Utii wa sheria bila shurti

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
ANZA WEWE!!!!!
Wajameni, siku za hivi karibuni serikali kupitia jeshi lake la polisi imeanzisha slogan ya kuwahimiza wananchi juu ya kutii sheria za nchi bila kushurutishwa. Kwa kufikiri kwangu kwa kawaida nikaona labda sheria za nchi hii zimewekwa kwa ajili ya wananchi tu huku tabaka la watawala na vyombo vyao likisamehewa. Kumekuwa na tuhuma nyingi zinazoionyesha serikali au watu wake kuwa wavunja sheria namba moja, mfano;
1. Polisi/usalama wataifa wametuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia sehemu mbalimbali, mf, musoma, songea, igunga , wafanya biashara wa madini, zanzibar baada ya uchaguzi nk nk. Pia vyombo hivyo vimetajwa kuhusika na majaribio kadhaa ya mauaji au kutekwa na kuteswa kwa watu kadhaa , mfano Dr ulimboka, wabunge wa CDM mwanza nk
2. Serikali ndiye mdaiwa sugu wa mashirika kadhaa ya umma mfano TANESCO, DAWASCO, TTCL nk
3. Serikali au watu wake baadhi wanatuhumiwa kuiba na kujilimbikizia mapesa huko benki za ughaibuni
4. watawala wengine ni waongo na wadanganyifu hasa kwa kuwa huku wakijua kuwa wanachoahidi hakitekelezeki hutymia fursa hiyo ya uongo kuwadanganya wananchi ili wawapigie kula na wao kuwa madarakani
5. Raia kadhaa wanadaiwa kubambikiziwa kesi za uongo na polisi. Polisi wengine wana tuhuma za kujihusisha moja kwa moja( au kwa kutumia watu fulani) na ujambazi
6 .Wizi wa raslimali za taifa kama madini, magogo, wanyama pori, vitaru vya uwindaji n.k
7.je kuhusu kutolipia mizigo yao ifikapo bandarini, kukwepa kodi mbalimbali......?
8.
9.
10



nk nk

Cha kushangaza katika tuhuma zote hizo, aidha serikali imeunda tume ( zisizo huru) ili ijichunguze yenyewe au imepotezea kabisa haijali uvunjaji huo wa sheria

SWALI LANGU; BABA KAMA YUKO UCHI NI NANI ATAKAYEWAVIKA NGUO WATOTO WAKE? KAMA WATAWALA NA TAASIS ZAO SIYO WATIIFU WA SHERIA WANATEGEMEA NANI ATII BILA SHURTI?
Nawasilisha!!
 
Back
Top Bottom