Uthibitisho wa Mhe. Lema kuhusu Pinda kuongea uongo Bungeni

Hapo kwenye Uongo wa 6 sita kuna mtihani kidogo unaweza kuwa Uongo mwingine tena Mhe. Lema kausema Bungeni, kamtaja Dr Slaa, kuwa hana mke kwani kaishafunga ndoa? Spika anaweza kuitaji Marriage Certificate
Sahihisho:
Huenda hapo kwenye bold ulimaanisha neno.."ana" badala ya uliloandika.."hana", maana umedistort kabisa maana ya nia yako ya msingi!

Lakininapenda nikujibu hoja zako kama ifuatavyo:
1.Hoja ya msingi si ya Dr Slaa kuwa na mke au kufunga ndoa...Hoja ya msingi ya No6.ni madai ya WM kuwa cdm walikaidi amri ya Jeshi lapolisi kutoandamana, na ndio sababu wakakumbana na dola.

2.Kwa sheria ya ndoa (1973?), mtu akikaa continously na mwanamke kwa miezi 3, automatically huyo ni mkewe halali(i may be corrected here)...
Jiulize kesi iliyofunguliwa na yule aliyedai kuwa mume wa mama Slaa imeishia wapi!...utagundua kuwa ccm ni majuha!
 
Asante genekai, nimeusoma na nimeridhika kuwa waziri mkuu alisema uongo, je unategemea nini kwa walio chini yake kama waziri mkuu, anashindwa kuandaa hotuba muhimu kama hiyo na kuishia kusema uwongo. Hiyo ndo serikali ya ccm inayotutawala.
Mkuu, hii nchi nyie acheni tu, juzi tu Mwinyi kajibu kwa kiburi kuwa hawezi kuwajibika kwa makosa ya mabomu ya G'mboto,na bosi waokikwete anaaangalia tu. Iko siku bongo kutakuwa kama Misri tu!
 
Kama Mh. Pinda alisema MAUONGO 10 kwenye kwenye taarifa hiyo moja tu, sijui atakuwa ameyasema mangapi mpaka atakapokuwa ameondoka kwenye huo wadhifa! Li serikali la waongo watupu.
 
Sasa nimeelewa ni kwaniniMakinda hakuruhusu hii kitu isisomwe na akasema swala hili halitarudi bungeni mkutano ujao...........Ingekuwa ni aibu ya mwaka kwa Pinda. Machozi yangemtoka. Kweli CHADEMA ni noma!
 
Itabidi kile kipindi cha maswali kwa PM bungeni kifutwe, maana kinaweza kuleta utata mkubwa huko mbele
 
Nakubali kwamba Chadema kuna watu makini sana, na hili sasa ni fundisho kubwa kwa serikali na vyama vingine.
Mwainisho, upembuzi, nukuru za sheria na viambatanisho vya ushahidi vingeanikwa kama ilivyo pale bungeni mtoto wa mkulima angedhalilika mno, ndio maana ccm wamemweka Makinda ambaye kwa sasa tunampa jina la MAMA FUKIA FUKIA.
Ujuavyo kuna jopo la wanasheria mahiri sana ndani ya chama hiki, na pale mtu akiteleza kidogo kuongea basi kesho yake atalipuliwa.
Inaelekea Mkwere anajua hilo ndio maana ameamua tu kushona midomo yake asiumbuke.
 
Sasa nimeelewa ni kwaniniMakinda hakuruhusu hii kitu isisomwe na akasema swala hili halitarudi bungeni mkutano ujao...........Ingekuwa ni aibu ya mwaka kwa Pinda. Machozi yangemtoka. Kweli CHADEMA ni noma!

Mkuu,

Samahani sikupata kujua ili suala liliishaje!!! Ina maana Spika alisema halipashwi kujadiliwa tena? Kwa nini lisijadiliwe? Vipi kauli hizo za uongo zingekuwa zimetolewa na Mbunge wa kambi ya upinzani? Hapana, nafikiri Chadema inabidi walivyalie njuga ili suala ikibidi Pinda afute kauli zake au athibitishe kwamba alichokisema ni ukweli ili mgogoro uhamie kwa Lema. Kulinyamazia suala hili, itakuwa ni sawa na kutoa blessings za spika kuendelea kuwanyanyasa wapinzani bungeni.

