taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,095
- 538
Kitendo cha hao madaktari kukubali kushiriki katika utoaji wa mimba hizo inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vitendo vya ngono zembe hususan kwa wanafunzi. Jambo la msingi ni kwa madaktari hao kutambua kuwa jambo wanalofanya ni dhambi kulingana mafundisho ya dini na kinyume na maadili ya Mtanzania na mbaya zaidi wanashiriki kuua viumbe visivyo na hatia.
Kama watakataa kutoa mimba hizo hiyo itatoa fundisho kwa wote wanaoamini kuwa pindi mimba ikinasa nitakwenda kutoa. Jamii pia inatakiwa kuangalia jambo hili kwa upana zaidi na Serikali kuingilia kati kwa kufanya ufuatiliaji wa kina na kutoa adhabu kali kwa wale wanaoshiriki kwenye shughuli hiyo. Inasikitisha sana kusikia kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanatoa mimba zaidi ya nne kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Ni vyema pia wanafunzi hao wakatambua kuwa hatari kubwa inayowakabili mbele yao ni kukosa uzazi kabisa kwa kipindi cha maisha na kuwa "KAMA MIMBA WANATOA, UKIMWI WATATOLEA WAPI?"