Utulivu na amani bila maisha bora kwa mtanzania ni ndoto za alinacha

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kila mtu ndani ya nchi yetu ana imba amani na utulivu.Rais anahubiri amani na utulivu,viongozi wa dini nao halikadhalika.Nikweli amani ni tunda la rehema lililosheheni utulivu upendo na uvumilivu.Ikitokea amani na utulivu ukavurugwa basi hali tete huikumba nchi ama jamii husika.

Tangu kuumbwa kwa nchi yetu tumekuwa waaumini wa kuhubiri amani kwa kipindi kirefu.Lakini cha ajabu leo hii amani tuliyoiimba kwa miaka mingi imetoweka ,kutoweka kwake kuna changiwa na wananchi kukata tamaa kutokana na ugumu wa maisha unaosababishwa na hali ngumu ya uchumi wetu.

Imekuwa ni kawaida kusikia takwimu za kukua kwa uchumi,lakini si kwa mwananchi mmoja mmoja.Mfumuko wa bei umelikumba taifa letu tangu tuingie awamau hii ya nne bila kupatiwa tiba mjarabu.Bwana mmoja aliwahi kubeza kwa kusema kiongozi wa uganda aliwahi kwenda kwa mganga kutafuta tiba mbadala kwa matatizo ya nchi yake na watu wake,alipomaliza kujieleza mbele ya mganga,yule kiongozi alidondoka akazimia,alipozinduka mganga akamwambia chukua dawa ya matatizo yenu nenda.Alipofika Uganda matatizo yale yalikwisha na uchumi wake ukakuwa kwa kasi kubwa.Alipoondoka tu Mkenya naye akaingia kwa shida ile ile naye akapatiwa tiba,matatizo yao yakaisha.Ilipofika zao ya Watanzania kuelezea matatizo ghafla mganga akadondoka na kufa papo hapo, kiasi cha kupelekea kukosa huduma hiyo ambayo imepelekea mpaka leo hii kukosa tiba mjarabu ya matatizo yetu.

Kisa hiki kinadhihirisha ni aina gani ya matatizo yaliyo likumba taifa letu na kukosa tiba mbadala wa uchumi wetu.Pengo la kipato kati ya maskini na tajiri linaongezeka kila kukicha.Rais wa nchi aliwahi kutumia kigezo cha wingi wa magari DSM kama kigezo cha uchumi wa nchi kukua na kusahau kama kuna watu wanaishi kwa kula mlo mmoja tena wa kubahatisha kwa siku.

Si kweli nchi yetu haina madaktari wa uchumi,la hasha wengi wao wanatumiwa na mataifa mengine kama washauri wa mambo ya uchumi katika nchi hizo ilihali nchini mwetu wananyimwa fursa hizo kwa makusudi kabisa.Hali kama hii ikiachiwa ikaendelea Tanzania itakuwa kiwanda cha kuzalisha omba omba na taifa fukara kuliko mataifa yote ulimwenguni ilhali tukiwa na rasilimali ambazo tumegawa sadaka kwa wageni kwa maslahi yao na ten percent kwa watawala wetu.

Siku zote mwenye njaa huwa hana nidhamu,na nidhamu ya nchi hii itazidi kuvunjika mpaka pale Serikali itakapoweza kuwajali watu wake kwa kuwatengenezea uchumi endelevu wenye kuleta tija kwa kila Mtanzania.Ni hatari iliyoje leo hii ndani ya nchi yetu wawekezaji wanaajiri mpaka wageni toka nje ya nchi kwa kazi za ulinzi ,wakati vijana wetu wanamaliza bora elimu kila kukicha.Bomu hili la vijana waliokosa elimu bora na ajira siku likilipuka watu watatafutana.

Mfumuko huu wa bei na anguko la uchumi ni kigezo kikubwa cha kutuingiza katika uvunjivu wa amani kutokana na matabaka yanayojengwa na watawala katika ya wenye nacho na wasio nacho.Wananchi wananyang'anywa ardhi na kugawiwa wageni huku wao wakigeuka kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao kwa kulala kwenye mahema ilihali walikuwa na maisha yao mazuri, lakini hali imebadilika kutokana na sera mbovu ndani ya nchi.Kwa mantiki hii utulivu na amani bila maisha bora kwa Mtanzania itakuwa ni ndoto za kufikirika.


Mwisho, serikali iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa kuliko kujinadi wao ndiyo chimbuko la amani iliyoko hapa nchini na kusahau wamechangia kiasi kikubwa kuvurugika kwa amani kutokana na sera zao za kugawana mali na kuchukua chao bado mapema kwa faida zao binafsi na familia zao.Ipo siku majuto atageuka mjukuu,wakati nao utakuwa umekwisha wa kubembelezana.
 
Back
Top Bottom