Uteuzi Wanafunzi wa vyuo Vikuu hadi Sept 22 -TCU

Status
Not open for further replies.

sir dak

Member
Aug 25, 2014
81
9
Uteuzi Wanafunzi wa vyuo Vikuu hadi Sept 22 -TCU

Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)imefunguka na kuweka wazi kuwa mpaka sasa hawajatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2014-2015 kama ambavyo watu wanakuwa

New-Media.jpg

Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV.

wakidai kuwa tume hiyo imatangaza,Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku amesema hayo leo alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wa ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana mpaka nane mchana.

"Mimi mwenyewe nimesikia kuwa watu wanadai Tume ya vyuo vikuuu imetangaza majina ya wanafunzi waliochanguliwa kwa mwaka wa masomo 2014-2015 lakini nashindwa kuelewa hizo tetesi au hayo majina waliyoyaona yametoka wapi?maana mpaka sasa Tume kama tume badao haijatoa majina hayo ya wanafunzi na tunategeme kuyatoa kwenye tarehe 22 ya mwezi huu,baada ya Joint Admission Comitee kupitia na kupitisha majina hayo."

Mbali na kueleza juu ya siku ambayo Tume ya vyuo vikuu itatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa vyuo mbalimbali lakini pia Edward Mkaku alijaribu kufafanua kuwa hawajachelewa kutoa majina ya wanafunzi kujiunga vyuo kwa kuwa miaka yote vyuo vilivyo vingi hufunguliwa mwezi wa kumi hivyo ni kawaida kwa majina hay9o kutoka mwezi wa tisa ili ifikapo mwezi wa kumi wawezi kujiunga bila matatizo,pia alidai kuwa hiyo imekuwa kawaida kwa Taasisi hiyo kutangaza matokeo mwezi wa tisa kwani hata miaka miwili iliyopita yalitangazwa mwezi huo huo.

"Nadhani kila mtu anatambua kuwa vyuo vikuu vingi hufunguliwa mwezi wa kumi hivyo imekuwa kawaida kwetu kutangaza majina ya wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo mwezi wa tisa maana hata mwaka jana na mwaka juzi ilikuwa hivihivi ndugu"

ADA ELEKEZI

Katika masuala ambayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wanafunzi wengi na wengine hata kupelekea kushindwa kumaliza masomo yao ni suala la Ada na kumekuwa na utofauti mkubwa sana katika masuala ya ada kutoka chuo kimoja mpaka chuo kingine hususani katika vyuo vya watu binafsi au taasisi.lakini kwa mujibu wa Afisa habari Mwandamizi toka TCU, Edward Mkaku amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo 2014-2015 Taasisi ya Vyuo

Vikuu imekuja na mfumo elekeze wa ada kwa vyuo vyote na wanapaswa kuufuata,yaani kila chuo kimepangiwa Ada inayostahili kulipwa na wanafunzi kulingana na uwezo wa chuo husika na huduma itolewayo katika chuo husika.

Kitendo cha Tume ya Vyuo Vikuu kuja na mfumo elekeze wa Ada kwa vyuo vikuu itasaidia kushuka kwa Ada kwa baadhi ya vyuo vilivyokuwa vikichaji Ada kubwa kuliko huduma wanayoitoa.pia itasaidia hata wanafunzi kuweza kumudu Ada hizo katika vyuo hivyo.

"Mkaku kuanzia mwaka huu kuna utaratibu wa Ada elekezi ambapo Tayari kila chuo kinapaswa kuufuata"
Source: eatv.tv
 
East Africa Television (EATV)
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)imefunguka
na kuweka wazi kuwa mpaka sasa
hawajatangaza majina ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali
kwa mwaka wa masomo 2014-2015 kama
ambavyo watu wanakuwa wakidai kuwa tume
hiyo imetangaza.
Soma zaidi hapa
NEWS | East Africa Television
wanafunzi-wa-vyuo-vikuu-hadi-sept-22-tcu

mtu aliyepata chuo kibaya utamjua tu
 
kuna maswali yanaboa sana. mtu anaulizia soko la ajira kama alilazmishwa kusoma vile. wengine wana haraka ya kuona matokeo wakati umeambiwa usubiri.

Mwingine utaskia tunatakiwa kujipanga. kama tangu unaona matokeo hujajipanga wewe sjui ni mtu wa aina gan.

Mwingne utaskia tumechoka kukaa nyumbani, kwani ukipewa matokeo utakaa barabarani? patience ni kitu moja kinacholipa sana. Kama mnatafuta soko nendeni mkatafute soko la subira.
 
East Africa Television (EATV)
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)imefunguka
na kuweka wazi kuwa mpaka sasa
hawajatangaza majina ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali
kwa mwaka wa masomo 2014-2015 kama
ambavyo watu wanakuwa wakidai kuwa tume
hiyo imetangaza.
Soma zaidi hapa
NEWS | East Africa Television
wanafunzi-wa-vyuo-vikuu-hadi-sept-22-tcu

mkielewa hii hakutokua na shida...

tusikatae kuwa tcu kuwa haijatangaza bado ila tukubal majina yali leak na mm ni mmoja wa nilieyaona na nimechaguliwa udom geology.. habari za watabadilisha hakuna kitu. ka hiyo
 
mkielewa hii hakutokua na shida...

tusikatae kuwa tcu kuwa haijatangaza bado ila tukubal majina yali leak na mm ni mmoja wa nilieyaona na nimechaguliwa udom geology.. habari za watabadilisha hakuna kitu. ka hiyo


Yeah na ninasikia hata mwaka jana majina yali leak pia na hamna mabadiliko yoyote yaliyotokea after the official release
 
kuna maswali yanaboa sana. mtu anaulizia soko la ajira kama alilazmishwa kusoma vile. wengine wana haraka ya kuona matokeo wakati umeambiwa usubiri. mwingine utaskia tunatakiwa kujipanga. kama tangu unaona matokeo hujajipanga wewe sjui ni mtu wa aina gan. mwingne utaskia tumechoka kukaa nyumban. kwan ukipewa matokeo utakaa barabarani? patience ni kitu moja kinacholipa sana. kama mnatafuta soko nendeni mkatafute soko la subira.

mbna akili yako na ulichopost havifanani!au ultaka utuoneshee mistari yako au co.
 
Walio yaona majina yao mara yakwanza ndo hayohayo no changes even after official release!!..wale mnaobisha hamlazmishw kuamin ila jibu mtapata tar 22!!
 
Matokea ni yaleyale yalioleak jmosi, TCU inawachagulia chuo si unilichochagua mtu aliyepata 1.7 PCB chaguo lake la 1 ni MUHAS wao wamempeleka BUGANDO mwingine chaguo lake la 1 ana div 3.10 wamempeleka MUHAS.

Kijana wangu chaguo lake la 1 ud law div 2.8 wamempeleka mzumbe rafiki yk 2.9 kapelekwa ud, mwingine kapelekwa st joseph na jina lake leo nimeliona kapata 1.7 PCM ST JOSEPH chaguo lake la mwisho.

Sio haki kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom