Utoaji maoni ya katiba mpya makete.

Kuna mtu form two drop out amependekeza chuo kikuu kuwe na tume ya kutunga na kusahihisha mitihani ili kukwepa degree za chupi!
 
Kuna watu wamechokonoa kuhusu machinjio. Wanataka wachinjaji wasihusishwe na mambo ya dini fulani. Mtu yeyote achinje na kuuza nyama bila kusubiri muislamu kuchinja. Swali: hivi nani aliweka huu utaratibu uliopo sasa hivi?
 
Kuna pendekezo la vikao vya bunge viwe vinarotate kati ya dodoma na zanzibar. Hii ngumu kumesa aisee! Duh! Hivi kina malima watakubali kwenda kukaa sehemu ambayo totozi wanajifunika kwote?
 
Naona polisi wamenangwa hapa kuhusu kuwa wakamataji, mahakimu na wauaji wao wenyewe. Kuna polisi hapa jirani yangu amestuka!
 
Wadada na wamama inaonekana wanaogopa kutoa maoni maana mpaka sasa watu zaidi ya hamsini wametoa maoni ni wanawake 6 tu ndio waliojitokeza. Hawa ndio wanapigania haki sawa kweli! Na wanautaka urais kupitia migongo ya wananchi.
 
Naona wanataka kumaliza mkutano maana wanaonyeshana ishara za watu wawili tu ndo waongezeke. Madaraka ya rais kila mchangiaji anahoji na kutaka yapunguzwe. Kuna hoja ya wafanyakazi wote wenye elimu sawa mfano degree wapewe mshahara sawa regardless of aina ya kozi anayoisomea. El mamry anamuuliza kama wanasoma miaka tofauti ni kwanini walipwe sawa? Dogo anajibu kwamba basi at least wawe wanapishana kidogo. Mf m1 akilipwa m1 mwingine alipwe laki nane.
 
Duh aise charge yangu inaelekea mwisho, lakini na maoni yanaelekea mwisho na maoni yanayotolewa muda huu yanarudiwa yaliyoongelewa mwanzo
 
Kulikuwa na maoni pia ya ardhi iwe mali ya kijiji na wananchi wa kijiji husika na kama matumizi yakibadilishwa basi wananchi wakubali kutoa idhini hiyo. Kuna daktari hapa kaongelea kwamba huduma za afya ziwekwe kwenye katiba na iwe ni haki ya msingi na serikali iwe na jukumu la kuratibu huduma zote zitolewazo nchini. Pia kazungumzia kwamba mbunge akifa au kuvuliwa ubunge basi aliyemfuata kwenye uchaguzi mkuu kama kura zake zilifikia nusu ya mbunge ndiye apewe ubunge.
 
Suala la uchinjaji nyama naona limepamba moto, watu wanasema kila mtu anamwabudu Mungu wake hivyo hakuna kulazimishana kwenye mambo ya imani. Waislam kama hawataki basi wafungue bucha zao na wakristo nao wawe na za kwao. Kama vipi huu utaratibu ufutwe.
 
Suala la uchinjaji nyama naona limepamba moto, watu wanasema kila mtu anamwabudu Mungu wake hivyo hakuna kulazimishana kwenye mambo ya imani. Waislam kama hawataki basi wafungue bucha zao na wakristo nao wawe na za kwao. Kama vipi huu utaratibu ufutwe.

Mwalemi sana binamu kuvosungilo kokonyumba.? Endelea kutuwakilisha pamoja sana
 
Back
Top Bottom