Tiba
 
Mods, please ziunganishe hizi threads mbili zinazozungumzia suala lile lile. Kuna thread nyingine inaendelea juu ya taarifa hii.

Tiba
 
Hapo kwenye Uongo wa 6 sita kuna mtihani kidogo unaweza kuwa Uongo mwingine tena Mhe. Lema kausema Bungeni, kamtaja Dr Slaa, kuwa ana mke kwani kaishafunga ndoa? Spika anaweza kuitaji Marriage Certificate

kwa kuwa hana akili yule supika anaweza kudai
 
Jamani, nimesoma aya baada ya aya, sentensi baada ya sentensi, neno baada ya neno kwa umakini mkubwa. Kwa maelezo hayo ya Mhe. Lema ni wazi kuwa waziri mkuu pinda angebomolewa bungeni kwa aibu ya mwaka na huo ndiyo ungekuwa mwisho wa heshima yake (kama bado ipo) mbele ya wananchi. Kwa nini nasema hivi nitaeleza. Watanzania wengi sasa hivi wanafuatilia sana mwenendo wa bunge letu la jamhuri na mijadala yake. Tukio la Mhe. Lema kutoa ushahidi wake kuhusu uongo wa mizengo pinda lingevuta wengi. Kwa maneno mengine, tukio hilo lisingetofautiana sana na lile Dr. Mwakyembe kusoma taarifa ya uchunguzi wa skendo ya Richmond. Kwa kufanya hivyo, watanzania wengi wangebaini kuwa waziri mkuu ni mwongo jambo ambalo kwa kiasi kikubwa lingemvunjia heshima mtoto wa mkulima.

Inavyoonekana, jeshi la polisi na waziri wa mambo ya ndani ndio waliomdanganya waziri mkuu kwa sababu katika hali ya kawaida wao ndiyo chanzo cha uhakika cha majibu ya waziri mkuu. Kwa maana hiyo basi, baada ya Mhe. Lema kusoma majibu yake hayo ilipaswa IGP na waziri wake wa mambo ya ndani wajiuzuru mara moja.

Ukitafakari kwa kina unaweza ukabaini kuwa kutosomwa kwa taarifa hiyo bungeni kunaepusha pia aibu kwa mama spika. Kauli yake ya jazba na staili aliyotumia kumuagiza Mhe. Lema ilionyesha kuwa Mhe. Lema ndiye mwongo kwa maana kwamba alimsingizia waziri mkuu. Kwa kiasi fulani Mhe. Lema (labda na chama chake) walipata demage ya credibility yake mbele ya jamii pana ya kitanzania. Kwamba Mhe. Lema ni mtu mwenye jazba, mpenda vurugu, mwenye majungu, mwongo, n.k. jambo ambalo ni kinyume na hali halisi.

My take:
Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CDM (Mungu aendelee kukitunza na kukipatia maisha marefu) ni chama makini na wananchi wengi tunaendelea kuamini hivyo na kila siku inayoitwa siku tunahakiki kwa vitendo. Kutokana na umakini huo, nawashauri viongozi wa chama muangalie namna fulani ya kushinikiza bila jazba usomwaji wa taarifa hii bungeni ili wananchi kwa ujumla wao wasikie na kuhitimisha suala hili. Kusomwa kwa taarifa hii bungeni kutasafisha jina la Mhe. Lema na kuendelea kuongeza hadhi ya CDM mbele ya wananchi. Vile vile, kusomwa kwa taarifa hii kutawezesha wananchi kutambua namna haki yao ya msingi ya kukusanyika kwenye mihadhara inavyochezewa na serikali kiasi cha kusababisha kifo kwa wananchi wake badala ya kuwalinda na kuwaepusha na kifo. Kutokana na mazingira haya, nashauri akina Tundu Lissu na wenzie watafute namna ya kumkumbusha spika suala hili ili wapewe nafasi ya kusoma taarifa hii bungeni. Wakati wa kumwomba spika waonyeshe masikitio yao kwamba endapo taarifa hii haitasomwa hadharani bungeni spika hatakuwa amemtendea haki Mhe. Lema kwa upande mmoja na CDM kwa upande wa pili kwa sababu hadi sasa wananchi wengi wanatambua kuwa Mhe. Lema ndiye aliyekuwa mwongo. Spika akionyesha msimamo wa kukataa taarifa isisomwe then CDM iangalie namna ya kuisambaza taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari hususani magazeti ili wananchi wasome.

