Utu na umuhimu wa kuripoti

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52

Wiki hii Mkuu wa Mkoa wetu wa Pwani Hajjat Mwantumu Mahiza alizungumza na waandishi wa habari na kuelezea masikitiko yake kwa binaadamu ambao wamekuwa wakitanguliza sifa na maslahi binafsi badla ya utu pale wanaposhughulikia majanga mbalimbali ikiwemo ajali.

Hajjat Mahiza ametoa kilio chake kutoka na kuwa mkoa wetu wa Pwani umekuwa ni muhanga wa matukio mbalimbali

ya ajali ambapo wanaofika eneo la ajali badala ya kushirikiana kuwasaidia wahanga au manusura wa ajali basi watu hufanya vitendo vya uhalifu kama kuwahi kuiba MALI au 'ngawira', na wengine kujihusisha na kuchukua PICHA za tukio zinazoonesha hali ya mambo ili waziuze kwenye vyombo vya habari.

Tabia hii imeota mizizi siku hizi ambako maendeleo yamekuwa makubwa katika kupashana taarifa. Bi Mwantum Mahiza ametoa wito kwa watanzania kuacha tabia hizo na badala yake wajenge tabia ya kutanguliza UTU kuwasaidia wanaokutwa na matatizo.
 
Back
Top Bottom