Uthibitisho wa Mhe. Lema kuhusu Pinda kuongea uongo Bungeni

Bunge lazima liambiwe kama Pinda muongo au la! Hapa spika ana wakati mgumu.
 
Kwani siku hizi kile kilichoombwa na bunge si ni lazima bunge lielezwe bayana. Spika aseme kama lema au pinda muongo.
 
Wana JF

Naomba tukumbushane Makinda alisema ushaidi wa Mhe Lema utasomwa Bungeni mbona hatuoni dalili au ndio imetoka kiaina vile? tutafika kweli
 
Utasomwa muda gani wako busy wanataka kutwangana kwa kuambiwa ukweli? Ukihoji unaambiwa ukane kauli yako!
 
Hapo kwenye Uongo wa 6 sita kuna mtihani kidogo unaweza kuwa Uongo mwingine tena Mhe. Lema kausema Bungeni, kamtaja Dr Slaa, kuwa ana mke kwani kaishafunga ndoa? Spika anaweza kuitaji Marriage Certificate

Pole; subiri basi spika adai hiyo marriage certicate naye spika adaiwe marriage certificate
 
Hivi ile riport aliyoambiwa Lema aiwasilishe Bungeni kuhusu madai yake kuwa Waziri mkuu amelidanganya bunge ndio hivyo tena?
Na je lema sasa ataruhusiwa kuizungumzia nje ya bunge kama kwenye mikutana anayoenda kulianzisha?
Maana nilimsiki pale NMC Arusha akisema kuwa hata kama wamemvua ubunge na alikuwa na kinga ya kutoshitakiwa kwa kusema waziri mkuu kalidanganya Bunge siku hiyo alisema anarudia kusema kama raia kuwa waziri mkuu kalidanganya bunge na sasa kama vipi wamkamate.
Tuna hamu sana ya kuisikia ile riport na tunajua kwa hali ilivyo ilikuwa vigumu sana kwa riport ile kujadiliwa, na sasa Lema wamemngoa je inawezeka ni sababu ya kuizima hiyo riport kama ndio sisi wananchi tutajuaje ukweli kama Lema alilidandanya bunge au waziri mkuu wetu ndio muongo hii inabidi Lema aichukue kama silaha namba moja ya kukimaliza chama cha mapinduzi ili tujue mbivu na mbichi.

Tujue kama tunaongozwa na waziri tena mkuu mwongo ili atakapokuwa naongea mambo ya serekali tujue tuyachukulie vipi?
 
Hii ni moja ya sababu ya rufaa ya kupinga ubunge wa Lema iliamuliwa kama ilivyotokea last week maana alimuanika Pindisha nje ndani na kuonesha how fool he is?
 
Back
Top Bottom