Utoro bungeni muda wa jioni.

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
793
101
Ukitazama Bunge wakati wa asubuhi maudhurio ya wabunge yanakuwa juu sana ila wanaporudi jioni Maudhurio yanashuka sana yaani hata Robo ya Wabunge hawarejei kikao cha jioni hii ndo inatudhihirishia Wabunge Wetu wapo Kiposho zaidi coz washasaini tu ile asubuhi imetoka.Nafahamu kuna wenye dharura ila haiwezekani kati ya Wabunge 300 na ushehe kikao cha jioni wabunge hawatimii 50.
 
Jaribu kuchunguza tujue ni wabunge wa chama gani ambao wanaongoza kwa kutoroka.
hivi lile tatizo la kusinzia bungeni hivi sasa lipo tena??
nina mda sijalisikia, au wanaogopa siku hizi!? maana sis wananch kama tutawakilishwa kwa usingiz na sis tutalala.
 
Ukitazama Bunge wakati wa asubuhi maudhurio ya wabunge yanakuwa juu sana ila wanaporudi jioni Maudhurio yanashuka sana yaani hata Robo ya Wabunge hawarejei kikao cha jioni hii ndo inatudhihirishia Wabunge Wetu wapo Kiposho zaidi coz washasaini tu ile asubuhi imetoka.Nafahamu kuna wenye dharura ila haiwezekani kati ya Wabunge 300 na ushehe kikao cha jioni wabunge hawatimii 50.

Hili halihitaji hata elimu ya ndumbaru kufahamu ni kwa nini. Asubuhi wanakuwa tayari wameshasaini daftari la mahudhurio hivyo kujihakikishia POSHO na kwa kuwa ndicho kilichowapeleka Bungeni, hawana haja ya kuonekana tena humo jioni isipokuwa wale wazalendo wa wachache wanaojua kilichowapeleka mle na wanafiki wachache pia.
 
hii ndo tanzania wabunge we2 wapo kimaslahi zaidi na jioni c ndo muda wa kwenye viti virefu
 
Aise sijaelewa vizuri hivi zile sitting allowance ni Asubuhi na jioni au per single signature?
 
muda huo nyama na bia pale chakonichako zinakuwa mwakemwake asa warudi kufanyaje
tena khaaaaaa
 
Yule Mbunge wa Chato huwa namwona Njia panda ya Airport anamendea kuku wa supu ya kienyeji
 
Yule Mbunge wa Chato huwa namwona Njia panda ya Airport Dodoma anamendea kuku wa supu ya kienyeji
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom