngozi
  • Andaa maji safi yenye joto kiasi unachomudu katika ngozi yako, osha uso wako kwa hayo maji safi.
  • Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake yale maji yake usoni, kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake. Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya matunda usoni kwa mtindo wa kusafisha taratibu usoni.
  • Chukua machicha ya nazi na anza kuusugua uso na shingoni taratibu mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang'aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi. Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong'aa bila vitu vyeupe yaani machicha.
  • Chukua kiini cha yai inapendeza ukitumia la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea angalau. Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine katika chombo mithili ya sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando. Paka ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.
  • Baada ya kupaka kiini cha yai unaweza kuendelea na shughuli zako huku likiendelea kukauka,linapokauka ngozi yako inakuwa kama inajivuta vuta.
  • Baada ya kule kuvuta kuisha inamaanisha yai limekauka kabisa. Osha uso wako kwa maji safi maji yawe ya baridi sasa.
Njia hii ya asili inavyofanya kazi
  • Kuosha uso kwa maji yenye joto kunafungua matundu ya ngozi.
  • Tango au limao hutumika kama cleaner, unapokuja kujifuta taratibu unaondoa uchafu katika ngozi yako.
  • Machicha ya nazi yanatumika kama scrub, yanaondoa seli zilizokufa, kuifanya ngozi kuwa laini na kuipa mng'ao.
  • Kiini cha yai hapa kinatumika kama maski, matundu ya ngozi yanajifunga vizuri na kinaipa ngozi yako lishe kutokana na vitamins zilizomo kwenye kiini cha yai kama vitamin E.
  • Mwishoni unanawa na maji baridi ili kuruhusu matundu ya ngozi kujifunga na kuifanya ngozi ijiweke sawasawa.
Faida ya njia hii ya asili
  1. Husaidia kutibu na kuikinga ngozi na chunusi.
  2. Kuipa ngozi mng'ao bila kutumia kemikali za sumu.
  3. Husaidia kupunguza mikunjo katika ngozi yako.
  4. Gharama ndogo kuifanya.
Mdau anaehitaji kujua jinsi ya kutunza ngozi
Wakuu tujuzane kuhusu utunzaji wa ngozi zetu.

Kiukweli ukiwa na ngozi nzuri laini/soft inapendeza na inavutia hasa usoni haijalishi ni ke or me. Na zipo njia tofauti za utunzaji wa ngozi na kila mtu ana aina yake ya utunzaji wa ngozi either kutokana na bidhaa anazotumia nikimaanisha lotion, mafuta, sabuni, scrub na vitu vingine.

Hebu tujuzane hapa wakuu unatumia nini kutunza ngozi yako? Kuhakikisha ngozi yako inavutia unakuwa na rangi moja, soft/laini

MB: Ngozi ya mwili nzima
.,.......

Michango ya wadau

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
----
Tafuta mafuta ya sunscreen..huwa yana kitu kinaitwa sun protective factor-SPF yenye namba.kwa mfano spf 26 inamaanisha ili kudhurika na mionnzi ya jua inatakiwa iwe mara 26 zaidi ya kiwango chake cha kawaida..Ila mi vyema umtafute daktari wa ngozi akushauri zaidi.

Ila kama utatumia hayo mafuta kumbuka kutafuta other sources of vitamin D..jua lina umuhimu wake katika kuhakikisha tunapata viyamini hivyo muhimu kwa kuimarisha mifupa yetu.
----
Nilikua napaka parachute mwili mzima nlikuwa na rangi yangu nzuri tu nkahamia kwenye botour nikawa mweupe nikaiacha nkapaka american dream promo nyingii ila ya kawaida labd haikunipenda ila niliona ya kawiada sana rafk ang mmoja akanishaur kupaka clinik clear nachangya na glycel ya kopo lile la njano nkamuona huyu shoga vp kwa nn asipake yeye akasema wenye ngz kam yang maji ya kunde ndo inawapendeza sana kaona watu km 3 ofsn kwao wametumia wana rangi nzur mnooo nkabisha akaninunulia mwenyew gharama yake ni kama elf 10 tu nkachkua nkaanza kupaka ivo ivo yan uku naogpa san mara rangi inanoga aisee nimekuwa mzur rangi ya chocolote sas iv nimeshtmia km kopo 3 :D alf very cheap
 
Tafuta mafuta ya sunscreen..huwa yana kitu kinaitwa sun protective factor-SPF yenye namba.kwa mfano spf 26 inamaanisha ili kudhurika na mionnzi ya jua inatakiwa iwe mara 26 zaidi ya kiwango chake cha kawaida..Ila mi vyema umtafute daktari wa ngozi akushauri zaidi.

Ila kama utatumia hayo mafuta kumbuka kutafuta other sources of vitamin D..jua lina umuhimu wake katika kuhakikisha tunapata viyamini hivyo muhimu kwa kuimarisha mifupa yetu.
 
tafuta mafuta ya sunscreen..huwa yana kitu kinaitwa sun protective factor-SPF yenye namba.kwa mfano spf 26 inamaanisha ili kudhurika na mionnzi ya jua inatakiwa iwe mara 26 zaidi ya kiwango chake cha kawaida..
ila mi vyema umtafute daktari wa ngozi akushauri zaidi..
ila kama utatumia hayo mafuta kumbuka kutafuta other
sources of vitamin D..jua lina umuhimu wake katika kuhakikisha tunapata viyamini hivyo muhimu kwa kuimarisha mifupa yetu
Ni muda gani sahihi kutumia.,?
 
Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.
Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:
• Kuridhi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Vidonge vya kuzuia mimba.
• Baadhi ya vipodozi .
• Hali ya unyevu (humidity) na hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta
Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-
1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.
2. Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.
3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipotze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.
4. Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.
5. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.
6. Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.
7. Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.
8. Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.
 
Wakuu tujuzane kuhusu utunzaji wa ngozi zetu.

Kiukweli ukiwa na ngozi nzuri laini/soft inapendeza na inavutia hasa usoni haijalishi ni ke or me. Na zipo njia tofauti za utunzaji wa ngozi na kila mtu ana aina yake ya utunzaji wa ngozi either kutokana na bidhaa anazotumia nikimaanisha lotion, mafuta, sabuni, scrub na vitu vingine.

Hebu tujuzane hapa wakuu unatumia nini kutunza ngozi yako? Kuhakikisha ngozi yako inavutia unakuwa na rangi moja, soft/laini

MB: Ngozi ya mwili nzima
.,.......
 
Mwanzoni nilikuwa napata tabu chunusi ndio ugonjwa wangu, Kuna mmama nilikutana naye akanisidia sielew kitu gani kile ila anadai anachanganya mayai, kitunguu na asali na paka mwili mzima jamani nimekuwa laini mpaka najitamani chunusi , kwarara zote hamna. Sabuni natumia ya jorjous .
 
Back
Top Bottom