Mojawapo ya watoa maoni kwenye thread hii kuna mtu anajiita 'chatu dume'. Ame-question uhalali wa kusema 'mke wa Dr. Slaa'. Inavyoonekana ni kwamba yeye anaona ni kosa. Pamoja na upuuzi wa hoja yake, naomba CDM wasimpuuze kwani ninavyokifahamu chama cha sisiem sitshangaa jambo kama hilo kuongelewa bungeni endapo taarifa hii itakubalika isomwe bungeni na Mhe. Lema. Yaandaliwe majibu ya kisheria kuhusu hoja hii ya kipuuzi. Alichosema PakaJimmy ni sahihi kabisa. Sisiem ni chama cha taarabu, cha mipasho. Kwa hiyo, sitashangaa kumsikia mheshimiwa fulani akimuuliza spika kama alivyouliza mtu anayejiita 'chatu dume' na wakati mwingine unaweza ukashangaa huyo anayejiita 'chatu dume' ni mbunge wa sisiem.
 
Mkuu naona ujapenda mimi kuchangia hii thread ya Uthibitisho wa Mbunge Lema, mpaka umeandika post yangu upuuzi wa hoja labda nikujibu mimi ni mtu wa kawaida kabisa wala sijawahi kuwa CCM kama ningekuwa mbunge kama unavyosema wewe ningesubiri huu Uthibitisho huu Bungeni niombe muongozo spika ni Question, nadhani sijafanya kosa ku-question hilo
 
Bro..
Dont take things too serious...
Hizi ni changamoto za kawaida tu, nia ikiwa ni kuwekana sawa juu ya jambo hili...hivyo tuliza moyo.
 
Hapo kwenye Uongo wa 6 sita kuna mtihani kidogo unaweza kuwa Uongo mwingine tena Mhe. Lema kausema Bungeni, kamtaja Dr Slaa, kuwa ana mke kwani kaishafunga ndoa? Spika anaweza kuitaji Marriage Certificate
Kama nakumbuka vizuri kuna sheria inasema watu (me&ke) wakiishi chini ya paa moja kwa kipindi cha miezi sita ni mume na mke.
 
Naona wengi mnakurupuka na kuuona kuwa huo ni "ushahidi" kuwa PM kasema "uongo", la, hasha. Ukiupitia ki umakini huo "ushahidi" utaona kuwa Lema au waliemwandikia huo "ushahidi" wamejikanganya vibaya sana na huo "ushahidi" una contradictions kibao na "self incriminatory".

Kama ni mwana sheria ndie aliuandika, basi huyo ni "bomu".

Ametoa maelezo mareeeefu ambayo yanazunguka halafu yanamkaanga mwenyewe. Sijaona hata pamoja panapo-onyesha kuwa PM kasema uongo.

Nna uhakika Makinda na jopo la wanasheria wanaomsaidia bungeni watausambaratisha huu "ushahidi" na uonekane kuwa ni upupu.

Mimi si mwanasheria, lakini, nimeona "ushahidi" una mapungufu mengi sana.
 
kazi kweli kweli serikali ya chama cha mapinduzi bana acha tu,karibia viongozi wote waongo.
 
Back
Top Bottom