Uteuzi wa Dr. Hussein Mwinyi Wizara ya Afya Umezingatia Masuala ya Muungano?

Hii si sawa kabisa.Ina maana hamna mtu wa bara anayefit hiyo nafasi? Ingekuwaje kama mbunge wa bara angeteuliwa kuwa waziri wa afya Zanzibar? Si wangeitisha maandamano na kila siku kupinga na kuchomea wabara vibanda vyao huko? Upole wetu watanganyika ndio uliotufikisha hapa na utatumaliza.....
 
Hussein Mwinyi kateuliwa kwa sababu ya "Utanzania" wake na si kwa sababu ya "Uzanzibari" wake!

Huyu bwana ana matatizo. Dr. H. Mwinyi kama tuliona anatufaa tungemteua kwanza kuwa mbunge kama alivyo NAHODHA. Suala si Uzanzibar, ila Ubunge wa URT!!
 
Ukienda Zanzibar kuomba kumiliki Ardhi wewe na Mtaliano, Mtaliano atapewa Ardhi ajenge Hoteli wewe utaambiwaArdhi si mambo ya Muungano. Wizara ya Afya si ya Muungano na hivyo haipaswi kuendeshwa na Mzanzibari watuachie tuendeshe mambo yetu sisi wenyewe na wao waendelee na "uamsho" wao!!

Kigarama umetukumbusha jambo la msingi sana.
Kwa mtu ambaye hajawahi kufika zanzibar huenda asijue hili ulilotaja hapa. Mimi binafsi nimefika mara kadhaa huko, maeneo ya pwani mchangani kiwengwa, nungwi, matemwe, makunduchi, paje pamoja na maeneo mengine mengi.

Hawa jamaa zetu wako radhi kuwapatia ardhi wataliano na wahindi. Na wakenya nao wameanza kuingia kwa kasi sasahivi, kuliko mtanzania mwenzao, kwa sababu tu ametoka bara.

Lakini wao wamejazana huku bara bila kubugudhiwa, hadi kahama nimekutana na wapemba wamejenga huko na biashara zinaendelea.
 
Last edited by a moderator:
Mwita, ndiyo maana wazenji hawautaki huu muungano, mambo yake hayaeleweki. Ni vurugu tupu!!!

Afadhhali uvunjike
 
Huyu bwana ana matatizo. Dr. H. Mwinyi kama tuliona anatufaa tungemteua kwanza kuwa mbunge kama alivyo NAHODHA. Suala si Uzanzibar, ila Ubunge wa URT!!

SONGEA hapa tunachohoji ni kama wizara ya afya ni katika mambo ya muungano hadi kustahili kuongozwa na mbunge kutoka zanzibar.

Kwa taarifa yako Dr. Mwinyi ni mbunge wa jimbo la Kwahani zanzibar, tofauti na Shamsi Nahodha ambaye alikuwa mwakilishi, ndio sababu aliteuliwa kwanza kuwa mbunge kabla hajateuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Last edited by a moderator:
Huyu bwana ana matatizo. Dr. H. Mwinyi kama tuliona anatufaa tungemteua kwanza kuwa mbunge kama alivyo NAHODHA. Suala si Uzanzibar, ila Ubunge wa URT!!

Er? Utata hapa! Unataka kunambia mzanzibari akiwa mbunge wa JMT anazo sifa za kuwa waziri kwenye wizara isiyohusisha maswala ya muungano? Tatizo hapa ni uzanzibari au kutokuwa mbunge wa URT? Navyojua Hussen Mwinyi ni mbunge wa JMT na si mwakilishi wa SMZ.
 
Mwita, ndiyo maana wazenji hawautaki huu muungano, mambo yake hayaeleweki. Ni vurugu tupu!!!

Afadhhali uvunjike

Mawenzi ni kweli wazanzibari wengi hawautaki muungano lakini wao ndio wananufaika zaidi na aina ya muungano tulio nao lakini bado ndio wanapiga kelele za kutaka kuuvunja kuliko sisi tusionufaika sana.
 
Last edited by a moderator:
nimesikitika sana jaman tanzania hatuna rais, hakuna rais dunian ambaye hazingatii all dimension za uongozi wake, huyu jamaa kamweka mzanzibari kuongoza bara na harusiwii kuingilia mambo ya afya ya zanzibar maaana si swala la muungano........ jaman jaman mi kikwete naapa sio rais wangu kuanzia leo.,... siwezi kuwa na rais ambaye si mwelewa kabisa....Nimekumbuka maneno ya prof wangu wa sugery kutoka italy aliniambia kuwa "THERE IS NO AMPUTATION OF THE HEAD BUT THE TANZANIA PRESIDENT IS THE ONLY LIVING THING WHO LIVES WITH AMPUTATED HEAD" mwanzo nilidhan kamtukana rais wangu lakin kumbe leo ndo nimejua alichoimanisha
 
SONGEA hapa tunachohoji ni kama wizara ya afya ni katika mambo ya muungano hadi kustahili kuongozwa na mbunge kutoka zanzibar.

