Utiifu... mapenzi ama ??

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,063
22,755
Watu watatu walituma maombi ya kazi usalama wa taifa. Wa kwanza alikuwa kijana wa miaka 25, wa pili alikuwa na miaka 35 na wa tatu alikuwa na miaka 45. Wote wakaitwa kwenye usaili wa utiifu na wakatakiwa kufika na wake zao na wakawa wanaitwa moja moja huku wake zao wakiwa wamewekwa vyumba tofauti.

Wa kwanza (25) akaitwa ndani na kupewa bastola akitakiwa kwenda aliko mkewe na kumpiga risasi. Kijana wa watu akaondoka lakini baada ya dakika zisizozidi 5 akarudi na kusema hakuweza kufanya hivyo kwa sababu bado anampenda sana mkewe.

Wa pili (35) akaingia ndani na kupewa maagizo kama yale yale. Huyu alichukua muda kidogo na baada ya dakika 15 akarudi na kusema hakuweza kumwua mkewe kwa sababu anawapenda sana watoto wake na bado wanaomhitaji mama yao.

Wa tatu (45) kupewa tu bastola akatoka na haikuchukua muda, mlio wa risasi ukasikika ukifwatiwa na vurumai kutoka chumbani aliko mkewe. Mlango kufunguliwa akakutwa jamaa kasimama na mbele yake kuna maiti ya mkewe. Kwa mshangao akaulizwa kafanya nini. Jamaa huku akihema akafoka, " Kuna mshenzi moja kaweka risasi bandia (blanks) na hivyo imebidi nimmalize kwa kumnyonga."
 
Du! Jamaa alimchoka mkewe kiasi hicho!!!

Laiti tungekuwa na hasira na CCM kama huyo jamaa...miaka 45 na bado hatuna ujasiri wa kuitokomeza !! Leaves one wondering ama ndiyo kulogwa ?
 
Haya ndiyo maisha. mapenzi motomoto kabla hamjawa na watoto, mtoto wa kwanza tu mapenzi yote yanahamia kwa mtoto. Baada ya watoto wawili hata kutoka na my wife wako hutaki, kisingizio watoto watabakia na nani nyumbani. Huko kwenye miaka 45 si ndo kabisa hatakiwi tena maana na mama naye anajua hana pa kwenda! Jeuri full mzuka.
Dah, lakini jamaa hakakumwingia hata ka-huruma kimtindo akakumbuka japo katendo kamoja kalikomfurahisha katika maisha yao?
 
Duh, hiyo ilikuwa kali..kumtoa roho mkewe! ni kweli kwa umri huo wanaume wengi huwa wanavurugana sana na wake zao. Ila cha ajabu kama huyo bwana angefikisaha miaka kuanzia 70 hivi asingethubutu, mapenzi huwa yanarudi tena uzeeni, tena huwa ya hali ya juu mno! Sijui inakuwaje!?
 
Laiti tungekuwa na hasira na CCM kama huyo jamaa...miaka 45 na bado hatuna ujasiri wa kuitokomeza !! Leaves one wondering ama ndiyo kulogwa ?

Mkuu unaona mbali!Kuna kila sababu ya kijapanga upya.
 
Duh, hiyo ilikuwa kali..kumtoa roho mkewe! ni kweli kwa umri huo wanaume wengi huwa wanavurugana sana na wake zao. Ila cha ajabu kama huyo bwana angefikisaha miaka kuanzia 70 hivi asingethubutu, mapenzi huwa yanarudi tena uzeeni, tena huwa ya hali ya juu mno! Sijui inakuwaje!?

Hii husababishwa na Kuwa kipindi hiki watoto wote ni watu wazima na wameshasambaa kujitafutia rizk so wanarudi kwa ile age ya 25 mtu bee ndo hamna tena excuse za watoto
 
Back
Top Bottom