Uteuzi wa Kadhi Mkuu waibua mvutano

Status
Not open for further replies.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, 17 July 2012 21:39

Raymond Kaminyoge

UTEUZI wa Kadhi Mkuu na makadhi wa mikoa 14 uliofanywa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba, umeibua mvutano miongoni mwa Waislamu.

Juzi, Mufti Simba alimtangaza Sheikh Abdallah Mnyasi kuwa Kadhi Mkuu na pia aliwateua Manaibu wake wawili, Sheikh Abubakar Zubeir na Sheikh Muhidini Mkoyogole.
Wakizungumzia uteuzi huo, baadhi ya viongozi wa taasisi za Kiislamu walisema kilichofanyika ni uteuzi wa kiserikali na si wa Kiislamu.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema uteuzi huo ni wa kiserikali na siyo wa dini... "Hata mkutano wenyewe ulisimamiwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ndiyo maana tunasema uteuzi huu una ladha ya kiserikali."

Sheikh Ponda alisema uteuzi huo ni wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) na haujawashirikisha Waislamu kutoka katika taasisi zao nyingine.
Alisema moja ya malengo ya uteuzi huo ni kuwaondoa Waislamu katika ajenda yao ya kutaka Mahakama ya Kadhi katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya.

Alisema lengo jingine ni kutaka kuwaondoa Waislamu kwenye msimamo wao wa kutoshiriki kwenye Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.

"Lakini, tunasema msimamo wetu upo palepale. Uteuzi huu hautarudisha nyuma harakati zetu kwa sababu Bakwata ni sehemu tu ya Waislamu nchini," alisema Sheikh Ponda.

Katibu wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita), Said Mwaipopo alisema kwa kuwa hawajashirikishwa, kuna uwezekano wa kila taasisi kuwa na kadhi wake.

"Bakwata si wamewateua makadhi wa mikoa bila ya kuzishirikisha taasisi nyingine za dini ya Kiislamu? Basi nazo zikiamua zinaweza kuteua makadhi wake wa mikoa," alisema.

Alisema kuna taasisi nyingi za Kiislamu nchini na kwamba, Bakwata ni moja ya taasisi hizo... "Sasa kama linafanyika jambo kubwa kama hilo halafu wadau wanalisikia kwenye vyombo vya habari unategemea nini? Nao wataamua kuteua makadhi wao."

Akizungumzia uteuzi huo, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Bakwata, Shaaban Simba alisema ulifanyika juzi Mjini Dodoma baada ya mkutano wa Tume ya Dini ya Baraza hilo na kwamba makadhi wa mikoa mingine watateuliwa baadaye.

"Mufti anaendelea na mchakato wa kuwateua makadhi wa mikoa mingine na watakapokamilika watatangazwa," alisema.

Simba alisema baada ya kuteuliwa makadhi wengine wa mikoa uteuzi utakaofuata ni wa makadhi wa wilaya.

Kwa upande wake, Kadhi wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab alisema uteuzi huo umefanyika katika kipindi muafaka.Alisema Serikali ilitoa tamko la kuwataka Waislamu waanzishe Mahakama ya Kadhi ambayo wataiendesha wao wenyewe.

"Badala ya kuendelea kubishana na Serikali, Baraza limeamua kufanya uteuzi kwa ajili ya kuanzisha chombo hiki lakini, bado tunaendelea kuzungumza na Serikali kuangalia namna inavyoweza kukiendesha chombo hiki kwa kushirikiana na Waislamu," alisema.

Walioteuliwa
Simba aliwataja makadhi wa Mikoa 14 walioteuliwa juzi kuwa ni Sheikh Masoud Himid Jongo (Dar es Salaam), Sheikh Mustafa Rajab Shaaban (Dodoma), Sheikh Zukher Bin Sheikh Bakher (Tanga) na Sheikh Hamis Maalim Abbas Mtupa (Pwani).

Wengine ni Sheikh Shaaban Bin Jumaa (Arusha), Sheikh Shaaban Rashid (Kilimanjaro), Sheikh Salum Fereji (Mwanza), Sheikh Ismail Habib Makusanya (Shinyanga), Sheikh Abdallah Ali (Mtwara), Sheikh Muhamad Hamis Mushangani (Lindi) Sheikh Athuman Magee (Mara), Sheikh Idrisa Abdul Muhsin Kitumba (Kigoma), Sheikh Rashid Akilimali (Rukwa) na Sheikh Shaaban Salum (Tabora).
 