Kwa taarifa yako Dr. Mwinyi ni mbunge wa jimbo la Kwahani zanzibar, tofauti na Shamsi Nahodha ambaye alikuwa mwakilishi, ndio sababu aliteuliwa kwanza kuwa mbunge kabla hajateuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Hili li muungano na mkatiba wetu bana... Inakuwaje pale Mwakilishi Zenji anapoteuliwa kuwa mbunge wa JMT, uwakilishi unakoma? Vikao vinapoenda sambamba mathalan wakati wa bajeti anahudhuria kikao kipi kati ya baraza la wawakilishi na bunge? Sitashangaa siku moja mtu mmoja akawa waziri wa JMT na wakati huohuo waziri wa SMZ! Hahah katiba haikatazi na hakuna mjadala wa muungano katika katiba mpya!
 
Last edited by a moderator:
Huyu bwana ana matatizo. Dr. H. Mwinyi kama tuliona anatufaa tungemteua kwanza kuwa mbunge kama alivyo NAHODHA. Suala si Uzanzibar, ila Ubunge wa URT!!

Off point! Mhusika tayari ni Mbunge wa Bunge la JMT. Kinachogombewa hapa ni: INAKUWAJE MBUNGE KUTOKA ZANZIBAR APEWE WIZARA "TANGANYIKA" AMBAYO SIO YA MUUNGANO? Alipokuwa Waziri wa Ulinzi na JKT haikuwa na shida kwa sababu wizara hiyo ni ya Muungano lakini Wizara ya Afya siyo!

UCHOKOZI: Hivi mbona Makao Makuu ya Wizara zote za Muungano yako Tanganyika a.k.a. Tanzania Bara? Hakuna hata moja yenye makao yake Zanzibar! Utajaza mwenyewe.
 
Hii si sawa kabisa.Ina maana hamna mtu wa bara anayefit hiyo nafasi? Ingekuwaje kama mbunge wa bara angeteuliwa kuwa waziri wa afya Zanzibar? Si wangeitisha maandamano na kila siku kupinga na kuchomea wabara vibanda vyao huko? Upole wetu watanganyika ndio uliotufikisha hapa na utatumaliza.....

Huyu jamaa ameshindwa wizara ya ULINZI ambayo ina watendaji wasiotegemea wizara katika kuendesha mambo yao, ndo ataweza wizara ya Afya yenye changamoto nyingi. Ni ndoto, ni mmoja wa watu ambao hawakupaswa kuwepo kwenye baraza la mawaziri la sasa. Coz kumbuka mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto alishindwa kuhandle kitu kidogo kama kile. Pia wizara ya afya haiko kwenye Muungano kwa nini wamemteua? Huu muungano unapaswa kurekebishwa kwa kiwango kikubwa sana.
 
Heri ya Mwinyi kuliko angepewa Hamis Kingwangwala

Ha ha haaa. Rev. Masanilo pwenti yako nimeielewa sana. Kama Kigwangalla alitegemea kuteuliwa basi alikuwa anajidanganya, yeye bado sana.

Nini maoni yako lakini kuhusu kwa wizara ya afya kupewa waziri anayetoka zanzibar wakati si suala la muungano?
 
Last edited by a moderator:
Huyu bwana ana matatizo. Dr. H. Mwinyi kama tuliona anatufaa tungemteua kwanza kuwa mbunge kama alivyo NAHODHA. Suala si Uzanzibar, ila Ubunge wa URT!!

Dr Mwinyi ni Mtanzania kama walivyo watanzania wengine. Hata Mtkila alipohoji Mahakamani kuhusu suala la Wazanzibari kuteuliwa kwenye Wizara zisizo za Muungano hoja yake ilishindwa vibaya! Tatizo linalotusumbua sasa hivi watz ni ubaguzi uliopandikizwa na wanasiasa! Utasikia siku hizi "Rais wa safari hii atatoka Kaskazini!" Tutafika kweli kwa style hii?
 
Inasikitisha kuona viongozi wakubwa wa nchi hawako serious, shame on them, kama una akili timamu uta-overlook vipi suala kama hili, inawezekana hata hawajui masuala gani yapo ndani ya muungano na yepi hayahusiki katika muungano, hii inadhihirisha kuwa muungano zaidi ni kwa faida ya wazanzibari.....upss.
 
dudus kuhamishia makao makuu ya wizara za muungano ''nchini zanzibar'' ni sawa na kuyahamishia nchi jirani.

Makao makuu ya nchi yapo Dodoma kinadharia lakini kiuhalisia yako Dar es salaam na ndiko wizara zote zilipo.
 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha kuona viongozi wakubwa wa nchi hawako serious, shame on them, kama una akili timamu uta-overlook vipi suala kama hili, inawezekana hata hawajui masuala gani yapo ndani ya muungano na yepi hayahusiki katika muungano, hii inadhihirisha kuwa muungano zaidi ni kwa faida ya wazanzibari.....upss.

Halafu ni hao hao wanaokaza wananchi wasijadili suala lolote la muungano wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya. Hii nchi sometimes ni kichefuchefu.
 
... kuhamishia makao makuu ya wizara za muungano ''nchini zanzibar'' ni sawa na kuyahamishia nchi jirani.

...

Mkuu heshima. Lakini mkuu hata hiyo "nchi jirani" si ina haki au share katika hizo wizara husika? Hata katika EAC makao makuu yapo Arusha, na ninaamini kila nchi mwanachama ina-host angalau Idara mojawapo katika Idara za Jumuiya.

Utaratibu ni huo huo kwa jumuiya zingine za kimataifa kama EU, n.k. Huoni hata hapa kwetu tunge-adopt utaratibu huo ingesaidia sana pengine hata kupunguza kinachoitwa "kero za muungano"?
 
Back
Top Bottom