Dr Mwinyi ni Mtanzania kama walivyo watanzania wengine. Hata Mtkila alipohoji Mahakamani kuhusu suala la Wazanzibari kuteuliwa kwenye Wizara zisizo za Muungano hoja yake ilishindwa vibaya! Tatizo linalotusumbua sasa hivi watz ni ubaguzi uliopandikizwa na wanasiasa! Utasikia siku hizi "Rais wa safari hii atatoka Kaskazini!" Tutafika kweli kwa style hii?
Nilikuwa naongea na rafiki yangu asubuhi hii kuhusu baraza jipya na nilipomtaja Mwinyi kuwa yeye ameteuliwa waziri wa afya kauli ya kwanza alisema "afya haiko muungano na huyu ni mbunge wa Zanzibar, ameingiaje? Hii ni kauli ya mzanzibari.tuachie hapo.
Sasa turudi kwenye muungano wenyewe, kuna makubaliano kuhusu wizara/mambo gani yawe ya muungano ya yape yasiwe ya muungano, sasa kama hayo mambo hayazingatiwi kwenye uteuzi wa mawaziri kuna sababu gani ya kuwa na makubalino ya muungano? Hoja hapa ni kuheshimu taratibu na makubaliano ya muungano. simple.
Mwisho, huu uteuzi wa Dr. Mwinyi unawaweka wapi wabunge wa CCM toka Tanzania bara? Kwamba miongoni mwao hakuna anayefaa kuongoza wizara ya afya na hivyo rais amelazimika kukopa toka Zanzibar? Nadhani wakati mwingine matatizo ya CCM yanasababishwa na wao wenyewe kama huu uteuzi. Hapa jukwaani tunaongea but I am sure ndani ya CCM kwenyewe watu wanahasira.