Sasa Ina Maana kama una kesi Wewe Mkristo na yeye Mwislamu mtakwenda Mahakama Tofauti?
 
Uteuzi wa Kadhi Mkuu waibua mvutano Send to a friend
Tuesday, 17 July 2012 21:39
0diggsdigg

Raymond Kaminyoge
UTEUZI wa Kadhi Mkuu na makadhi wa mikoa 14 uliofanywa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba, umeibua mvutano miongoni mwa Waislamu.

Juzi, Mufti Simba alimtangaza Sheikh Abdallah Mnyasi kuwa Kadhi Mkuu na pia aliwateua Manaibu wake wawili, Sheikh Abubakar Zubeir na Sheikh Muhidini Mkoyogole.
Wakizungumzia uteuzi huo, baadhi ya viongozi wa taasisi za Kiislamu walisema kilichofanyika ni uteuzi wa kiserikali na si wa Kiislamu.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema uteuzi huo ni wa kiserikali na siyo wa dini... “Hata mkutano wenyewe ulisimamiwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ndiyo maana tunasema uteuzi huu una ladha ya kiserikali.”

Sheikh Ponda alisema uteuzi huo ni wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) na haujawashirikisha Waislamu kutoka katika taasisi zao nyingine.
Alisema moja ya malengo ya uteuzi huo ni kuwaondoa Waislamu katika ajenda yao ya kutaka Mahakama ya Kadhi katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya.

Alisema lengo jingine ni kutaka kuwaondoa Waislamu kwenye msimamo wao wa kutoshiriki kwenye Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.

“Lakini, tunasema msimamo wetu upo palepale. Uteuzi huu hautarudisha nyuma harakati zetu kwa sababu Bakwata ni sehemu tu ya Waislamu nchini,” alisema Sheikh Ponda.

Katibu wa Baraza la Habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita), Said Mwaipopo alisema kwa kuwa hawajashirikishwa, kuna uwezekano wa kila taasisi kuwa na kadhi wake.

“Bakwata si wamewateua makadhi wa mikoa bila ya kuzishirikisha taasisi nyingine za dini ya Kiislamu? Basi nazo zikiamua zinaweza kuteua makadhi wake wa mikoa,” alisema.
Alisema kuna taasisi nyingi za Kiislamu nchini na kwamba, Bakwata ni moja ya taasisi hizo... “Sasa kama linafanyika jambo kubwa kama hilo halafu wadau wanalisikia kwenye vyombo vya habari unategemea nini? Nao wataamua kuteua makadhi wao.”

Akizungumzia uteuzi huo, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Bakwata, Shaaban Simba alisema ulifanyika juzi Mjini Dodoma baada ya mkutano wa Tume ya Dini ya Baraza hilo na kwamba makadhi wa mikoa mingine watateuliwa baadaye.
“Mufti anaendelea na mchakato wa kuwateua makadhi wa mikoa mingine na watakapokamilika watatangazwa,” alisema.

Simba alisema baada ya kuteuliwa makadhi wengine wa mikoa uteuzi utakaofuata ni wa makadhi wa wilaya.

Kwa upande wake, Kadhi wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab alisema uteuzi huo umefanyika katika kipindi muafaka.Alisema Serikali ilitoa tamko la kuwataka Waislamu waanzishe Mahakama ya Kadhi ambayo wataiendesha wao wenyewe.

“Badala ya kuendelea kubishana na Serikali, Baraza limeamua kufanya uteuzi kwa ajili ya kuanzisha chombo hiki lakini, bado tunaendelea kuzungumza na Serikali kuangalia namna inavyoweza kukiendesha chombo hiki kwa kushirikiana na Waislamu,” alisema.

Walioteuliwa
Simba aliwataja makadhi wa Mikoa 14 walioteuliwa juzi kuwa ni Sheikh Masoud Himid Jongo (Dar es Salaam), Sheikh Mustafa Rajab Shaaban (Dodoma), Sheikh Zukher Bin Sheikh Bakher (Tanga) na Sheikh Hamis Maalim Abbas Mtupa (Pwani).

Wengine ni Sheikh Shaaban Bin Jumaa (Arusha), Sheikh Shaaban Rashid (Kilimanjaro), Sheikh Salum Fereji (Mwanza), Sheikh Ismail Habib Makusanya (Shinyanga), Sheikh Abdallah Ali (Mtwara), Sheikh Muhamad Hamis Mushangani (Lindi) Sheikh Athuman Magee (Mara), Sheikh Idrisa Abdul Muhsin Kitumba (Kigoma), Sheikh Rashid Akilimali (Rukwa) na Sheikh Shaaban Salum (Tabora).

