Kiraka Kikuu
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 5,904
- 1,976
- Thread starter
- #41
Tuliambiwa na kaka yetu kuwa ukitaja nyoka usipotema mate na kusema "Mungu pishia mbali sio mimi niliyesema ni mchawi" nyoka atatokea na kukung'ata. Basi kaka yetu mkubwa akawa anatutesa kweli mimi na mdogo wangu. Anakuja mbele yetu na kusema nyoka, nyoka, nyoka mara nyingi tu. Sisi kwa ajili ya imani kuwa nyoka atatokea tulikuwa tukitema mate na kusema hayo maneno hapo juu. Kwa kila mtajo mmoja wa nyoka tulikuwa tukitema mate na kusema hayo maneno. Basi kaka yetu anaweza kutamka hilo neno mfululizo hata mara 50. Tulitema mate hadi yanakauka mwisho tunalia na kumkimbilia mama tukidai kaka anatuchokoza, anataka nyoka waje. Utoto jamani! Lakini natamani nirudie utoto mie!
Nyinyi nanyi mlizidisha!!!!LOL!!!!