Utoaji maoni ya katiba mpya makete.

usungilo

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
522
331
Wajumbe wamewasili hapa iwawa na shangingi tatu. Wanafanya maandalizi ya mawasiliano
 
Mwenyekiti wa kijiji anafungua mkutano na kukaribisha utambulisho wa msafara
 
Mwenyekiti ni salama ahmed, kuna el mamry, na Nasoro khamis. Sekretariati ni andrew,fadhila, othman na wengineo. Mwenyekiti anatoa ufafanuzi wa kazi zao. Anaelezea mchakato ulivyoanza mpaka sasa. Anaeleza kwamba kila mtu yuko huru kutoa maoni kwani analindwa na sheria
 
Anawaelekeza wananchi watoe maoni yatakayotoa na solution ya yale wasiyoyataka
 
Katiba ifuate utakatifu wa ndoa ya mme mmoja na mke mmoja. Na mipango iwe inaanzia kwa wananchi na sio kutoka juu
 
Kuna pendekezo wa viti maalumu vifutwe, vinginevyo na vya wanaume viwekwe ili kuweka haki sawa
 
Madaraka ya rais kila anayekuja analizungumzia kuhusu kupunguzwa. Kila mwananchi amekerwa na namna jk alivyozitumia weakness za katiba hii kunufaisha familia na rafiki zake
 
Kuna mtu kawananga wakuu wa wilaya mpaka wajumbe wa tume wametikisa vichwa kumkubali. Pia mkuu wa mkoa ni lazima wachaguliwe na wananchi.
 
Aisee, nimegundua wananchi wanajua vitu vingi kuliko inavyodhaniwa. Wanafunguka kama kuna mtu kawakaririsha. Kuna oni la viongozi washitakiwe baada ya kutoka madarakani. Pia yoyote anayetoa ahadi za uongo wakati wa kampeni washtakiwe ili watu wasiwe wanaongea uongo hadharani. Mwenge, mwenge jamani! Wananchi wamechoka nao na uzinzi unaofanyika. Watu wanataka uwekwe museums
 
Back
Top Bottom