Sasa hii ni chokochoko. Kadhi si mmepewa? Kaeni wenyewe kwa wenyewe mmalize suala la kadhi. Pia sioni uhusiano wa kadhi na kususia sensa.
 
Sasa Ina Maana kama una kesi Wewe Mkristo na yeye Mwislamu mtakwenda Mahakama Tofauti?
yakhe kuna mambo ndio yanahusishwa na sio kila kitu,kama hilo jambo lina mikataba au lilifanywa kwa njia za kupitia hapo mahakama basi mtaenda hapo la kama ni vichochoroni mtaenda za huko serikalini.
 
Sasa hii ni chokochoko. Kadhi si mmepewa? Kaeni wenyewe kwa wenyewe mmalize suala la kadhi. Pia sioni uhusiano wa kadhi na kususia sensa.

Kwani unadhani utashirikishwa wewe mkristo ktk mchakato huu kadhi ??? Naona inawauma sana.
 
Mwanaharaki Ponda.
Kwa nini kila wakati unakuwa against Bakwata?
Tulikuwa tunalilia kupata Mufti na tayari tumempata,huoni kama hii ni hatua moja mbele?
Mara nyingi nimekuwa sikuelewi kwani unaelekea kuwa mtu wa shari kuliko kusaidia jami ambayo ipo chini.
Wenzetu wanaitumia nafasi vizuri na wamejaza vyuo vikuu sisi hata sekondari za kuhesabu na tukitoka hapo ni kulia kuonewa kama yatima.
Tutumie fursa na tuwe waadilifu tutapata maendeleo.
Kama una hoja nenda kaongee na Sheikh Mkuu lakini kwangu nashindwa kukuelewa.
Hebu Ponda mtizame Kijana Arfu wa Islamic foundation mambo anayosimamia,huu ni mfano wa kuigwa sio kila wakati kupinga wenzio.
 
Kadhi courts are special for brain dead idiot people !
This is a sarcastic statement.Take some time to read on how these courts work and get a little bit of insight on Shariah.
You may not agree with it but at least you can widen your thinking horizon.
 
Kuchaguliwa kwa makadhi ni kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi Tanzania bara. Ni vema kufahamu mipaka ya kadhi court na secular/ civil court. Pia endapo civil court inapogongana na kadhi court ni ipi ina-prevail. Halafu ni muhimu sana tukafahamu vyanzo vya fadha kwa ajili ya kugharamia hizo kadhi courts, kama ni kodi yangu mimi mkatoliki aisee! sitaki kabisa na taanza kukwepa kodi!! Kama pesa inatoka Iran sawa lakini mkataba uwe wazi!!
 
This is a sarcastic statement.Take some time to read on how these courts work and get a little bit of insight on Shariah.
You may not agree with it but at least you can widen your thinking horizon.

Well said chief! LIKE
 
hivi ndani ya uislam mfumo wao wa uongozi ukoje,kwani hamna mwenye mamlaka ya mwisho hadi kufikia hatua ya kupingana kila wakati.!
 
Hayo ndo madhara ya kuwa tegemezi.waislam mnapenda mno vya bure.BAKWATA inaendeshwa na serikali unategemea serikali iwaruhusu mjiamulie mambo?
 
i hate this..
Kama hii itaendelea hivi huu utakua ndio mwisho wa usalama kati ya waislam na wakristo wakristo na serikali na waislam na serikari!Hii ni kwasababu waislam si wamoja na hawana kiongozi mmoja ila inapokuja suala fujo hujifanya ni wamoja!kuna kipengele kinaruhusu waislam kudanganya wakristo ili kuendeleza uislam hivo kitendo cha kusema eti kadhi atadili na ishu zile simpo ni kudanganya watu ili waingize mauaji makubwa ya kishetani hapa nchini maana kwa mujibu wa sheria za kiislam watu hawapo sawa mbele ya sheria, wanaume ni bora kuliko wanawake adhabu zote zinaishia na kuua so hii nailaani na nitakubali kfanya chochote kuweka kumbukumbu mbaya juu ya serikali kukubali upuuzi huu
 
What??? You don't deny that kadhi courts are for the "brain dead ******"??

Naona umekurupuka alafu sielewi unachozungumzia ni nini ...?!Mate IF you have to replay me in English would you please do us a favor & learn the language ..?! other wise andika kwa kiswahili kilichonyooka ulitaka kuongea nini..?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom