Utundu ni dalili kuwa mtoto ana akili?

STALLEY

JF-Expert Member
May 5, 2012
619
206
Jamaa mmoja alikuwa anamsifu mtoto wake kuwa ana akili sababu anaharibu sana vitu nyumbani yani haipiti siku mbili lazima avunje chombo au aharibu remote control.alipoulizwa kama hiyo ni akili au ujinga akajibu ni akili kwa sababu mtoto asiyekuwa na akili hawezi kushika remote control sababu hawezi kuitumia.je jamaa yuko sahihi kuwa mtoto akiwa anaharibu haribu vitu nyumbani ni kigezo kuwa ana akili
 
Kitu chochote mkuu , kinatakiwa kiwe kati kwa kati.
Suala la mtoto kua mtundu wa kukithirisha, kwa sura hiyo mtoto husika hatokua na sifa ya kua na akili, bali atabaki na sifa ya muharibifu, ambapo hilo ni tatizo.
Na mtoto akiwa mtulivu, ule utulivu wa kukithiri napo ni tatizo atakua mzubaifu.
Mtoto mahiri hua na sura au miondoko ya kati na kati .
 
Jamaa mmoja alikuwa anamsifu mtoto wake kuwa ana akili sababu anaharibu sana vitu nyumbani yani haipiti siku mbili lazima avunje chombo au aharibu remote control.alipoulizwa kama hiyo ni akili au ujinga akajibu ni akili kwa sababu mtoto asiyekuwa na akili hawezi kushika remote control sababu hawezi kuitumia.je jamaa yuko sahihi kuwa mtoto akiwa anaharibu haribu vitu nyumbani ni kigezo kuwa ana akili

Jamaa alikuwa sahihi kabisa...tatizo ni jinsi ulivotunga swali lako. Unaweza kutujuza umri wa mtoto na kutofautisha kuharibu kwa makusudi na kuharibu kwa bahati mbaya yaani in the process ya kujifunza? Binafsi siamini kama mtoto anayezungumziwa ni yaule anayeamka na kuoina TV na kusikuma, au kubamiza remote ukutani. Naomba mwongozo.
 
m
Mo, you hv written and spoken my thoughts. Intelligent thought; thank u.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom