Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Kwamba Maaskofu hawapaswi kuongelea mambo yanayohusu siasa au viongozi wa kisiasa ni ufinyu wa mawazo na kutokujua hakika utume wa viongozi wa kidini na hata historia yake.
Mtume Mohammed (SA) alihubiri juu ya Mola Mmoja & Haki na Wakureshi (Quarash) na Viongozi wao waliokuwa wanafahidika na mfumo huo mbovu hawakumpenda kwa kuona kuwa anawaingilia. Hii ikasababibsha hadi kumfukuza Mtume toka Macca akaishi na familia yake ukimbizini katika milima ya Shobe Abu Talibu. Kudai & kutenda haki ni kusudi mojawapo kuu la dini Islam. Mungu hutuamuru kutenda haki (Quran 16:90), Hakika Wanaohubiri ni Mitume wa kujenga Haki miongoni mwa jamii. We sent Our Messengers with clear signs and sent down with them the Book and the Measure in order to establish justice among the people (Quran 57:25).
Kwamba, kwa ajili ya yenu (Wakristo) wamepewa, Yesu ambaye ni Mshauri wa ajabu na pia Bwana wa Amani (Isaya 9:6). Na hakika Mitume na Manabii wengi sana akina Hosea, Hagai, Amos, Isaya, Paulo nk walisimamia haki na kuisema kweli popote hata dhidi ya Watawala. Yohana Mbatizaji alitupwa gerezani na hata baadaye kukatwa kichwa zawadi iliyoombwa na mama Herodia kupitia binti wake kwa sababu alionekana mwiba juu ya ndoa batiri ya Herode Antipas. Isaya msahauri wa Wafalme kufuatana na masimulizi ya mapokeo ya Wayahudi, aliuawa wakati wa utawala wa mfalme mwovu Manase kwa njia ya kukatwa vipande viwili kwa msumeno (taz.Ebr 11:37).
Kama kuisema na kuitetea KWELI na kuonya juu ya MAOVU au KUTOTENDWA KWA HAKI mahala fulani ndiko kunaitwa kuingia katika Siasa au kuingilia Wanasiasa, basi hata Waasisi wa dini hizo na nyinginezo kama vile Yesu Kristo, Mtume Mohammed (SA) na karibu Mitume na Manabii wote walikuwa Wanasiasa!
Hebu pata Facts:
ii. Kwa wale wasiounga mkono Utume wa kuikabiri kweli kwa nguvu zote, yaani ni wale ambao watapenda kuliita koleo, kijiko kikubwa wangependa Maaskofu waseme tu kuwa Kuna mgogoro katika Manispaa ya Arusha uliotokana na uchaguzi wa meya na hivyo vyombo husika vilisimamie jambo hilo pasi kupoteza muda. Mtizamo wao huwa ni kujaribu kuepuka kuamsha hisia na hasira za watu na hatimaye kuibuka kwa migogoro katika jamii; (ingawa ukweli unaweza kuwa ukazuia mgogoro kwa muda mfupi lakini baadaye hata baada ya miaka kukazuka migogoro mikubwa zaidi ya visasi ambayo chanzo chake ni Utume wa kuepuka mgogoro wa leo!). Aidha pia kundi hili laweza kuwa ni wale pia wanaoona kuwa Maaskofu hawana kazi ya kuwatambua au kutowatambua Viongozi waliochaguliwa bali Tume za Chaguzi na au Mahakama.
Popote unapoosimamia kuhusu hili, binafsi nasema kuwa Maaskofu walivyotamka kuhusu Meya, ni maoni yao katika uchache / wingi wao baada ya uchambuzi wao. Sasa chombo kinachohusika kiteremke Arusha kiitishe uchaguzi huo halafu tuone matokeo yake na watakao chaguliwa wawe Meya na Msaidiazi wake! Na hapo turudi katika jukwaa hili katika mada hii ili tukamilishe hitimisho.

- Ni wajibu wao Maaskofu kama sehemu ya jamii (Civil Society) na pia kama Viongozi wanaohubiri na kusimamia haki (bila jeshi) ya Waasisi wao, Maaskofu kulaani na kutoa pole kwa mauaji yaliyotekea Arusha hivi karibuni.
- Hao Maaskofu walioongea ni sehemu ndogo sana ya Maaskofu au tuseme Viongozi wa Madhehebu ya Kikristo Tanzania. Kuna Madhehebu kibao ambayo hayako chini ya TEC wala CCT. Na hata leo tungepitisha survey najua wako wengi tu (hata ndani ya TEC & CCT) ambao wangepinga au kubeza au kulaani walichokifanya hao Maaskofu! Na ndivyo ilivyotokea hata wakati wa Mauaji ya Mwembe-Chai, si wote walikaa kimya au sema si wote walilaani mauaji yale! Ni uzembe wa kufikiri kulaani dini yote ya Kikristo au Kiislam kwa wachache kuwa kimya au wachache kuongea.
- Suala la Maaskofu kutomtambua Meya wa Arusha lina mitamo miwili: